tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,129
uchawi upo kabisa, kuna watu wanatuma radi na wengine huko ukerewe wanafuga mamba na kuwatumia kichawi.
Uchawi ni imani muflis kuwa watu fulani wana nguvu fulani yenye uwezo wa kudhuru wengine. Hili jambo ni imani tu na imani hizo zimejikita katika jamii kweli kweli. Hao waliokuwa wakiitwa au wanaoitwa wachawi katika jamii huwa ni watu dhaifu sana, maskini na waoga wanaodharauliwa sana na jamii. Mara nyingi watu hao wakiitwa wachawi, hawakatai wala kukubali, kwani wengine hufikiria kuwa watu wakimuona ana nguvu hiyo ya ajabu (yaani uchawi) itakuwa ni sababu ya kuheshimiwa na kuogopwa.
Wengi wao hujiingiza katika matendo ya kufanya viinimacho au mazingaombwe ya kuwasadikisha watu kuwa wao kweli wanazo hizo nguvu na wana uwezo wa kudhuru. Kutokana na hilo, wakazaliwa watu wanaoitwa wachawi au walozi. Hawa watu wameanzisha utamaduni wao, kama zilivyo dini. Tofauti yao ni kuwa wao mambo yao hufanyika kwa siri, kwani lengo ni kuwadanganya watu waamini kuwa kweli wanazo nguvu za ajabu.
Hizi jamii za kichawi, kama secrete societies zingine hutoa sadaka na kufanya vitimbi vya hapa na pale vyenye lengo la kuwaaminisha watu kuwa wao wana nguvu zisizoonekana.
Lakini ukweli ni kuwa kama zilivyo jamii zote za siri, mambo haya yanagundulika na walio wengi kuwa si kweli. Wale wanaodanganyika wanabaki kuishi kwa hofu na wakati mwingine enzi hizo watu walilazimika kutoa kitu kidogo kwa wachawi ili wasirogwe. Huo ndo uchawi.
Ukiogopa vitimbi vyao, utajisalimisha kwao na kuwapa kitu kidogo ili wakulinde na uchawi.
Jamii ya wachawi ina umri mrefu kuliko hata dini zetu nyingi, ambazo nazo zimetumia mbinu kama zile zile wanazotumia wachawi kupambana nao. Mbinu wanayotumia wachawi ni kutangaza uwezo wa kudhuru watu kwa kutumia "magic". Dini zinatumia "nguvu za kimungu" kupambana na wachawi. Nguvu zote hizo ni 'supernatural'.
Kwa mtu mwenye scientific knowledge ya mwili wa binadamu na mazingira yake, uchawi ni kama hadithi za riwaya kwake na hauna madhara yoyote!
Huo ndo uchawi!
Hiyo ni sehemu ya mazingaombwe na mauza uza ya kukufanya uamini kuwa kweli uchawi upo. Lakini mwenye akili ya ukweli ulivyo hawezi kutishika eti kwa sababu mtu kachukua viungo vya uzazi vya mnyama. Unaweza kweli kulitumia hili kama kithibitisho cha kuwepo kwa uchawi? Samahani, naona tuko kwenye viwango tofauti mno vya uelewa wa mambo na itakuwa vigumu kueleweshana ikiwa haya ndo madai ya kuthibitisha kuwepo kwa uchawi.
Uchawi ni dhana. Ni dhana inayoishi na watu. Ziko dhana nyingi sana zinazoishi na watu hadi leo. Hata mira nyingi na desturi ni dhana tu ambazo zimejijenga kwa muda mrefu. Nyingine zina sababu za msingi, nyingine hazina sababu yoyote.
Dhana ya uchawi ipo na itaendelea kuwepo kwa sababu mazingira yanayochochea kuwepo kwa dhana hiyo bado yapo. Si ajabu watu wakafanya mauaji, wakasingizia aliyeuawa karogwa! Ila kadri siku zinavyoenda ndivyo watu wanavyozidi kuacha kimoja, kimoja kati ya yale waliyokuwa wakifikiria uchawi unaweza kuyafanya. Mfano imani hizo katika miaka ya 1970 na kurudi nyuma zilikuwa nyingi na nguvu zaidi. Ila leo tunaona maeneo hasa ya mijini hayo mambo yakizidi kukosa mshiko kwani wengi wanaona kuwa ni uongo.
Kusema kuwa uchawi ni uongo, haina maana kuwa hauna madhara. Uongo una madhara mengi mno! Ila silaha ya kupambana na uongo ni kuujua ukweli. Kwenye uchawi, ukweli ni maalifa ya kupambana na matatizo ya kila siku ya binadamu na mazingira yanayomzunguka. Ukishajua mengi kwenye hii, hofu ya uchawi inapungua, ......, hatimaye inaisha. Ikiisha hofu ya uchawi, uchawi umeisha.
Neno uchawi aslil yake ni Biblia, maana halisi ni kuufanyia mwili yale yaliyokinyume na kawaida na hatimaye yakauletea mwili maumivu, mauti, kuvuruga akili au ulemavu. Hivyo basi hata kama umewahi kutoa mimba, kuua mtu, kufamfamyia mtu operesheni (kwa madaktari), kumpa dawa yeyote ikamdhuru mtu huyo, kumfukuzisha kazi mtu kwa majungu, kutoa/ kupokea rushwa, kudanganya, na kama hayo, jihesabie wewe ni mchawi. Haijalishi unatumia gitaa chupa ya pombe, biblia au mazingira gani. GOOD DAY.
Uchawi haupo bana.
Kama uchawi upo mbona hatuoni wakiwa na maendeleo?,ukifuatilia wengi wao hao wanaoitwa wachawi ndio wanamaisha magumu. Na kama uchawi upo unawasaidia nini? Lol
Nini maana ya uchawi?...unaweza kuthibitisha kuwa haupo?
nitathibitisha vipi kitu ambacho hakipo?
Hivi kweli uchawi upo?
hili lipo toka zamani na mataifa yote duniani yanaamini na kufuata UCHAWI,
Nalog off
Nini maana ya mazingaombwe?
na hapo ndipo ninapoiweka sayansi pembeni na kuamini yale nayaonayo kwa macho yangu na yanayothibitisha uwepo wa UCHAWI.Sio kila kitu kinathibitika,hata wanasayansi wanaamini baadhi ya vitu/mambo ambayo kwa vigezo vya kisayansi katu havithibitki.mfano,kwenye mwili wa binadamu kuna organi kadhaa,ila akili haimo na huwezi sema ni ogani,japo ubongo upo,lakini ubongo sio akili.
Wanasayansi wanaamini kuwa kuna saa ya kimaumbile (biological clock) ndani ya viumbe,hususan ndani ya ubongo ingawa saa hiyo haithibitiki kwa vigezo vya kisayansi.
Hivyo basi,kama sayansi inavyoshindwa kuuthibitisha akili kwa vigezo vya kisayansi ndivyo vivo ivyo haiwezi thibitisha uwepo wa Mungu,wala vituko vya shetani kama vile uchawi.
uchawi haupo!!
Hivi kweli uchawi upo?