Je, unafahamu kwamba kuna Bunge la Bajeti linaendelea Dodoma?

Je, unafahamu kwamba kuna Bunge la Bajeti linaendelea Dodoma?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Wewe kama mwana Jf unafahamu kwamba wabunge wapo bungeni kujadili bajeti ya nchi?

Tangu bunge lianze kujadili bajeti umefuatilia na kuona mjadala wowote wa kibajeti? Kwa namna mambo yanayokwenda kwanini tusiachane na mfumo wa kupeleka bajeti bungeni?

Nasema tuachane nao kwa sababu fedha nyingi zinatumika kwenda Dodoma bungeni kupitisha kushuhudia jambo ambalo lingeweza kuwa declared once na waziri wa fedha tukaendelea na maisha.

Mfuko huu wakusoma bajeti ambayo hakuna mbunge anayechambua bajeti husika umepelekea kufa kwa lengo la bajeti kupita bungeni. Hata wabunge kwenye viti vyao hawapo wapo busy na mambo mengine.....tunapeleka bungeni kwa ajili ya nini?
 
Mimi huwa naangalia kupitia tv ya ofisini tu. kinachoendelea pale ni ujinga uliopitiliza. wale wabunge wamemezeshwa desa la KUMSIFIA RAISI SAMIA, YANI KILA ANAYESIMAMA ANAONGEA KAMA ALIYEPITA BORA HATA HAO KINA MSUKUMA
 
mbunge anayechambua bajeti husika umepelekea kufa kwa lengo la bajeti kupita bungeni
Bunge lililijaa asilimia zaidi ya 95 % wabunge wa chama dola kongwe.

Tutizame nchi jirani kulipo na mchanganyiko wa wabunge toka vyama mbalimbali

15 May 2024
Nairobi, Kenya

Muungano Wa Azimio Sasa Unatishia Kuandaa Maandamano Kote Nchini Kupinga Mswada Wa Kifedha Wa Mwaka 2024. Katika Mkutano Wa Kujadili Mapendekezo Ya Nyongeza Ya Uhsuru Katika Mswada Huo, Kinara Wa Wiper Kalonzo Musyoka Amedokeza Kuwa Upinzani Hautakubaliana Na Serikali Kupitisha Mswada Huo Na Kuwataka Wabunge Wote Wa Azimio Katika Bunge La Kitaifa Kupinga Mswada Huo Utakapofikishwa Bungeni.


View: https://m.youtube.com/watch?v=fZtheoYH-tE

15 May 2024
Nairobi, Kenya

Rais William Ruto ametetea hatua ya serikali kuongeza ushuru maradufu akisema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza mapato ya kitaifa na kupunguza hulka ya kutegemea mikopo. Ruto amesema kuwa ananuia kuongeza ushuru kutoka asilimia 14 hadi kumi na sita kufikia mwisho wa mwaka huu, lengo kuu likiwa kufikisha ushuru wa asilimia 22 atakapoondoka kama rais.

View: https://m.youtube.com/watch?v=4-3gfUEF7oo
 
Abas Tarimba anazungumza muda huu

Hivi waliopo karibu na abas huwa anatumiaga KILEVI CHOCHOTE

MAANA NAVYO MWONA KAMA YUPO HIGH

anae jua atuambie..
 
Bungeni kodi, tozo zikipanda wahawataki kusema katika magazeti rais Dr. Samia Hassan amepandisha kodi, wakati Bill / mswada wowote wa fedha hauwezi kufikshwa bungeni Dodoma bila rais kuridhia na hata ukipitishwa pia lazima rais aidhinishe kwa kusaini

KENYA MEDIA HAZIPINDISHI, RAIS NDIYE ANAYELETA MAPENDEKEZO KTK MSWADA WA FEDHA

Kenya serikali ikipandisha kodi wanasema bila kupepesa macho rais William Ruto kupandisha kodi, tozo ...

Rais Ruto kuongeza ushuru kutoka asilimia 14 hadi asilimia 22


View: https://m.youtube.com/watch?v=4-3gfUEF7oo
 
Tujikumbushe umuhimu wa bunge kuwa na kambi ya upinzani iliyo na wabunge wengi.

Wabunge kambi ya upinzani bila kupepesa macho walitumia jina rais rais katika kila kipengele cha muswada wa fedha / finance bill kuelezea majukumu na mamlaka ya rais katika kuongeza kodi, kuanzisha kodi mpya, tozo, makato n.k lakini spika Ndugai alikataa hotuba hiyo ya upinzani ingawa iliandikwa kwa kufuata katiba kuwa ni rais pekee ndiye mwenye mamlaka katika miswada yote ya kodi n.k inayoletwa bungeni Tanzania .... lakini spika hakupendezwa rais kutwikwa mzigo wa miswada ya kodi kama katiba inavyosema

TOKA MAKTABA 2020 BUNGE LA BAJETI HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI

 
Wewe kama mwana Jf unafahamu kwamba wabunge wapo bungeni kujadili bajeti ya nchi?

Tangu bunge lianze kujadili bajeti umefuatilia na kuona mjadala wowote wa kibajeti? Kwa namna mambo yanayokwenda kwanini tusiachane na mfumo wa kupeleka bajeti bungeni...
Wamesambaa nchi nzima kugawa mikopo walioipa jina "mikopo ya akina mama". Na sijui mapesa haya wameyatoa wapi.

Kila Mbunge anayo mapesa haya.

Je, ni posho zao? - JIBU NI HAPANA, HAIWEZEKANI. CCM hawana huruma hii!!

Je, ni mapato ya kazi za biashara zao? - JIBU NI HAPANA, HAIWEZEKANI, CCM hawana huruma hii!!

Je, ndiyo mapesa ya Mama Abdul kupitia kwa Mwigulu Nchemba kwa kuchota toka hazina ya nchi? - HILI LAWEZA KUWA NDILO JIBU SAHIHI


Hii serikali ya CCM na Mama Abdul wao iko desperate kulinda madaraka yake kwa hongo na rushwa kwa wananchi, wakati huohuo huduma za kijamii kwa watu wote elimu, afya, miundo mbinu ya barabara, umeme, nk zikiwa choka mbaya.

Aidha, funding ya miradi ya kimkakati kama SGR, barabara, maji ikiwa imesimama na wakati huohuo gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida na masikini kabisa wa nchi hii zikipaa juu kuliko kawaida kila siku!!

Honestly, THIS IS UNACCEPTABLE!

Hata hivyo, ukweli ni kuwa hii inayotolewa sio mikopo bali ni rushwa na hongo kwa kina mama kwa ajili ya kura mwaka huu 2024 na mwaka kesho 2025.

Wabunge wamesambaa nchi nzima kugawa hongo na rushwa kwa jina la "mikopo". Hivi kama nchi tutapataje kupona kama hawa watu waliobeba roho hii chafu ya Ibilisi shetani wakiachwa kutawala taifa na nchi hii?

Tumejenga utamaduni mbaya wa kuwapa uongozi wa nchi watu wanaonunua uongozi kwa rushwa. Hii ni tabia ya shetani si ya Mungu Yehova mwenye nchi hii.

Tunaposema tunatawaliwa na viongozi mawakala wa shetani, maana yake ni hii!!

Tutawezaje kupiga hatua za maendeleo kwa kuwa na viongozi watoaji na wala rushwa namna hii?
 
Wewe kama mwana Jf unafahamu kwamba wabunge wapo bungeni kujadili bajeti ya nchi?

Tangu bunge lianze kujadili bajeti umefuatilia na kuona mjadala wowote wa kibajeti? Kwa namna mambo yanayokwenda kwanini tusiachane na mfumo wa kupeleka bajeti bungeni...
Mawaziri wenyewe wanajadili kuongeza nguvu za kiume sasa unategemea nini?
 
Miswada yote ni yake mheshiwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania :

Rais wa JMT ni sehemu ya Bunge kwa mambo matatu tuu,
  1. 1. Kuliunda Bunge,
  2. kuridhia muswada kuwa sheria na
  3. kulivunja Bunge.

Kwa upande wa miswada ya sheria, Bunge likitunga sheria, rais anaweza kukataa kuisaini, anatakiwa kurejesha Bungeni kurekebishwa, Bunge likigoma kurekebisha, rais anakuwa hana jinsi bali ni kulivunja Bunge!.

Lakini kwa upande wa Azimio la Bunge, Bunge likiisha pitisha Azimio la Bunge, rais wa JMT hana mamlaka ya kuingilia chochote bali ni kuteleleza tuu Azimio la Bunge, vinginevyo ni alivunje Bunge!.


Kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais wa JMT halazimiki kufuata ushauri wa yoyote kwenye kufikia maamuzi, isipokuwa katika mambo mawili tuu, ambayo rais wa JMT analazimika kuamrishwa kufuata.
Source : Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?
 
Aisee hii nchi Kuna watu wanaamua kwaajili yetu bila hata kutushirikisha na mbaya zaidi ni kimyakimya.
Wanasemaje lakini kuhusu maisha ya mtanzania wa hali ya Tanzania
 
Wewe kama mwana Jf unafahamu kwamba wabunge wapo bungeni kujadili bajeti ya nchi?

Tangu bunge lianze kujadili bajeti umefuatilia na kuona mjadala wowote wa kibajeti? Kwa namna mambo yanayokwenda kwanini tusiachane na mfumo wa kupeleka bajeti bungeni?

Nasema tuachane nao kwa sababu fedha nyingi zinatumika kwenda Dodoma bungeni kupitisha kushuhudia jambo ambalo lingeweza kuwa declared once na waziri wa fedha tukaendelea na maisha.

Mfuko huu wakusoma bajeti ambayo hakuna mbunge anayechambua bajeti husika umepelekea kufa kwa lengo la bajeti kupita bungeni. Hata wabunge kwenye viti vyao hawapo wapo busy na mambo mengine.....tunapeleka bungeni kwa ajili ya nini?
🤣🤣
 
Back
Top Bottom