Je, unaamini kuwa uchawi upo?

mkuu usicomment tu bila kuwa na elimu ya kutosha juu ya unachokicomment, infact uchawi upo uwe na imani ya kikiristo au kiislamu hzo dini zote zmethbitixa kT
uwepo kwa uchaw

Kwani unafikiri dini ni hizo mbili tu.....mmmh
 
cc Free ideas
 
Last edited by a moderator:
Tokea tunakua hadi kufikia sasa tumesikia sana mambo haya mara yule kalogwa mara huyu kaloga akafanikiwa mara yule kalogwa awe chizi, hivi kweli huu uchawi upo au ni story tu zilizoanzishwa na watu waliokuwa hawataki kufikiria nje ya box....??

kama uchawi upo....
1. kwann hao mababu zetu walishindwa kuwaloga wazungu waliokuja kuwafanya watumwa, kuwaasi, kuwatoboa na kuwafunga minyororo??!!, ukisema wazungu walikuwa au ni wachawi je unaweza thibitisha hilo

2 kama uchawi upo mbona lile taifa linalosemekana ni nguli kwa mambo hayo(NIGERIA) wanashindwa kuwaloga hao BOKO HARAM warudishe hao watoto au kufanya ukombozi wowote wa kiuchumi katika nchi yao ifike level za zile za mataifa ya yaliyopo juu

3. kama kweli kuna watu wanapaa usiku na ungo hadi Nigeria kwa dakika moja kwann wasigeuze ungo chombo cha usafiri wawatoze watu pesa kama kwenye ndege inamaana wachawi hawana shida ya pesa, sifa na umaarufu!!

4 kwann wachawi wa Tanzania wanashindwa kuloga ipatikane katiba mpya kwa maslahi yao au kutatua matatizo mengine ya kitaifa

5 kwann Tanzania haitaki kuutambua kisheria!!


kama uchawi haupo

1 . inamaana hawa mitume na manabii wanaofufua watu(misukule) ni waongo??

2. Ni nani aliyeanzisha fununu kuwa kuna uchawi

3 Mababu, na vitabu vyetu vya kiimani vilitudanganya
 
Usingekuwepo hata huo msamiati (uchawi) usingeusikia
 
Asili ya uchawi ni shetani mwenyewe ......Shetani hawezi kujifitini ......umeona wapi ufalme ukijifitini?.....Hivyo Kuroga Boko Haram ambao ni kazi ya shetani pia ni sawa na shetani kujifitini ......Umewahi kusikia mchawi akimroga chizi ? Kwa faida ipi kwa shetani?
 
Uchawi upo tena sana, lakini kufanikiwa kuleta madhara hutegemea imani na hofu ya mlengwa. Usipokuwa na imani ya kudhurika nao hutalogeka abadan.
 

kweli, asili ya uchawi ni shetani.

Mtu ukimwona kwa mbali ana mkuki anageuka akichoma hewani mara chini fikra zinaweza kukutuma anafanya uchawi!

Uchawi hasa ni nini?
 
Mtu anakurupuka na kudai uchawi haupo kwa sababu sayansi imeshindwa kuthibitisha wakati anajua kabisa sayansi hiyo hiyo inakiri kuna isiyoweza kuyajua

Watu wengine wa ajabu sana!

Eiyer tuna watu wengi sana ambao ufahamu wao ni wa kiwango cha chini mno na judgement yao ni majanga kwenye lolote lile its pathetic kwakuwa kwa baadhi yao ni viongozi
 
Last edited by a moderator:
You have nailed it.
 
Mtu anakurupuka na kudai uchawi haupo kwa sababu sayansi imeshindwa kuthibitisha wakati anajua kabisa sayansi hiyo hiyo inakiri kuna isiyoweza kuyajua

Watu wengine wa ajabu sana!
Basi fanya hivi;
Anza kuamini tafiti tu za kawaida ambazo ni wazi kuwa wafanya tafiti hawana sababu za kudanganya.
Hivyo basi tafiti hizo zinaweza kuaminiwa.

CNN wamefanya utafiti na kugundua kuwa asilimia 97 ya watanzania wanaamini ushirikina, nchi zingine za Afrika mashariki zikiwemo Rwanda na Burundi ni chini ya 50% ndiyo wanaamini mssuala ya uchawi.

Utafiti pia ukaonyesha kuwa ni 20% tu ya watanzania ndio wamefikia elimu ya sekondari, Kenya ni 70% ambapo uganda ni 50%, Rwanda ni 40%.

Nakupa tafiti hizi ili ugundue kitu, imani za ushirikina zinaenda sambamba na ukosefu wa elimu.
Asilimia kubwa ya watu wadio na elimu hawaezi kureason, hawawezi kujua sayansi, saikolojia, baiolojia, viini macho na kadhalika.

Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini Ulaya na Marekani hakuna imani za ushirikina?, Albino hawakatwi mikono?
Ni kwa sababu asilimia kubwa ya watu wamepata walau elimu ya sekondari.
 
Sifuri ipo... (mfano kwenye sh. 100,000,000 zipo sifuri 8)

Hata ziwe mia kama hazina namba ya ziada nyuma yake ni bure hapo umeanza na moja zikafuata hizo sifuri ndio imeleta maana
 
Shida moja hapa ni kwamba watu wanachanganya uchawi, ulozi, mazingaombwe uganga wa kienyeji! hivi vyote ni vitu vinavyofanana lakini pia vikitofautiana
 
Eiyer tuna watu wengi sana ambao ufahamu wao ni wa kiwango cha chini mno na judgement yao ni majanga kwenye lolote lile its pathetic kwakuwa kwa baadhi yao ni viongozi

Mkuu we acha tu ...!!
 

Sijui ni kwanini mnakuwa na mawazo kuwa elimu ni kitu cha maana kwa kiasi hicho kwenye maisha ya binadamu wakati hiyo elimu imetoka kwenye mfumo wa kufikiri wa binadamu halafu binadamu asiekuwa na hiyo elimu anaonekana wa ajabu

Elimu,kwa namna ninavyojua mimi elimu ni moja kati ya "zimwi" linalopendwa sana na watu ambalo limewanyang'anya uwezo wao wa kawaida wa kutafakari mambo

Nani amekudanganya Ulaya na Marekani hakuna uchawi?

Danganyaneni wenyewe lakini sio mimi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…