Je, unaelewa nini kuhusu Ugaidi unaofanywa na mamlaka za Serikali (state sanctioned terror)?

Je, unaelewa nini kuhusu Ugaidi unaofanywa na mamlaka za Serikali (state sanctioned terror)?

Huu uzi kwangu umenifungia mwaka vizuri, kwani umejaa ukweli kwa 100%.Serikali iliyoshindwa kuongoza huanza kugombana na wananchi wake. Serikali ya magufuli imeshindwa kuongoza nchi.
 
Kilichomshinda kusema haya yapo Tanzania na akatoa mifano ni nini? Je, kama anaogopa hata kuitaja Tanzania kwenye mifano yake, tutarajie nini kwa kijana kama huyu? By the way, uliishawahi kusoma kitabu cha "Harakati za Ukombozi"?
Mkuu acha kuhema sana,Shusha Pressure,Soma taratibu na hakikisha unaelewa kabla ya kucomment.Kwa unataka niandike kama unavyotaka wakati mimi nmeandika nilivoandika na wewe umeelewa?Huna haja ya kuwa na matarajio yoyote kutoka kwangu zaidi ya kusoma huu uzi na kuuelewa.
 
Ila Wasukuma huwa wana misemo inayoniacha hoi: eti mji wa mwoga nao ni mji: "Kaya ya ng'woba nayo Kaya." Waswahili wao husema 'kunguru mwoga hukimbiza bawa lake.'
Yaani hata wewe una mji huenda na mke na watoto wanaokuita baba ila huna tofauti na mtumwa tu!!!

Tumeshuhudia watu wakitekwa na kutoweka au kushambuliwa kwa silaha na kuuwawa mchana kweupe!

Kuna mifano hai kama kutekwa kwa Mo Dewji, kutoweka kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na kushambuliwa kwa Tundu
Lissu na kifo cha Alphonce Mawazo n.k.

Kitu ambacho ni very interesting hapa ni kwamba wanaofanya ugaidi huu ni kundi la WATU WASIOJULIKANA ambao wako smart kuliko Policcm, smart kuliko TISS na smart kuliko JWTZ maana hawajawahi kukamatwa wala kushtakiwa popote…! Kwa kawaida ya Magaidi wakifanya shambulio, utekaji au mauaji hujitangaza kama Al-shaabab, Boko Haram, Islamic Jihad au Black September n.k…!
Swali ni: Je, hili ni kundi gani la Magaidi hapa Tanzania?
 
Mkuu acha kuhema sana,Shusha Pressure,Soma taratibu na hakikisha unaelewa kabla ya kucomment.Kwa unataka niandike kama unavyotaka wakati mimi nmeandika nilivoandika na wewe umeelewa?Huna haja ya kuwa na matarajio yoyote kutoka kwangu zaidi ya kusoma huu uzi na kuuelewa.
This is rubbish. Na una bahati hii sio kama assignment ambayo ningeweza kuisimamia mimi. Ungeramba sifuri, lakini kwasababu hii ni JF andika unavyoweza na wajinga wenzako watakupongeza!
 
Richard, Kwa makusudi unataka kupotosha. Ukweli ni kuwa kundi moja muhimu ni "state sponsored." Hapa tunazungumzia nchi ambazo zinaminya haki za watu. Hizi zinaweza kuwa za kidikteta au zile za kidemokrasia zisizo na agenda ya Utawala. Tawala hizi huunda vikundi nje ya mfumo au hata kutumia watu wa mfumo rasmi kukandamiza haki za wengine hasa zilizo halali kisheria. Pia hutumia mifumo dhaifu ya kikatiba Kama Bunge na mahakama kutengeneza sheria kandamizi ili kupata mwanya wa kukandamiza wengine. Hatimaye wanaokandamizwa wata - retaliate. Hivyo nao kutafuta njia zisizo rasmi na kuanzisha mapambano.

Nakumbuka miaka ya nyuma makaburu walipokuwa wakiwasaka wana ANC kama magaidi. Hii ni kwa sababu milango ya siasa za wazi ilifungwa. ANC wakawa hawana namna ila kutumia "Umkhoto we Sizwe." Hata katika kesi maarufu ya Revonia, Mandela alishtakiwa si Kama mpigania uhuru, Bali gaidi na mhaini.

Leo unapomsikia mtu aliyevuruga uchaguzi wa serikali za mitaa akitamka hadharani bila majuto kuwa ' hata kususia uchaguzi nayo ni demokrasia,' unategemea upande wa pili ufanye nini hasa.

Watakuja na Moto: 'No hate, no fear,' ila mwisho wa siku ni mapambano ya ukweli yasiyo na mapambio.
 
This is rubbish. Na una bahati hii sio kama assignment ambayo ningeweza kuisimamia mimi. Ungeramba sifuri, lakini kwasababu hii ni JF andika unavyoweza na wajinga wenzako watakupongeza!
Mkuu,nafikiri unahitaji kula ndimu/limau.Hio sio assignment wala sitafuti maksi hasa kutoka kwa mtu kama wewe ambaye sidhani kama una hadhi hata ya kuwa mwanafunzi wangu wa mwisho darasani kwa sababu mwanafunzi wangu wamwisho hawazu kuwa na fikra fupi kama zako.

Usikosse heshima JF nafikiri wewe utakuwa ndo mjinga pekee uliopo JF ambaye unalengo moja tu kuhakikisha unahamisha msing na uelekeo wa mjadala jamba ambalo umelifanikisha.Mengine nafikiri ushayaelewa vizuri.Kunywa maji ushushie
 
Mkuu,nafikiri unahitaji kula ndimu/limau.Hio sio assignment wala sitafuti maksi hasa kutoka kwa mtu kama wewe ambaye sidhani kama una hadhi hata ya kuwa mwanafunzi wangu wa mwisho darasani kwa sababu mwanafunzi wangu wamwisho hawazu kuwa na fikra fupi kama zako.Usikosse heshima JF nafikiri wewe utakuwa ndo mjinga pekee uliopo JF ambaye unalengo moja tu kuhakikisha unahamisha msing na uelekeo wa mjadala jamba ambalo umelifanikisha.Mengine nafikiri ushayaelewa vizuri.Kunywa maji ushushie
Ahahahahahaha! Lingekuwa jambo jema kama ungeuchukua ushauri wangu na kuufanyia kazi. Ukiucha, shauri yako!!!
 
Kilichomshinda kusema haya yapo Tanzania na akatoa mifano ni nini? Je, kama anaogopa hata kuitaja Tanzania kwenye mifano yake, tutarajie nini kwa kijana kama huyu? By the way, uliishawahi kusoma kitabu cha "Harakati za Ukombozi"?
Uandishi wa kifasihi humfanya msomaji afikiri nje ya box. Si lazima kutaka mifano halisi. Hilo huachiwa msomaji kuamua hujiwekea mifano mingi awezavyo.
Nitakitafuta kitabu hicho, ila unajuaje kama mwandishi wa bandiko hili ni kijana!!!? Labda ni Mzee wa mkongojo au wa kiume au kike!!?
 
Zakaria Lang'o,

Nimeandika kwa uwazi kabisa na wala sijapotosha kitu hapo.

Umeongelea pande mbili za Makaburu (wakandamizaji) na ANC (wakandamizwaji)

Kundi moja Makaburu lilikuwa llikikandamiza na pia kusaidiwa na mataifa ya nje na ANC nao walikuwa wakisaidiwa na hata kuwa na kambi mpaka Morogoro.

Usijidanganye kwa kuamini kwamba kwa kuwa udikteta unaitwa kwa mataifa fulani lakini pia upo kwa namna ingine katika mataifa ambayo wewe unaamini kuwa hayana udikteta na hivyo vikundi vya kusaka wanaokosoa serikali.

Fuatilia kwa uzuri mkasa wa Hispania na jimbo la Catalonia la kutaka kujitenga na jinsi kiongozi wao wa harakati alivyopelekeshwa mpaka kufungwa jela.

Hivyo ni sawa kabisa na nilichokieleza.
 
Uandishi wa kifasihi humfanya msomaji afikiri nje ya box. Si lazima kutaka mifano halisi. Hilo huachiwa msomaji kuamua hujiwekea mifano mingi awezavyo.
Nitakitafuta kitabu hicho, ila unajuaje kama mwandishi wa bandiko hili ni kijana!!!? Labda ni Mzee wa mkongojo au wa kiume au kike!!?
Mkuu, katika uandishi, unapoelezea jambo Fulani ili kuthibitisha kiwa lipo lazima utoe mfano/mifano. Kama hutoi so rahisi kuthibitisha kiwa lipo. Kwahiyo, nilichokuwa namtaka mwandishi kufanya ni kutoa mfano/mifano tu. Kama anaogopa kutoa hiyo mifano maana yake anachokiogea HAKIPO!! Hili ni jambo la kawaida kwenye uandishi!
 
Richard, Hapo kwenye vyanzo vya fedha umesahau jamaa alishaweka sheria inayozuia baadhi ya vyanzo vya mapato kukaguliwa kama Fedha za madini, Vocha za 19, 20 hazikaguliwi na mtu yeyote a hazihojiwi so zaweza kutumika kwa namna anavyotaka.

Na ni ukweli kuwa vikundi hivi ya wasiojulikana viko well finacially supported, vina nyenzo na mafunzo makali.
 
Back
Top Bottom