Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Walkati mwingine ngoja nikujibu kwasababu inawezkana ukanielewa

Mfano tuchukulie kuna vyombo viwili ambavyo havina uwezo wa kuju yote,chombo kimoja kimeweza kugundua mambo mengi sana lakini kimeshindwa kugundua kama kuna maji kwenye chumba cha raisi

Chombo kingine nacho kimegundua mengi nalakini pia kimeweza kujua kwenye chumba cha rais kuna maji

Vyombo vyote hivi viwili vina wafuasi ambao wanavikubali,wale wafuasi wa chombo cha kwanza wanasema kwenye chumba cha rais hakuna maji kwasababu chombo chao kimeshindwa kujua kama kwenye chumba hicho kuna maji wakati wanajua kuwa chombo chao hakina uweo wa kujua yote

Hawa watu wangekuwa na hoja ya msingi kama chombo chao kina uwezo wa kugundua yote,lakini sio hivyo

Hawa wafuasi wa chombo cha pili wanawashangaa hawa wafuasi wa chombo cha kwanza kwa kuhitimisha maji hayapo kwasababu chombo chao kimeshindwa kufanya hivyo wakati wanajua chombo chao hakina uwezo wa kujua au kugundua yote

Kwa mfano huo naweza kuwa nimeeleweka kwasababu,unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote kwasababu hicho kilichojulikana na mfumo huo ni miongoni mwa vile ambavyo mfumo huo unaweza kujua

Mfano hai ni sayansi,kwasababu haina uwezo wa kujua yote haimaanishi haina uwezo wa kujua baadhi ya mambo,lakini kusema kitu fulani hakipo kwasababu tu sayansi umeshindwa kuyagundua au kuthibitisha ni upuuzi!

Kama umekubali.

Kwa mfano huo naweza kuwa nimeeleweka kwasababu,unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote kwasababu hicho kilichojulikana na mfumo huo ni miongoni mwa vile ambavyo mfumo huo unaweza kujua

Then objection yako ya kuwashangaa wanaotumia sayansi kukataa kuwapo kwa uchawi haina msingi, maana umeivunja kwa kauli yako mwenyewe hiyo ya hapo juu.

Kama unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote, then unaweza kutumia sayansi kujua uchawi haupo na objection yako ni umasikini wa fikra.

Otherwise, you are trying to talk from both sides of your mouth.

To eat your cake and still have it.

Unataka kusema "unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote" halafu hapo hapo uutoe uchawi katika "chochote" bila sababu.
 
Eiyer

Unajuaje kwamba kile kinachoitwa "uchawi" ni uchawi kweli na si mambo yanayoweza kuelezewa naturally tu ambayo labda inawezekana ni miongoni mwa hayo unayosema sayansi haijayajua?

Kabla ya bacteria kugunduliwa na kusomwa kisayansi, mtu ambaye alijua uwepo wa bacteria na kuwa contain vizuri, angeweza kujifanya ni mchawi kwa kuwanyunyizia vitu vyenye bacteria watu wakaugua na kufa.

Kwa watu wasiojua bacteriology wangeweza kukubali huyu mtu ni mchawi ana supernatural powers, wakati ukweli ni kwamba ametumia bacteria tu.

Arthur C. Clarke, one of my favorite Science Fiction author, said "any sufficiently advanced technology is indistinguishable from magic".

Given that tushakubaliana ufahamu wako haujui kila kitu, unajuaje kwamba unachofikiri kuwa ni uchawi ni uchawi kikweli na si mambo tu ambayo yanaweza kuelezewa naturally lakini bado hatujayaelewa vizuri?

Waafrika walivyokutana na wazungu, wazungu ambao walishasoma elimu ya anga na kuweza kutabiri kupatwa kwa mwezi/ jua, wazungu hawa walipowaambia kwamba jua/ mwezi vitapatwa siku fulani, halafu ikatokea hivyo, waafrika waliwaona wazungu hawa kama wachawi na miungu (by the way, etimologically speaking, "mungu" and "mzungu" have the same root).

Sasa wewe unajuaje kwamba unachoona uchawi leo hakina a perfectly natural explanation kama hawa waafrika wa zamani walivyoona the "prediction" of the eclipse of the sun kuwa uchawi wakati ukisoma astronomy kuna charts zinazotabiri kupatwa kwa jua kwa mamia ya miaka yajayo, kwa kutumia sayansi tu, bila uchawi?
 
Last edited by a moderator:

Kama sayansi imeweza kujua uchawi haupo niambie hapa hapa,maana ninawasikia mnasema uchawi haupo kwasababu tu sayansi imeshindwa kuuthibitihsa uwepo wake
Otherwise, you are trying to talk from both sides of your mouth.

To eat your cake and still have it.
Hapana hujaelewa tu,kutokuelewa kwako hakuwezi kufanya nilichoandika kuwa hakieleweki au kiko kama unavyodhani wewe
Unataka kusema "unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote" halafu hapo hapo uutoe uchawi katika "chochote" bila sababu.
Sijautoa uchawi kwenye chochote,lakini huo uchawi nimeshakuambia uhahidi wa uwepo wake upo na sayansi tayari imeshashindwa kuuthibitisha kama upo na ndio maana nikasema kuwa kama kuna ambacho sayansi imeshindwa kukithibitisha sio sahihi mtu kuhitimisha hakipo kwasababu sayansi imeshindwa kuthibitisha kwasababu haijui vyote

Kusema ni kosa haina maana kuwa mimi ninacho ambacho kinajua yote,hapana,inawezekana ninachotumia mimi kuthibitisha uwepo wa uchawi bado na chenyewe hakina uwezo wa kujua yote ila imekigundua au kujua ambacho sayansi imeshindwa kufanya hivyo

Madai yako yangekuwa na maana kama kungekuwa kuna kitu nasema hakipo kwasababu tu nimeshindwa kuthibitisha uwepo wake kwa kifaa au mfumo nilioutumia kuthibitisha uwepo wa uchawi wakati hicho kifaa au mfumo hauna uwezo wa kujua vyote!
 
Kama sayansi imeweza kujua uchawi haupo niambie hapa hapa,maana ninawasikia mnasema uchawi haupo kwasababu tu sayansi imeshindwa kuuthibitihsa uwepo wake

Hapana hujaelewa tu,kutokuelewa kwako hakuwezi kufanya nilichoandika kuwa hakieleweki au kiko kama unavyodhani wewe

Sijautoa uchawi kwenye chochote,lakini huo uchawi nimeshakuambia uhahidi wa uwepo wake upo na sayansi tayari imeshashindwa kuuthibitisha kama upo na ndio maana nikasema kuwa kama kuna ambacho sayansi imeshindwa kukithibitisha sio sahihi mtu kuhitimisha hakipo kwasababu sayansi imeshindwa kuthibitisha kwasababu haijui vyote

Kusema ni kosa haina maana kuwa mimi ninacho ambacho kinajua yote,hapana,inawezekana ninachotumia mimi kuthibitisha uwepo wa uchawi bado na chenyewe hakina uwezo wa kujua yote ila imekigundua au kujua ambacho sayansi imeshindwa kufanya hivyo

Madai yako yangekuwa na maana kama kungekuwa kuna kitu nasema hakipo kwasababu tu nimeshindwa kuthibitisha uwepo wake kwa kifaa au mfumo nilioutumia kuthibitisha uwepo wa uchawi wakati hicho kifaa au mfumo hauna uwezo wa kujua vyote!

Discussion ya uchawi upo/ haupo kimsingi ni ile ile ya mungu yupo/haupo.

Unaondoa "mungu" na kuweka "uchawi".

Kimsingi, mdahalo ni kati ya wanaosema the world operates under natural laws and can be explained naturally and those who say the world, at some level at least, operates under some supernatural influences.

How do you know that what you think is supernatural is merely the not understood natural?

Unajuaje kwamba hicho unachofikiri kuwa ni ushahidi wa uchawi si sawa na wale waafrika wa zamani waliofikiri mzungu kutabiri kupatikana kwa jua ni ushahidi wa uchawi wa mzungu?
 
Eiyer

Unajuaje kwamba kile kinachoitwa "uchawi" ni uchawi kweli na si mambo yanayoweza kuelezewa naturally tu ambayo labda inawezekana ni miongoni mwa hayo unayosema sayansi haijayajua?

Kabla ya bacteria kugunduliwa na kusomwa kisayansi, mtu ambaye alijua uwepo wa bacteria na kuwa contain vizuri, angeweza kujifanya ni mchawi kwa kuwanyunyizia vitu vyenye bacteria watu wakaugua na kufa.

Kwa watu wasiojua bacteriology wangeweza kukubali huyu mtu ni mchawi ana supernatural powers, wakati ukweli ni kwamba ametumia bacteria tu.

Arthur C. Clarke, one of my favorite Science Fiction author, said "any sufficiently advanced technology is indistinguishable from magic".

Given that tushakubaliana ufahamu wako haujui kila kitu, unajuaje kwamba unachofikiri kuwa ni uchawi ni uchawi kikweli na si mambo tu ambayo yanaweza kuelezewa naturally lakini bado hatujayaelewa vizuri?

Waafrika walivyokutana na wazungu, wazungu ambao walishasoma elimu ya anga na kuweza kutabiri kupatwa kwa mwezi/ jua, wazungu hawa walipowaambia kwamba jua/ mwezi vitapatwa siku fulani, halafu ikatokea hivyo, waafrika waliwaona wazungu hawa kama wachawi na miungu (by the way, etimologically speaking, "mungu" and "mzungu" have the same root).

Sasa wewe unajuaje kwamba unachoona uchawi leo hakina a perfectly natural explanation kama hawa waafrika wa zamani walivyoona the "prediction" of the eclipse of the sun kuwa uchawi wakati ukisoma astronomy kuna charts zinazotabiri kupatwa kwa jua kwa mamia ya miaka yajayo, kwa kutumia sayansi tu, bila uchawi?
Ninaweza kusema ni uchawi kwasababu ya definition ya uchawi

Kwa definition ya uchawi ninayoijua mimi ni kuwa;Uchawi ni nguvu ambayo inatumiwa kuumiza au kuua viumbe wengine au hata kuvuruga au kufanya mambo mengine ambayo ni hasi,nguvu hii haiwezi kuonekana lakini unaweza kuona matokeo yake

Nitakupa mifano miwili;

1;Niliwahi kufua nguo siku moja,siku hiyo nilifua nguo zote ambazo zilikuwa ni chafu.lakini nilikuwa shuka za kujifunika zote zilikuwa ni chafu,ilinibidi nifue shuka zingine zote ila nilibakiza moja ambayo niliitumia kujifunika siku hiyo,nilifua na kumaliza jioni saa 12,nilienda kufanya mambo yangu pamoja na kula kwa mama ntilie na usiku nilikuja kulala,siku hiyo mfua ilinyesha sana na kufanya zile nguo pamoja na shuka kulowana upya pale nilipokuwa nimezianika

Kulikuwa na baridi sana niliitumia ile shuka kujifunika na nililala sana siku hiyo,nilistuka alfajiri ya saa 11 na kwenda kuwasha taa ili nijiandae kwenda kazini,nilishtuka baada ya kukuta mezani,yaani kwenye meza iliyokuwepo mule ndani ilikuwa ina sinia ambalo lilikuwa na mabaki ya ugali pamoja na bakuli la mboga ambalo lilitumiwa kulia na waliokula

Mezani kulikuwa kumetapakaa mabaki ya chakula kama ilivyo kawaida ya watu wakimaliza kula,hii imetokea sio mara moja,hili ninawezaje kuelezewaje kisayansi?

Mfano wa pili;
Hapa Mwanza kuna kiwanda cha soda aina za coca kola,pale kuna mashine ya kuzibia pancha,kuna vijana kama wanne ambao wameshafanya kazi pale ambao ninawafahamu,vijana hawa wameishia kupata matatizo ya akili,lakini pia kuna vijana wengine watano pamoja na aliyeko sasa wamefanya kazi na hawajapata matatizo ya akili

Ishu iko hivi,wale vijana ambao wamepata matatizo ya akili makabila yaoni wawili wasukuma na mmoja ni mnyamwezi na mmoja ni msumbwa,hao ambao hawajapata matatizo ya akili ni wajaluo wote

Unaweza kuelezea hili kisayansi?

Mifano iko mingi,lakini ili tukio liwe ni uchawi ni hadi liwe na mazingira yenye sifa ya uchawi kama vile ambavyo wanyama wenye jamii ya paka wana sifa zinazowafanya wawe wa jamii hiyo!
 
Discussion ya uchawi upo/ haupo kimsingi ni ile ile ya mungu yupo/haupo.

Unaondoa "mungu" na kuweka "uchawi".

Kimsingi, mdahalo ni kati ya wanaosema the world operates under natural laws and can be explained naturally and those who say the world, at some level at least, operates under some supernatural influences.

How do you know that what you think is supernatural is merely the not understood natural?

Unajuaje kwamba hicho unachofikiri kuwa ni ushahidi wa uchawi si sawa na wale waafrika wa zamani waliofikiri mzungu kutabiri kupatikana kwa jua ni ushahidi wa uchawi wa mzungu?

Nimekupa mifano miwili kwenye hiyo post hapo juu na hapa nitakupa mfano mwingine

Mama mwenye nyumba wangu mahali ambapo nilikuwa naishi mwaka 2005 aliwahi kupatwa na maradhi ya kichwa,alikuwa anaumwa kichwa sana,alipelekwa hospital ambazo ni Bugando,KCMC na Muhimbili bila mafanikio yoyote yale

Kichwa kiliendelea kumuuma hadi kufikia hawezi kukaa wala kusimama,ndugu na jamaa walishauriana na kuona kuwa kwakuwa wameshaenda sana hospital na kushindwa kupata suluhu ni bora waende kwa waganga wa kienyeji kwakuwa ndio njia mbadala

Kati ya wale ambao walikuwepo kwenye huo msafara wa kumpeleka kwa mganga na mimi nilikuwa mmoja wao,ndugu walikodisha gari na aliyekuwa anatuongoza kwenda kwa "mtaalam" alikaa mbele,mimi na mama mmoja ambae alikuwa ni mdogo wa mgonjwa tulikaa nyuma na mgonjwa huku tukiwa tumemshikilia

Tulitumia kama masaa mawili na nusu hivi kufika kwa mganga na tulipofika tulipokelewa na tulipofika kabla hatujasema lolote mganga yule alituambia shida yetu na alitaja majina yetu pamoja na aina ya ugonjwa ambao mgonjwa tuliempeleka alikuwa anaumwa

Nilistuka kidogo,tulimuingiza mgonjwa ndani na alimfanyia mambo anayojua yeye na alituambia kuwa mgonjwa atapona muda ule ule,alituambia tutoke nje na yeye abaki na mgonjwa

Tulitoka nje na baada ya nusu saa mgonjwa alitoka nje akiwa mzima kabisa,ndugu zake wawili ambao tulikuwa nimeongozana nao waliitwa kwa mganga ambako walilipa gharama na waliambiwa mambo mengine

Mazingira kama haya unaweza kuyaelezaje Kiranga?
 
Umejiridhisha kabisa kwamba hayo yote hayawezekani kwa namna yoyote iliyo perfectly natural bila kuhitaji uchawi?
 
Ninaweza kusema ni uchawi kwasababu ya definition ya uchawi

Kwa definition ya uchawi ninayoijua mimi ni kuwa;Uchawi ni nguvu ambayo inatumiwa kuumiza au kuua viumbe wengine au hata kuvuruga au kufanya mambo mengine ambayo ni hasi,nguvu hii haiwezi kuonekana lakini unaweza kuona matokeo yake

Nitakupa mifano miwili;

1;Niliwahi kufua nguo siku moja,siku hiyo nilifua nguo zote ambazo zilikuwa ni chafu.lakini nilikuwa shuka za kujifunika zote zilikuwa ni chafu,ilinibidi nifue shuka zingine zote ila nilibakiza moja ambayo niliitumia kujifunika siku hiyo,nilifua na kumaliza jioni saa 12,nilienda kufanya mambo yangu pamoja na kula kwa mama ntilie na usiku nilikuja kulala,siku hiyo mfua ilinyesha sana na kufanya zile nguo pamoja na shuka kulowana upya pale nilipokuwa nimezianika

Kulikuwa na baridi sana niliitumia ile shuka kujifunika na nililala sana siku hiyo,nilistuka alfajiri ya saa 11 na kwenda kuwasha taa ili nijiandae kwenda kazini,nilishtuka baada ya kukuta mezani,yaani kwenye meza iliyokuwepo mule ndani ilikuwa ina sinia ambalo lilikuwa na mabaki ya ugali pamoja na bakuli la mboga ambalo lilitumiwa kulia na waliokula

Mezani kulikuwa kumetapakaa mabaki ya chakula kama ilivyo kawaida ya watu wakimaliza kula,hii imetokea sio mara moja,hili ninawezaje kuelezewaje kisayansi?

Mfano wa pili;
Hapa Mwanza kuna kiwanda cha soda aina za coca kola,pale kuna mashine ya kuzibia pancha,kuna vijana kama wanne ambao wameshafanya kazi pale ambao ninawafahamu,vijana hawa wameishia kupata matatizo ya akili,lakini pia kuna vijana wengine watano pamoja na aliyeko sasa wamefanya kazi na hawajapata matatizo ya akili

Ishu iko hivi,wale vijana ambao wamepata matatizo ya akili makabila yaoni wawili wasukuma na mmoja ni mnyamwezi na mmoja ni msumbwa,hao ambao hawajapata matatizo ya akili ni wajaluo wote

Unaweza kuelezea hili kisayansi?

Mifano iko mingi,lakini ili tukio liwe ni uchawi ni hadi liwe na mazingira yenye sifa ya uchawi kama vile ambavyo wanyama wenye jamii ya paka wana sifa zinazowafanya wawe wa jamii hiyo!

Unaweza kuthibitisha kwamba hao waliopata matatizo ya akili hawakupata hayo kwa sababu zinazoweza kuelezewa naturally zisizohitaji uchawi?

Naona kama vile kitu chochote ambacho hujakielewa unakiita uchawi.

Kama wale waafrika wa zamani walioona wazungu wanaotabiri kupatwa na jua kuwa ni uchawi.

Kumbe hawa wazungu wana kalenda za kupatwa kwa jua kwa mamia ya miaka ijayo.

Unathibitishaje kwamba kile unachofikiri ni uchawi leo si kitu tu kitakachoweza kuthibitishwa kuwa si uchawi na kinaweza kuelezewa in a perfectly natural way kikifanyiwa uchunguzi wa kutosha.
 
Nature ni nini?

Nature as in that which is in the realm of logical and explainable laws of science and observable empirically, as opposed to the supernatural which is beyond explanation and empirical examination.

Hujanijibu swali.

Unajuaje unachofikiri uchawi leo kwa sababu kinavuta vyuma hakitaelezewa vizuri tu kesho kama.nguvu ya usumaku inayoelezewa bila kuhitaji uchawi?
 
Hujaona nilichokujibu ulipouliza maana ya uchawi?
 
Unaweza kuthibitisha kwamba hao waliopata matatizo ya akili hawakupata hayo kwa sababu zinazoweza kuelezewa naturally zisizohitaji uchawi?

Naona kama vile kitu chochote ambacho hujakielewa unakiita uchawi.

Kama wale waafrika wa zamani walioona wazungu wanaotabiri kupatwa na jua kuwa ni uchawi.

Kumbe hawa wazungu wana kalenda za kupatwa kwa jua kwa mamia ya miaka ijayo.

Unathibitishaje kwamba kile unachofikiri ni uchawi leo si kitu tu kitakachoweza kuthibitishwa kuwa si uchawi na kinaweza kuelezewa in a perfectly natural way kikifanyiwa uchunguzi wa kutosha.

Jifunze kujibu maswali kabla ya kuuliza swali

Kama unamaelezo ya hiyo hali si uniambie badala ya kuzunguka tu?
 
Hujajibu swali unajuaje kile unachisema ni uchawi leo huoni hivyo kwa ujinga wa mawazo yako tu na kwsho kitaelezewa vizuri bila kuhitaji habari za uchawi?

Nimekuambia uchawi ni nini,findings zozote zitakazoweza kuthibitisha uwepo wa aina ya nguvu nilizozisema hapo juu atakuwa amethibitisha uwepo wa uchawi hata kama ataipa hiyo nguvu jina lingine

Ni sawa na wewe uone maji yakipita kwenye eneo fulani na maji yale ukayaita molongi halafu mimi nikayaita mto,kitu kitakuwa ni kile kile lakini majina tofauti!
 
Wewe umethibitisha uchawi upo?
 
Wewe umethibitisha uchawi upo?

Hii post yangu hapa chini uliiona au husomi ninachokuandsikia?
Kama sayansi imeweza kujua uchawi haupo niambie hapa hapa,maana ninawasikia mnasema uchawi haupo kwasababu tu sayansi imeshindwa kuuthibitihsa uwepo wake

Hapana hujaelewa tu,kutokuelewa kwako hakuwezi kufanya nilichoandika kuwa hakieleweki au kiko kama unavyodhani wewe

Sijautoa uchawi kwenye chochote,lakini huo uchawi nimeshakuambia uhahidi wa uwepo wake upo na sayansi tayari imeshashindwa kuuthibitisha kama upo na ndio maana nikasema kuwa kama kuna ambacho sayansi imeshindwa kukithibitisha sio sahihi mtu kuhitimisha hakipo kwasababu sayansi imeshindwa kuthibitisha kwasababu haijui vyote

Kusema ni kosa haina maana kuwa mimi ninacho ambacho kinajua yote,hapana,inawezekana ninachotumia mimi kuthibitisha uwepo wa uchawi bado na chenyewe hakina uwezo wa kujua yote ila imekigundua au kujua ambacho sayansi imeshindwa kufanya hivyo

Madai yako yangekuwa na maana kama kungekuwa kuna kitu nasema hakipo kwasababu tu nimeshindwa kuthibitisha uwepo wake kwa kifaa au mfumo nilioutumia kuthibitisha uwepo wa uchawi wakati hicho kifaa au mfumo hauna uwezo wa kujua vyote!
 
Habari zenu...
Note:Kuamini kwako au kutokuamini kwako hakufanyi kitu kisiwepo.
Ni hivi ilikuwa siku ya jumamosi nikitoka katika mizunguko yangu ya kusaka maisha pande za Songea nikirudi dar kwa kutumia usafiri wa basi[Superfellow].

Ila tulipofika Kijiji kimoja kinaitwa kiwalala tulikutana na maajabu ya dunia.Tulipofika kiwalala tulikuta watu wengi sana wamezagaa maeneo ya barabara hivyo tulishindwa kuendelea na safari gari likasimama.Baada ya kudadisi kumbe kulikuwa na mkasa wa mambo ya uchawi mambo yalikuwa hivi~

Kuna bibi mmoja aliwapa kibarua mabinti wawili shambani kwake kazi ya kulima shamba lake.Wale mabinti walipofika shambani wakaanza kulima ghafla akatokea nyoka yule binti mmoja akamuuwa,baada ya kumuuwa wakaendelea kulima kabla hawajafika mbali akaja nyoka mwingine baada ya kuja nyoka wa pili akaja na yule bibi mwenye shamba.

Alipofika yule Bibi akamwambia yule binti aliyeuwa nyoka wa kwanza kama unaweza muuwe na nyoka huyu.Wale mabinti wakaanza Kuogopa wakashindwa kumuuwa yule nyoka mwingine.Kuanzia hapo Bibi akaanza kudai nyoka wake yule wa awali/kwanza aliyeuliwa.

Bibi akawa anawadai yule nyoka aliyeuliwa awali na wale mabinti,mabinti wakawa wanalia tu wanashindwa kumpa yule bibi nyoka wake.Ile kesi ilifika hadi serikali ya kijiji lakini cha ajabu yule bibi hakusita kudai nyoka wake.Kesi iligusa wananchi wengi wa maeneo ya kiwalala na viunga vyake.

kwanini bibi alidai nyoka ambaye ameshakufa?
Swali hili lilizunguka katika kichwa changu,ndipo nilipoanza kufanya udadisi kwa wananchi waliko pale.

Kumbe nyoka yule alikuwa ana matumizi mbalimbali katika ulimwengu wa giza.Nyoka aliyeuliwa alikuwa anamiliki vijiji 15 katika maeneo hayo alitumiwa kuuwa watu na kuiba vitu mbalimbali kama vile pesa,Kuku n.k.Pia nyoka huyo alikuwa anakodishwa kwa watu Kwa ajili ya matumizi mbali mbali yaani yule Bibi alikuwa anaishi kwa kutegemea yule nyoka.

Nyoka huyo ni wakawaida kama walivyo nyoka wengine?
Cha kushangaza kumbe yule nyoka hakuwa nyoka kama nyoka wakawaida bali alikuwa ni mtoto wa yule bibi alimfanya msukule kwa kumgeuza nyoka.Serikali ya kijiji ilishindwa kuamuwa kesi hiyo na kuamuru kesi ifike mahakamani.

Alafu kesi hii unaambiwa sio ya kwanza katika kijiji hiki kumewahi kutokea kwa kesi za namna hii nyingi sana hapo kiwalala.Kwa tukio hili nimeamini uchawi Upo.
Nawasilisha kwenu...

critical thinker

Back
Top Bottom