Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Walkati mwingine ngoja nikujibu kwasababu inawezkana ukanielewa
Mfano tuchukulie kuna vyombo viwili ambavyo havina uwezo wa kuju yote,chombo kimoja kimeweza kugundua mambo mengi sana lakini kimeshindwa kugundua kama kuna maji kwenye chumba cha raisi
Chombo kingine nacho kimegundua mengi nalakini pia kimeweza kujua kwenye chumba cha rais kuna maji
Vyombo vyote hivi viwili vina wafuasi ambao wanavikubali,wale wafuasi wa chombo cha kwanza wanasema kwenye chumba cha rais hakuna maji kwasababu chombo chao kimeshindwa kujua kama kwenye chumba hicho kuna maji wakati wanajua kuwa chombo chao hakina uweo wa kujua yote
Hawa watu wangekuwa na hoja ya msingi kama chombo chao kina uwezo wa kugundua yote,lakini sio hivyo
Hawa wafuasi wa chombo cha pili wanawashangaa hawa wafuasi wa chombo cha kwanza kwa kuhitimisha maji hayapo kwasababu chombo chao kimeshindwa kufanya hivyo wakati wanajua chombo chao hakina uwezo wa kujua au kugundua yote
Kwa mfano huo naweza kuwa nimeeleweka kwasababu,unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote kwasababu hicho kilichojulikana na mfumo huo ni miongoni mwa vile ambavyo mfumo huo unaweza kujua
Mfano hai ni sayansi,kwasababu haina uwezo wa kujua yote haimaanishi haina uwezo wa kujua baadhi ya mambo,lakini kusema kitu fulani hakipo kwasababu tu sayansi umeshindwa kuyagundua au kuthibitisha ni upuuzi!
Kama umekubali.
Kwa mfano huo naweza kuwa nimeeleweka kwasababu,unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote kwasababu hicho kilichojulikana na mfumo huo ni miongoni mwa vile ambavyo mfumo huo unaweza kujua
Then objection yako ya kuwashangaa wanaotumia sayansi kukataa kuwapo kwa uchawi haina msingi, maana umeivunja kwa kauli yako mwenyewe hiyo ya hapo juu.
Kama unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote, then unaweza kutumia sayansi kujua uchawi haupo na objection yako ni umasikini wa fikra.
Otherwise, you are trying to talk from both sides of your mouth.
To eat your cake and still have it.
Unataka kusema "unaweza kutumia mfumo usioweza kujua yote kujua chochote" halafu hapo hapo uutoe uchawi katika "chochote" bila sababu.