Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Mimi mwenyewe ni mchawi walahi!
Hahahaha
That’s all!
 
Kama unaamini mungu yupo huwezi kusema uchawi haupo utakuwa ni ujinga mkubwa mno
 
Kama uchawi upo mbona hatuoni wakiwa na maendeleo?,ukifuatilia wengi wao hao wanaoitwa wachawi ndio wanamaisha magumu. Na kama uchawi upo unawasaidia nini? Lol
Una wasaidia kukuhalibia maisha yako maana wanapo kuloga ukaumwa au kukutupia mikosi ndo furaha yao
 
Kwa wasema kuwa uchawi upo ila wachawi hawana maendeleo au haupo kabisa?

Tatizo lako mkuu unataka uchawi wa maendeleko
Wakati siku zote mchawi haendelei
Na hajishughulishi kazi yake ni kumhalibia mtu anaye jishughulisha ili naye asiendelee abaki kama mchawi
 
kwani mtoa mada hujasoma hata utamaduni wa Mtanzania au Afrika ndani yake kuna uchawi. kama huamini kuna uchawi basi nipm majina yako matatu mama matatu correctly, then ulete mrejesho hapa baada ya muda
 
Uchawi ni imani muflis kuwa watu fulani wana nguvu fulani yenye uwezo wa kudhuru wengine. Hili jambo ni imani tu na imani hizo zimejikita katika jamii kweli kweli. Hao waliokuwa wakiitwa au wanaoitwa wachawi katika jamii huwa ni watu dhaifu sana, maskini na waoga wanaodharauliwa sana na jamii. Mara nyingi watu hao wakiitwa wachawi, hawakatai wala kukubali, kwani wengine hufikiria kuwa watu wakimuona ana nguvu hiyo ya ajabu (yaani uchawi) itakuwa ni sababu ya kuheshimiwa na kuogopwa.

Wengi wao hujiingiza katika matendo ya kufanya viinimacho au mazingaombwe ya kuwasadikisha watu kuwa wao kweli wanazo hizo nguvu na wana uwezo wa kudhuru. Kutokana na hilo, wakazaliwa watu wanaoitwa wachawi au walozi. Hawa watu wameanzisha utamaduni wao, kama zilivyo dini. Tofauti yao ni kuwa wao mambo yao hufanyika kwa siri, kwani lengo ni kuwadanganya watu waamini kuwa kweli wanazo nguvu za ajabu.

Hizi jamii za kichawi, kama secrete societies zingine hutoa sadaka na kufanya vitimbi vya hapa na pale vyenye lengo la kuwaaminisha watu kuwa wao wana nguvu zisizoonekana.

Lakini ukweli ni kuwa kama zilivyo jamii zote za siri, mambo haya yanagundulika na walio wengi kuwa si kweli. Wale wanaodanganyika wanabaki kuishi kwa hofu na wakati mwingine enzi hizo watu walilazimika kutoa kitu kidogo kwa wachawi ili wasirogwe. Huo ndo uchawi.

Ukiogopa vitimbi vyao, utajisalimisha kwao na kuwapa kitu kidogo ili wakulinde na uchawi.

Jamii ya wachawi ina umri mrefu kuliko hata dini zetu nyingi, ambazo nazo zimetumia mbinu kama zile zile wanazotumia wachawi kupambana nao. Mbinu wanayotumia wachawi ni kutangaza uwezo wa kudhuru watu kwa kutumia "magic". Dini zinatumia "nguvu za kimungu" kupambana na wachawi. Nguvu zote hizo ni 'supernatural'.

Kwa mtu mwenye scientific knowledge ya mwili wa binadamu na mazingira yake, uchawi ni kama hadithi za riwaya kwake na hauna madhara yoyote!

Huo ndo uchawi!
Nimeipenda hii, lkn nahisi kama una vitu zaidi ya hivi!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]babu yangu alinisimulia hiki kisa kipindi yeye akiwa mlinzi, kumbe muhusika ndo wewe!!!!! anadai alikimbia kama rocket launcher
 
Uchawi (kwa Kiingereza "Witchcraft") ni nguvu zinazotumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansi katika jamii nyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.
Lengo lake ni kujaribu bahati ya mtu na kujilinda na maadui wengine kimazingara, au kwa ajili ya kujifurahisha, japo wenye imani potofu hulichukulia maanani na kupandikiza chuki kwa ndugu jamaa hata jirani kuwa ni mchawi.

Witchcraft or witchery broadly means the practice of and belief in magical skills and abilities exercised by solitary practitioners and groups.

Uchawi upo na watu wanaufanya sana. Cha msingi inategemeana na imani yako katika hili. Kwahiyo serikali yetu haijarasmisha hiyo imani ya kichawi kwa kuhofia mkanganyiko kwa jamii, Pia kuuthibitisha au ushahidi wake ni mgumu kwani ni mazingara fulani
 
kwani mtoa mada hujasoma hata utamaduni wa Mtanzania au Afrika ndani yake kuna uchawi. kama huamini kuna uchawi basi nipm majina yako matatu mama matatu correctly, then ulete mrejesho hapa baada ya muda
Jamaa amekuPM
 
Uchawi ndio misingi yote ya ulimwengu!
B2D22B21-C874-4115-83F4-7581DB901266.jpeg
B2D22B21-C874-4115-83F4-7581DB901266.jpeg
 
Back
Top Bottom