Je, unaelewa nini kuhusu Ugaidi unaofanywa na mamlaka za Serikali (state sanctioned terror)?

Je, unaelewa nini kuhusu Ugaidi unaofanywa na mamlaka za Serikali (state sanctioned terror)?

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Habari za sikukuu?

Natambua kwamba kwa watanzania wengi hii ni siku kama siku nyingine na kwamba maisha yanaendelea kama kawaida. Natambua pia kwamba kuna ambao wako katika huzuni na pia wapo ambao wako katika furaha. Hayo ndio maisha na inabidi tukubaliane na hali halisi kabla ya kuanza kukabiliana nayo.

Leo nataka nizungumzie kwa uchache kuhusu jambo nyeti sana liitwalo UGAIDI-ambo kwa mujibu wa maelezo anuai ni Vitisho na mashambulizi yanayolenga kutia hofu, wasiwasi pamoja na kuleta taharuki. UGAIDI ni uhalifu unaofanywa na mtu au watu ukiwa na lengo la kuleta hofu kwa watu fulani au jamii nzima. Lengo la ugaidi ni kuleta hofu na taharuki.

Kwa wengi wetu unauchukulia ugaidi kama matendo ambayo yanafanywa na watu wanaopinga mamlaka fulani na wenye maslahi yao binafsi. Na hii ni kutokana na ukweli kwamba vyombo vingi vya habari vimekuwa vikitoa kipaumbele zaidi katika upande mmoja tu wa maelezo bila kuonesha au kutafiti iwapo kuna upande wa pili ambao nao unaweza kuwa na madai ya msingi ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele. Hili linaweza kuwa linafanyika kutokana hofu kwa kujua au kutokujua na wakati mwingine vyomba vya habari vinaweza kuwa sehemu ya mpango mzima wa kuleta hofu.

Kwa kawaida UGAIDI wowote ule ni matokeo ya watu kuto kuridhika na hali ya mambo au kutokana na kuwa na ajenda au mipango binafsi ambayo inawez akufanikiwa kwa kuleta taharuki. Pamoja na hayo huwa kuna aina ya ugaidi ambao huwa unafanywa na taasisi za kiserikali au vikundi vinavyoafadhiliwa nwa serikali au watumishi fulani wa serikali wenye maslahi katika jambo fulani. Huu ni ugaidi unaoitwa STATE SANCTIONED TERRROR ambao huwa ni maarufu sana katika nchi za kibabe ni kidiktea ingawa piwa unaweza kuwepo katika nchi za kidemokrasia.

Katika aina hii ya ugaidi,serikali inaweza kutumia idara za serikali kutishia watu kwa kuwashambulia,kuwaua,kuwateka na hata kutaka mifumo ya kikatiba na kisheria katika namna ambayo itawakandamiza wale ambao wanatofautiana kiitikadi,kimsimamo na kimtizamo dhidi ya serikali. Aina hii ya ugaidi mara nyingi utakuta kuna mgawanyiko wa mtazamo katika jamii kuokana na ukweli kwamba unafanywa na mamlaka halali za nchi na wakati mwingine ni kwa ni ambayo inaonekana ni njema machoni kwa wengi.

UGAIDI huu huweza kuwa wa kutumia mfumo wa kisheria kwa ama kutunga sheria kandamizi na onevu na kisha kuwalenga aina fulani ya watu kwa lengo la kuwafanya washindwe kukosoa na kutoa maoni dhidi ya serikali.Wakati mwingine sheria kandamizi zinaweza kutungwa kwa lengo la kuwatia hofu watu hao na kuweza kuwafuatilia. Mfano wa sheria hizo unaweza kuwa sheria zinazopinga faragha(Anti Privacy Laws) Sheria zinazoruhusu detention without trial,Sheria zinazoruhusu bail denial, sheria zinazo criminize maswala halali na ya kawaida kama vile, haki ya kushirikiana,haki ya kufanya shughuliza za kuingiza kipato, haki ya kupata taarifa n.k..Sheria zote zinawekwa si kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na kijamii bilahuwa zinawalenga watu fulani au makundi fulani katika jamii.

AINA hii ya UGAIDI ndio hupelekea kuzaliwa kwa vikundi vya kigaidi vya nje ya MFUMO ambavyo huwa vinazaliwa kama matokea ya kukosa njia halali za kudai na kupata haki zao na hivyo kujikuta wakilazimika kutumia njia zisizokuwa halali.Kwa lugha nyingine ni kwamba Pale serikali inapozima njia zote halali za kuweza kupata haki basi jamii hulazimika kutafuta njia mbadala ya kupata haki na hapa ndipo vikundi vya KIGAIDI huzaliwa.

Hivyo basi ugaidi ni matokea ya kushindwa serikali katika utawala.Ni ishara ya kwamba serikali imeshindwa kuelewa kila Jamii inataka na hivyo kuamua kutumia nguvu katika kuhakikisha inathibitisha uhalali wake.Pale jamii inapoamua kujizatiti ndipo basi huzaliwa vikundi vinavyoitwa vya kigaidi ambavyo mara nyingi huundwa na watu ambao ni VICTIMS wa UGAIDI wa SERIKALI.

Ninchotaka kusisitiza hapa ni kwamba UGAIDI mwingi huanza na kutokuridhika kwa watu na mfumo wa haki wa nchi na ni matokea ya STATE SANCTIONED TERROR.Vikundi hivi hujikuta vikilazimika kutumia UGAIDI kama namna pekee ya kuhakikisha madhila yao yanasikika.

Itoshe tu kusema kwamba, tusikae kimya tunapoona Jamii yetu na serikali yetu inavunja haki kwa uwazi kabisa kwani matokeo yake yanaweza kuwa mabaya hasa kutokana ukweli kwamba kila mwanadamu anataka kutendewa HAKI.

Niwatakie Maisha Mema.
 
"AINA hii ya UGAIDI ndio hupelekea kuzaliwa kwa vikundi vya kigaidi vya nje ya MFUMO ambavyo huwa vinazaliwa kama matokeo ya kukosa njia halali za kudai na kupata haki zao na hivyo kujikuta wakilazimika kutumia njia zisizokuwa halali"

Mkuu, Mungu akubariki sana kwa hoja murua kabisa. Kwa maana watawala wameamua kushupaza shingo zao, kwa sababu ya kiburi cha uzima na nguvu za dola walizokuwanazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ubongokid,
Hapa ndipo naikubali JFs, full madini yaaani. JFs haichoshi...

Tayari ya kwetu ishakuwa Full Sanctioned na Watu waleeee...
 
Mungu aepushie mbali kuzaliwa kwa hivyo vikundi vidogo vidogo vya kigaidi ingawa kuna viashiria vya mamlaka husika kujianzishia hiyo "Sanctioned State Terror" kwa makusudi au kwa kutokujua.

Inafahamika fika tutakaoumia zaidi ni sisi wananchi wa kawaida na tusio na hatia! huku wale waliosababisha hiyo hali kutokea, wakijiimarisha zaidi kiulinzi ili kulinda nafsi zao na zile za wapendwa wao.
 
Mungu aepushie mbali kuzaliwa kwa hivyo vikundi vidogo vidogo vya kigaidi ingawa kuna viashiria vya mamlaka husika kujianzishia hiyo "Sanctioned State Terror" kwa makusudi au kwa kutokujua.

Inafahamika fika tutakaoumia zaidi ni sisi wananchi wa kawaida na tusio na hatia! huku wale waliosababisha hiyo hali kutokea, wakijiimarisha zaidi kiulinzi ili kulinda nafsi zao na zile za wapendwa wao.
Tusiposema sasa hawatajua
 
Tusiposema sasa hawatajua
Mkuu umeongea ukweli usioacha shaka kwenye post yako namba moja. Mada kama hizi ni chache sana siku hizi hapa jukwaani. Ni vyema watu wenye upeo mpana kama nyie wangalau kila mwezi msiache kumwaga nondo nzito za hivi. Dalili zote ulizosema kwenye post mama zipo hapa nchini, na baadhi zimeshaanza.

Ni hatua sasa ya vikundi vya kigaidi kujiunda na kudai haki, maana njia halali zimezibwa, na watawala wanatuaminisha tutii sheria ambazo wanazitunga ili kutukandamiza.
 
ubongokid,
Vijana wetu "wasomi" sijui wakoje!? Yaani mtu anaandika maelezo marefu na mazuri na ambayo anataka atuaminishe yapo kwenye jamii zetu. Lakini cha ajabu, hakupi mfano au mifano ya anachokiongelea. Sasa unabaki unajiuliza, ameyatoa wapi? Kama yapo, yapo nchi gani? Wasomi wetu bwana!
 
ubongokid,

Kwahio wamaanisha hivo vikundi vyinazozalishwa nje ya mfumo vyaweza kuitwa pia majina kama Special Task force, auxialiiary force, killing squads na vingine.

Watu kama Pol Pot na jenerali Pinichet walikuwa na vikundi kama hivi na sidhani kama Tanzania kama nchi tupo kwenye stage ya akina Pol Pot na jenerali Pinochet.

Lakini usisahahu kwamba hivi vikundi pia vinapamabana na kikundi vingine kutoka upande wa pili au kwa jina la mercenaries au jeshi au kundi la kukodi kwa muda maalum.

Hitilafu ikitokea au kutofautiana itikadi ndio ajenda kuu huchangaywa na mtu kama TL akiwekwa kati huleta utata nani ni mhusika halisi.

Mercenaries wanafadhiliwa na vyanzo vya nje au "external sources" na hawana mipaka katika maamuzi na utendaji wa kazi zao.

Hizi external sources ni lazima kwa sababu ni ngumu kupata fedha za uendeshaji kwa kutumia vyanzo vya ndani kutokana na umakini wa vyombo vya fedha na mamlaka za mapato pamoja na ukaguzi wa lazima ulowekwa kisheria.

Hivyo kwa maoni yangu naona mada yako ni muhimu sana lakini ungeainisha mpambano huu wa chini kwa chini baina ya makundi haya mawili.

Yaani kundi la sponsored state terorrists na vikundi viingine vya pembeni dhidi ya kundi la mecernaries na mawakala wengine mbalimbali.

Hii ni vita hivyo weka mada iwe pana na ioneshe pande mbili.

Kheri ya Christmas.
 
Tunaogopa hata ku comment thread kama hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila Wasukuma huwa wana misemo inayoniacha hoi: eti mji wa mwoga nao ni mji: "Kaya ya ng'woba nayo Kaya." Waswahili wao husema 'kunguru mwoga hukimbiza bawa lake.'

Yaani hata wewe una mji huenda na mke na watoto wanaokuita baba ila huna tofauti na mtumwa tu!!!
 
Vijana wetu "wasomi" sijui wakoje!? Yaani mtu anaandika maelezo mareeeefu na mazuuuuuuri na ambayo anataka atuaminishe yapo kwenye jamii zetu. Lakini cha ajabu, hakupi mfano au mifano ya anachokiongelea. Sasa unabaki unajiuliza, ameyatoa wapi? Kama yapo, yapo nchi gani? Wasomi wetu bwana!
Wewe utakuwa ni 'spin doctor.' Lengo lako si kuujua ukweli wa uzi huu bali kutufanya wasomaji tuone kilichoandikwa hakituhusu Tanzania.

Ni hivi yote yaliyoandikwa yanaihusu Tanzania hii ya serikali ya awamu ya tano. Hivi kama Polisi wanakamata watu kama vibaka mchana kweupe kisha kuwanyima haki zao za kisheria, hadi kelele zipigwe ndipo wawapeleke mahakamani, kama huo siyo ugaidi nini hasa!!?

Kwa kawaida huwa wanaanza wao kisha raia wakichoka wanamalizia.
 
Wewe utakuwa ni 'spin doctor.' Lengo lako si kuujua ukweli wa uzi huu bali kutufanya wasomaji tuone kilichoandikwa hakituhusu Tanzania.
Ni hivi yote yaliyoandikwa yanaihusu Tanzania hii ya serikali ya awamu ya tano. Hivi kama Polisi wanakamata watu kama vibaka mchana kweupe kisha kuwanyima haki zao za kisheria, hadi kelele zipigwe ndipo wawapeleke mahakamani, kama huo siyo ugaidi nini hasa!!?
Kwa kawaida huwa wanaanza wao kisha raia wakichoka wanamalizia.
Kilichomshinda kusema haya yapo Tanzania na akatoa mifano ni nini? Je, kama anaogopa hata kuitaja Tanzania kwenye mifano yake, tutarajie nini kwa kijana kama huyu? By the way, uliishawahi kusoma kitabu cha "Harakati za Ukombozi"?
 
Back
Top Bottom