Je unafahamu hili kuhusu makucha yako?

Je unafahamu hili kuhusu makucha yako?

Joined
Jul 9, 2015
Posts
23
Reaction score
2
Binadamu tunatumia pesa nyingi sana kutunza makucha yetu, bila kuzingatia ya kwamba hamna kitu chochote kile utakacho nunua chenye kufanya makucha yako yakue haraka na kuwa imara.

Makucha yana seli iliyokufa kwahio hamna 'growth formula' au 'nail builder' ambayo itasaidia yaote haraka. Dawa hizi sio tu hazisaidii bali ukali wake huweza kuleta madhara ya kuzidhoofisha makucha yako. Madaktari tunashauri njia bora ya kupata makucha yenye afya ni kuyasafisha na kuyapunguza urefu mara kwa mara pamoja na kukwepa kutumia kemikali na sabuni za kufulia kali. Pia kupata lishe nzuri.

Mwisho nakushauri kuvaa gloves kulinda makucha yako unapofanya kazi za nyumbani zenye kuhitaji ushike maji mengi /sabuni kali/kemikali....

Niko tayari kutoa somo kwa upana zaidi ya jinsi ya kutunza makucha yako;

Mfano
-Unajua Nail polish haitakiwi kupakwa kwenye mwanzoni kabisa wa kucha maana itaziba seli iliyo hai?
-Nail polish remover inatakiwa kutumiwa mara moja tu kwa wiki maana ina kemikali inayo kausha na kudhoofisha makucha?......

Nifollow kwenye account yangu ya Instagram @ daktari_sundae
 

Attachments

  • unnamed (14).jpg
    unnamed (14).jpg
    15.4 KB · Views: 79
Back
Top Bottom