Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Hebu andaa maswali yako yote halafu tukutane live hii mijadala inahitaji uwanja mpana nakaribisha na wengine watakaokuwa tayari nitaleta na zana halisi
Tuandae ukumbi mlimani city au pengine wapi pazuri mkuu unapendekeza?
 
Uchawi na ulozi ni sawa???ushirikina ni nini???
 
Ukitaka kujuA Kama uchawi upo lazima ujue defn yake kwanza
Ukiangalia vizuri hata Simu Mabomu na computer ni uchawi

Ni uchawi kabisa,,sema wameweza kuuelezea tu unafanyaje kazi,hata umeme ni uchawi,simu PIA halikadharika
 
Hakuna tofauti mkuu

vyote vinatumia nguvu za Giza zisizoonekana..

Na zinaweza kuthibitika kwawewe kuamua tu kushiriki kimojawapo
Kwa hiyo uchawi ndio ulozi ndio uganga wa kienyeji au?
 
uchawi...ulozi...uganga ni jamii moja na inatumia nguvu moja ( nguvu za Giza)
Ninachouliza mimi ni hivi;
Mtu akisema ni uchawi, ni amesema ni uganga wa kienyeji na ni sawa na aliyesema ni ulozi?
Hivi vitu havina tofauti?
 
Ninachouliza mimi ni hivi;
Mtu akisema ni uchawi, ni amesema ni uganga wa kienyeji na ni sawa na aliyesema ni ulozi?
Hivi vitu havina tofauti?

Kwa akili hii ya ufipa utapata tabu Sana na maisha post zote mbili umeshindwa pata conclusion?

too low!!
 
Hakuna uchawi simama katika dini yako kiimani zaidii.
 
Uchawi na ulozi ni sawa???ushirikina ni nini???

Vyote vinaangukia katika kundi moja lakini vikifanya kazi tofauti mfano viungo vya mwili vyote viko mwilini lakini kila kimoja kina kazi yake
 
Ni uchawi kabisa,,sema wameweza kuuelezea tu unafanyaje kazi,hata umeme ni uchawi,simu PIA halikadharika

Hapana hapa mnachanganya maarifa yenye maelezo na kitu ambazo hakielezeki uchawi hauna formula ndio maana ukaitwa dark science
 
Uchawi ni shina ambapo matawi yake ni 1.kuwanga/ulozi 2.kufanya ushirikina 3.kuroga 4.kufanya mazingaombwe .....>>> 1.kuwanga ni mtu/watu wenye uwezo wa kichawi kufanya mambo ya kichawi lakini yasiyo na madhara makubwa mfano kuingia kichawi kwenye majumba ya watu wakiwa wamelala na kuwachezea watakavyo kisha kuondoka lengo kubwa ni kujifurahisha na kujiburudisha 2.kufanya ushirikina ni tendo la kichawi lenye nia ya kudhuru mara nyingi likihusisha kuchukua vitu vya mhanga mfano nywele nguo kucha nk 3.kuroga nako ni tendo hilo hilo la kichawi ambalo ni matokeo ya kufanyiwa ushirikina lakini pia hushirikisha na maapizo na kutoa kafara za damu na wanyama 4.kufanya mazingaombwe ni kucheza na akili za watu tu kufanya mambo ambayo si ya kawaida mfano mtu kujichomeka panga katikati ya kichwa nk SASA haya yote hufanywa mchawi (ukiacha mazingaombwe) na mganga wa kienyeji ndio mtaalam wa kutibu
 
Vyote vinaangukia katika kundi moja lakini vikifanya kazi tofauti mfano viungo vya mwili vyote viko mwilini lakini kila kimoja kina kazi yake

Je nchi ikituma kombora la masafa marefu,huo ni ulozi au uchawi?
 
Vyote vinaangukia katika kundi moja lakini vikifanya kazi tofauti mfano viungo vya mwili vyote viko mwilini lakini kila kimoja kina kazi yake

Je nchi ikituma kombora la masafa marefu,huo ni ulozi au uchawi?
 
Kwa akili hii ya ufipa utapata tabu Sana na maisha post zote mbili umeshindwa pata conclusion?

too low!!
Akili ya ufipa ndio ya wapi?
Nitapata tabu sana na maisha kwa sababu nimeshindwa kuelewa ulivyotofautisha ulozi, uchawi na uganga?!!
You must be kidding.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…