Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

I'll be waiting for you
Here inside my heart
I'm the one who wants to love you more
You will see I can give you
Everything you need
Let me be the one to love you more
Some way all the love that we had can be saved
Whatever it takes we'll find a way
 
This was dope!
 
Hii tabia mbaya sana kukata Maneno na kuQuote sehemu unayotaka wewe



Story yako ni ndefu sana na nisingeweza ku quote yote na isitoshe sikutaka ku quote yote ilhali sehemu niliyodhani inahusika ni ni ndogo tu, hata hivyo hii hapa nime quote.

 
Story yako ni ndefu sana na nisingeweza ku quote yote na isitoshe sikutaka ku quote yote ilhali sehemu niliyodhani inahusika ni ni ndogo tu, hata hivyo hii hapa nime quote.
Swala la Mungu kila mmoja anajua anavyomwelewa Mungu wake. Mizimu,miti,ngombe,sanamu nk. As long as kitu hicho wakiita Mungu. Kila mtu ana Mungu wake anayemuamini
 
Swala la Mungu kila mmoja anajua anavyomwelewa Mungu wake. Mizimu,miti,ngombe,sanamu nk. As long as kitu hicho wakiita Mungu. Kila mtu ana Mungu wake anayemuamini


Nakubaliana nawe 100%, lakini imani za mizimu zimekuwa ni chanzo kikubwa cha mambo mengi ya kishirikina na mara nyingi yakihusisha mambo ya kikatili dhidi ya ubinadamu, katika dini za Abrahamic Ushirikina ndio dhambi kubwa kabisa kupita zote na ipo wazi kwamba mtu akishakuwa mshirikina anaweza kufanya jambo lolote "analoamrishwa" na "mizimu", kifupi ni kwamba lengo langu ni utambue kuwa dini au imani za mizimu ni jambo la kupigwa vita kabisa katika zama hizi za kisasa zama za elimu kubwa za dini, sayansi nk.

Imani za Mizimu hazina nafasi tena na haziendani na kasi maendeleo ya kisasa.
 
But mada hii haikua special kwa ajili ya washirika wa Dini za ibrahim pekee
 
But mada hii haikua special kwa ajili ya washirika wa Dini za ibrahim pekee


Mkuu ninakuelewa, ila usichonielewa ni; Dini ya mizimu ni Uncivilised religion, ni dini kwa kiasi kikubwa inahamasisha ushirikina nk, ushirikina ni moja ya vitu vinavyochochea inhumanity katika jamii, mfano vitendo vya kuua albino na vikongwe nk, hayo ni mambo yanayoambatana na imani za kishirikina na mizimu nk, sasa katika mada yako unapojumuisha imani za mizimu hiyo ni sawa na kuunga mkono indirectly vitendo viovu vinavyoambatana na imani za mizimu/ushirikina, na ndio maana mimi nikaona hapo kidogo uliteleza.

Mfano, duniani kuna starehe nyingi sana, sasa mtu aandike mada inayohamasisha watu baada ya kuchoka na kazi wafanye starehe ili kujiliwaza na uwaambie; kila mtu anatakiwa afanye starehe anayoipenda ili kujiongezea maisha na afya tele, starehe za kufanya ni pamoja na:- kuangalia mpira, kucheza draft, kunywa soda, kusikiliza mziki, kunywa pombe, kufanya ngono na malaya nk,----

Kufanya ngono na malaya na kunywa pombe kwa baadhi ya watu hizo ni starehe lakini katika morality huwezi kuzitia katika kundi la starehe kwa maana hiyo hiyo mada ya starehe itakuwa imeunga mkono immortality indirectly japo the theme was invariable about recreations.

Point yangu ipo hapo, kwamba chochote unachokiandika pima its negative impact, hakuna mahali ambapo kuna imani za mizimu na ukose kuona imani za kishirikina na uncivilizations, underdevelopment na mambo ya kishenzi.
 
Unakataa imani za mababu zako unafuata imani wa waarabu na wazungu,sio ujinga huo[emoji706][emoji706][emoji706]
 
Unakataa imani za mababu zako unafuata imani wa waarabu na wazungu,sio ujinga huo[emoji706][emoji706][emoji706]


Suala sio imani imetoka wapi suala ni imani ipi ni sahihi na inayoingia akilini, kama Babu yako aliamini Mbwa ndiye Mungu wake na wewe utafuata imani hiyo sababu tu ni imani ya Babu yako ???------ huo si ujuha tu bali ni upumbavu pia.
 

Shukrani kwa mada, mkuu

Umeielezea vizuri sanaa, hasa kwenye mfano wa komputa na binadamu, vitu vingi vinavyotutokea sio bahati mbaya, bali ni matokeo ya matamanio, vitu tunavyowaza au kufanya mara kwa mara

Wataalamu wanasema mambo mengi mazuri au mabaya yanayotutokea, husababishwa na sisi wenyewe kwa asilimia 90. Eidha kwa kujua au kutojua kupitia kitu au vitu tunavyoamini / matamanio ya nafsi (Affirmations / subconscious mind).

Unaukumbuka huu msemo “Aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea.” Ukweli ni kwamba sub conscious mind ya binadamu haijui baya wala zuri, bali hupokea chochote unachokiamini, ndio maana kuna msemo wa “ be areful what you wish for, you just might get it”

Natamani hii mada iwafikie watu wengi ili waelewe na kutumia vizuri uwezo / nguvu walizo nazo. Watu wengi wanashindwa au wanafanikiwa kwa sababu ya mitazamo waliojijengea au kujengewa na mazingira, shule, dini na wazazi, hasa utotoni.

Ipo mifano mingi… Hinduism, Buddhism, wa-Islam, wa-Kristo na wa-pagani wanamuomba Mungu na wote wanafanikiwa! Unaweza kujiuliza Mungu yupi ni sahihi? au mbona wengine wanaomba mizimu na wanafakiwa?… Wajuzi zaidi watatusaidia hapa [emoji120]
 
Shukrani kwa mada, mkuu.
Asante sana mkuu, Shukrani it really means something to me✌️
Kweli kabisa kiongozi hili nimejaribu kuelezea kwenye mada ya Mind Illusion projection, Mind data storing na kulazimisha mapenzi.
Kweli kabisa mkuu
Natamani hii mada iwafikie watu wengi ili waelewe na kutumia vizuri uwezo / nguvu walizo nazo. Watu wengi wanashindwa au wanafanikiwa kwa sababu ya mitazamo waliojijengea au kujengewa na mazingira, shule, dini na wazazi, hasa utotoni.
Vijana wa sasa hizi habari hawazipendi wazee ndio tunazisoma mkuu.
Ipo mifano mingi… Hinduism, Buddhism, wa-Islam, wa-Kristo na wa-pagani wanamuomba Mungu na wote wanafanikiwa! Unaweza kujiuliza Mungu yupi ni sahihi? au mbona wengine wanaomba mizimu na wanafakiwa?… Wajuzi zaidi watatusaidia hapa [emoji120]
Mkuu hapa umenifirisha, je unaweza kuhisi ni kwanini inakua hivi?? Ngoja nami nigikirie..
 
Uko sawa kabisa labda sijawasilisha point yangu vizuri ninachomaanisha ni haijalishi jambo gani limetokea nitalichukulia ktk mtazamo chanya na si kujiambia nina bahati mbaya japo najua bahati mbaya ipo.

Eti a random guy! Yu
Nilikuomba unipe utajiri ili nipate kujaa furaha, nawe ukanipa ufukara nipate kuishi kwa busara.Nilikuomba unipe nguvu nipatekufanikiwa, nawe ukanipa udhaifu nipate kumnyenyekea Mungu.

Nilikuomba unipe afya nipate kutenda mambo makuu, Nawe ukanipa maradhi nipate kutenda mambo mema zaidi.
Nilikuomba unipe kila kitu nipate kufurahia maisha, nawe ukanipa uhai nipate kufaidi vitu vyote.

Umenihurumia umenijalia mema yote, Nasema Ahsante kwa wema wako Mungu, Umeninyima niliyokuomba ila umenipa yanayonifaa. Nami nasema kati ya watu wote nimebarikiwa mnoo
Eeh Mungu Ahsante 😴😴😢😢😢
 
Nalimngoja bwana kwa zaburi, akakisikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibufu toka udongo wa utelezi, akaisimamisha miguu yangu na kuimarisha hatua zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…