Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 489
FFU ni sehemu ya Jeshi la Polisi ambacho chimbuko lake ni kikosi tangulizi cha askari 31 wa Jeshi la Polisi la Makaburu wa Afrika Kusini, chini ya Major Stephen T. Davies, kilichoazimwa kutoka vikosi vya msituni vya majeshi ya Afrika Kusini. Waliletwa nchini mwaka 1918 na wakoloni wa Kiingereza kuwadhibiti wananchi waliothubutu kuhoji utawala wa kikoloni na utumikishaji katika miradi yao ya kiuchumi.
Askari hao walianzia kituo cha mji wa Wilhemstal [sasa Lushoto] kwa sababu eneo hili lilikithiri kwa Wazungu kupora ardhi ya wananchi, kuanzia na Wajerumani, ambapo kufikia mwaka huo, kulikuwa na idadi kubwa ya jamii ya Masetla waliopora maeneo makubwa ya ardhi. Kwa sababu hii, kulikuwa na kila hatari kwao kuvamiwa, au kuibukakwa maasi kutoka kwa Waafrika waliopokonywa ardhi. Hivyo kuwepo kwa Vikosi vya FFU kulitarajiwa kuleta hali ya utulivu kwa njia ya matumizi ya nguvu.
Ikumbukwe kwamba, Makaburu wa Afrika Kusini walirithisha Jeshi la Polisi la Tanganyika, muundo wa utawala uliozingatia ubaguzi wa rangi, ambapo askari wa Kizungu walibeba vyeo vyote vya juu; Waasia walichukua vya kati na Waafrika waliambulia vyeo vya chini. Kwa hiyo, siku zote amri kwa FFU za kuwanyuka Waafrika zilitoka kwa Maafisa wa Kizungu na Kiasia wasiokuwa na uchungu na hatima ya Mwafrika wala kudumisha haki hadhi yake ya kijamii. Askari kamchoche hao wa Kiafrika, walitumika kuwanyuka na hata kuwaua baba zao na mama zao kwa kutii amri halali za mabosi wao.
Kuna tofauti gani kati ya leo na enzi hizo, ambapo askari waliua na sasa wanaendelea kuua raia wasio na hatia mijini na vijijini kwa amri halali za Mabosi wao, wakati wakuu hao wakila kuku kwa mrija kwenye ofisi zenye viyoyozi mijini? Uko wapi usawa na haki za binadamu, kwa mwananchi masikini, ambaye jasho lake ndiyo maji yake ya kuoga, na jembe la mkono ndilo gitaa la kuliwaza fikra zake; asiyechuma lakini anahenya miaka nenda miaka rudi; aliyefukarishwa na mifumo ya uchumi kandamizi na uwekezaji usiojali; anapigwa mabomu, na pengine risasi za moto na kuuawa kwa sababu tu ya kuandamana kudai mabadiliko dhidi ya mifumo kandamizi na demokrasia ya kiuchumi na kijamii?
Uporaji ardhi hadi utumikishaji wanyonge
Baada ya Vita ya Pili ya Dunia [1918 1945], na kufuatia Usetla kuota mizizi, Serikali ya Wakoloni ilikabiliwa na adui mpya, kutoka adui mpwa zamani, kwa maana ya Mwafrika mpambanaji dhidi ya uporaji wa ardhi, hadi adui mpya wa upambanaji dhidi ya uonevu, utumikishwaji na kudhalilishwa. Kipindi hiki kilishuhudia kuibuka na kushamiri kwa vyama vya Wafanyakazi kupambana dhidi ya maovu hayo; na hivyo haraka sana, Serikali ya kikoloni ikanusa hatari ya maasi, migomo yenye machafuko na isiyo na machafuko ya Wafanyakazi nchini.
Hali hii ilisababisha kuanzishwa kwa Kikosi cha Polisi chenye uwezo wa kukabiliana na machafuko kama hayo, kama si kuyazima kabisa kabla ya kuibuka. Kikosi hicho kiliundwa kwa misingi na kwa muundo ule ule wa Kikosi cha S. T. Davies cha mwaka 1918; na kikapewa jina hilo hilo: Field Force Unit -FFU.
Wafanyakazi waliishi na kufanyakazi mijini, na katika mashamba makubwa, na pia katika mashamba ya Masetla na Migodi. Kwa hiyo, vikosi vya FFU hawa vichwa maji, viliwekwa katika maeneo muhimu ambako vingeweza kujitosa kwa urahisi na kwa haraka sana kwenye maeneo yaliyodhaniwa kuwa hatari na hatarishi. Kwa msingi huo, Dar es Salaam iliwekewa vikosi viwili; wakati mjini Moshi, Tanga, Mwanza na baadaye Iringa, Morogoro na Mbeya, kulikuwa na kikosi kimoja kimoja. Ilivyokuja kutokea, ni kwamba shughuli za kikosi hiki hazikuishia kuzima maasi ya wafanyakazi pekee, bali kilitumika pia kunyamazisha wakulima na wanaharakati za uhuru kipindi hicho cha ukoloni nchini.
Source: Joseph Mihangwa, Raia mwema No 263.