Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

Inashauriwa ufanye visualization na affirmations ya nini unataka na uicommand subconcious mind kupokea na kuifanya kuwa need yako. Ukiweza hili then Subconscious mind inajua lugha ya kuongea na universe (call it nature, God, Allah, Buddha, whatever kwa imani yako) then universe itakuletea solutions. Chumvi inatoa negative energies (call it mapepo) kusaidia kufocus kuziconcentrante positive energies. Kuna uzi wa Mayalla nafikiri unaongelea nguvu ya kutenda miujiza ambayo kila binadamu anayo na anaitumia bila kujua sometimes una sehemu kubwa pia ya huu mjadala.

Kwenye kitabu ya cha Napoleon Hill Think and grow rich kuna point anaongelea kitu kinaitwa autosuggestion hii inatokea ndani (kwa kufikiria mwenyewe) au nje (kwa kusikiliza suggestions za watu) yani ni limiting power ambayo inakwamisha watu wengi sana na kuua sn vipaji. Subconscious mind inapokea kila unachokiwaza, kukiona, kukitaka, na unachoambiwa au kusikia kwa watu na kukikubali etc kwa mfano unajisemea mwenyewe "siwezi" au mtu anasema huwezi na wewe unakubaliana naye.

Autosuggestion ni km unasema nataka mwaka huu nipate pesa ya kujenga nyumba na kufanya affirmation (wengine wanaita kunuia) zako then unaanza kujiwekea negativitiy mwenyewe km kusema "lkn ntapata kweli pesa"? Ukianza kujiuliza mwenyewe wakati umeweka lengo mwenyewe unaiconfuse nature inashindwa kujua ikupe nini, unachotaka au yale mashaka yako (bahati mbaya sn nature inatoa negative kiurahisi zaidi kunapokuwa na mixed feelings so unakosa unachotaka au unapata kidgo).

Wana maombi na watu wa kiroho wanaposema wakikuombea amini umepona, ni kwamba wanataka ufanye affirmation na visualization kwamba umepata tayari unachotamka then nature inachukua mkondo wake. Hamna mtu anaponya Bali nia na matakwa yako yanapokuwa strong enough. Hata Yesu alisema imani yako imekuponya au nataka takasika hamna mahali alisema amekuponya!

Ukisema napata kazi mwezi huu usirudi tena kuanza kutilia mashaka imani yako mwenyewe. Amini, komaa na chukua hatua, utaona matokeo! Kuna video nyingi sana YouTube za visualization na affirmations zina maelezo mengi mazuri na wengi wanafanikiwa sana kwa njia hii tu. Actually wakubwa kama kina Gates, Steve Jobs, Branson, na matajiri wengine huwa wanafanya visualization ya nini wanataka, wanatengeneza michoro, ideas, concepts, rRamani,picha nk then wanacommand inaingia kwenye subconscious mind halafu njia za kuumba zinaletwa na universe, zinaletwaje ni topic ingine kubwa, ndo maana unakuta mtu mwenye ndoto anaweza kuiimba na kuieleza in details hata kabla haijatokea physically bado. Ukimuuliza mtu anayevisualize kuitengeneza mashine utashangaa anavyoileza km vile tayari ailishaiunda.

Sijui km nimerukaruka bila kumaliza points au naeleweka. Humbly...

Mkuu nimekuelewa sana🫡🫡
 
It's always start on your mindset. Keep your mijd Calm
 
Kumbe 4th Annivesary ishapita. Happy anniversary my favourite topic
 
SALUTE

Maisha ni safari ndefu yenye mabonde na mashimo tu Yenye matumaini tu huku raha zikiwa chache mateso na taabu yamejaa! Kuna mambo yanaweza au yanatokea kwenye maisha yako hadi ukabaki unashanga. Yaani jambo fulani baya au zuri linakufata wewe tu kila siku hadi unajiuliza Why me?

Mfano uko mtaani kila tukio baya likitokea basi unahusishwa, unaweza kuta yaani wewe kila mwanaume anayekufata ni ni wa aina fulani usiyoipenda, labda mwizi, muhuni, mweusi, mfupi, mjinga nk.

Kwa upande wa wanaume nadhani hii inawatokea sana utasikia kabisa mtu anasema "Aisee mimi nina bahati na wanawake weupe/walimu/manesi/wanawake washamba nk nk. Yote haya ni maisha yetu ya kila siku ya sisi wanadamu, wengi hatuelewi kwanini hii inatokea hivi lakini ni vitu ambavyo vinahusiana na mambo ya kiroha na Kiasili (nature).

Lakini hadi mtu yanamtokea mambo haya bila yeye mwenyewe kujua hua nini kinafanyika? Hapa nitaenda kuelezea zaidi jinsi mambo mabaya yanavyokua yanaambatana nasi pasipo sie kupenda. Ili nieleweke vizuri nitatumia terminologies za kwenye mambo ya teknoloji.

Kwenye Computer Processors kuna kitu kinaitwa Caches, hii ni sehemu ambapo ukifinya kitu fulani kwenye computer basi kile kitu kinahifadhiwa huko ndani ili ukitaka kukitumia tena basi kinafanyiwa kazi kwa haraka zaidi. Pia kuna kitu kingine kinaitwa HTTP Cookie hizi zinafahamika pia kama Web cookie, browser cookie, internet cookie. Hizi ni data ndogondogo ambazo huchukuliwa kwenye web, internet, browser n.k na kuhifadhiwa kwenye Computer wakati mtumiaji yuko anaperuzi. Kazi yake ni kurekodi mambo yote ambayo mtumiaji (user) anayafanya kwenye internet mfano. Zinarekodi Password, page ipi umetembelea, Majina, nk. Hayo yote yanakusaidia wewe mtumiaji wa internet utakapotaka kuperuzi mitandaoni basi iwe rahisi kutumia.

Kwa upande wa Google huko wao wana project yao wanaita Hummingbird, hii ni alogarithm ambayo inafanya kazi ya kumwezesha mtumiaji wa huduma za google (Hasa YouTube na Google as Search engine) kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa haraka...wanasema Google inakujua kuliko mama yako mzazi, Ni kweli.

Unapotafuta kitu Google chochote Hummingbird inarekodi kila kitu baadae ukitaka kuitumia tena inakuletea vitu kama vile ulivyotafuta mwanzo. Ndio maana ukitafuta kitu fulani YouTube ukaangalia ukamaliza labda ukatoka huko baadae ukirudi tena youtube utakuta video mbalimbali zinazoshabihiana na zile ulizoangalia mwanzo.

Yes kwakua Google wanakua washajua ni vitu gani unapendelea ili usisumbuke kuandika wanakuletea hapo kwenye homepage as suggestion posts.

Sasa turudi kwenye mada kuu, mada yetu inahusu kwanini mambo fulani (upande wa ubaya) yanaweza kua yanakufata wewe tu!. Kwenye moja ya post zangu zilizopita nilieleza kua Roho ya binaadamu ndio inabeba taarifa ya kila kitu kukuhusu wewe, so nikachukulia kwamba Roho ya binaadamu ni kama BIOS CHIP (ROM) iliyopo kwenye Motherboard ya Computer halafu mwili wetu ni kama kasha la nje la Computer. Unapokufa Mungu anachomoa Bios chip tu iliyo na taarifa zako!

Leo twende tofati kidogo, tuchukulie Roho ni HummingBird au Cookie au Cache japo mimi nitapendelea tuichukulie kama HummingBird. Roho (Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind, Intellect na Impression. Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasa kwenye kutambua lipi baya na lipi zuri. Kwenye Mind kuna kitu kinaitwa Subconcious Mind hii ndio sehemu kuu ya Roho (Soul) ambayo kazi yake ni kurekodi shughuli zetu za kila siku ziwe za kimwili au kiroho.

Sasa kwenye maisha halisi ipo hivi, unapofanya kitu fulani roho(subconcious mind) yako inarekodi. Labda siku moja uliwahi kuwa na mahusiano/ Kutongozwa/za na mwanaume au mwanamke ambao kwako wewe ambae wewe unaona hakufai, roho yako inahifadhi taarifa kwamba uko interested na watu wa namna hiyo. Au siku moja imetokea umeiba kitu roho itahifadhi taarifa. Siku umeenda jela basi roho itasevu. siku ukitembea na mtu aliekuzidi umri roho itahifadhi nk. Kwa upande wa Psychology roho tunasema kwamba Roho (Subconcious mind) inafanya kazi kwa ukaribu zaidi au inashirikiana katika kutenda kazi na Nature.

Kwa hiyo sasa unapofanya kitu fulani roho yako ikakihifadhi, baadae Roho itawasiliana na Nature kwamba unapenda vitu fulani hivyo nature itakua inakuletea vitu hivyo mara kwa mara. Hiki kitendo nature kuwasiliana na roho kisha kukuletea yale usiyoyapenda ndio tunaita MKOSI.

Mfano: Mbaba aliyekuzidi umri kakutongoza wewe kwa kua unashida zako ukamkubalia roho inahifadhi. Baadae itawasiliana na nature kua fulani anapenda wanaume wa umri fulani kisha nature itakuletea mwingine kama suggestion. ukikubali tena na tena basi ndio itakua tabia yako kabisa. Hii ipo kwa kila kitu iwe kibaya au kizuri.

Je, tufanyaje ili kuepuka mambo mabaya yanayotuandama?

Kwenye Computer ili kuziepuka cookies baada ya kutumaliza kuperuza mitandaoni inatakiwa uende upande wa setting kisha chagua Clear Cookies ili kuondoa kumbukumbu zote zote za kuperuzi siku hiyo. Kwa upande wa Google kubaki na taarifa zako. Huwa tunashauri kutumia Search Engine ya Duck Duck Go, Hii web ni nzuri zaidi maana hua ina clear taarifa zako zote baada ya kumaliza kuitumia..ina mengi mazuri ya kiusalama hasa kwenye taarifa za utumiaji wa kila siku (Browsing History). Jamani siipigii debe hii web, ni kuwaweka sawa tu na mada yetu hii. Sasa kuclear cookies au kuondoa mikosi kwenye maisha kuna mambo kadha ambayo tutayafanya.

Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini mtu akitoka jela au mahabusu (kituoni) zile nguo alizoenda nazo huwa zinatupwa, pia itabidi aoge kabisa kabla hajaingia ndani, wengine huenda mbali zaidi kwa kuogeshwa dawa za mitishamba ili kuondoa mikosi. Hapo sasa ndio kitendo cha kuclearcookies. Wanafuta taarifa zote zilizomo kwenye roho zihusuzo jela. ni mfano tu huu ila hizi hapa chini ni njia zangu amabazo mimi kwa ufahamu wangu nadhani tukizitumia tutaweza kuondoa mshikamano wa mambo mabaya kwenye maisha yetu (Mikosi)​
  • Kujua Preferences zako
Ili kuondoa kushikamana na mambo mabaya maishani inabidi mtu ujitambue wewe binafsi unapenda nini hasa. Je unapenda Kuwa mwema? Unapenda kuiba?unapenda mwanamke wa namna fulani?unapenda mwanaume wa aina fulani nk nk.. ukishajua ukipendacho basi futa yale uyapendayo nawe yatakua yanashikamana nawe.

Hatima yako ipo mikononi mwako, usiache Nature ikuchagulie Hatima yako kwa vitu ambavyo hupendi. Hivyo basi tukisha tambua yale tunayoyapenda na kuayafuata tutaifanya nature ituletee yale pia mabayo tunayapenda.Hapo tutakua tumekwepa kufuatwa na mabaya.​
  • Kujiondoa kwenye mikosi. (Kuclear Cookies maishani)
Jamani maishani huwezi kua smart muda wote Nature always win!!!, ipo siku utanasa tu. Sasa hapa labda tuseme umeshavuruga mambo maisha yamejaa mikosi na mabaya yanakuandama. Hapa sasa tutaangalia jinsi ya kuondoa hayo mambo.

1. Tutumie Chumvi na maji, Usishangae sio uganga wala uchawi. Chumvi ni dawa nzuri sana kwa binaadamu nadhani member wengi wameielezea sana humu, sina haja ya kueleza zaidi. Cha msingi chukua chumvi ile ghafi ambayo haijapita kiwandani changanya na maji kisha nuia unavyotaka kisha oga. Hata nabii Ezra aliambiwa na Mungu achanganye maji naNchumvi kisha kuwapatia wana wa Israel wajitakase, ndio maana kwetu RC kuna maji ya baraka yenye Chumvi.

Kama utakua karibu na bahari itapendeza kabisa wewe ni kwenda na kujitupa tu majini maana huko chumvi kibao

2. Mshirikishe Mungu unayemuamini hata kama ni mzimu, hapo inabidi uombe toba kabisa, mweleze mapungufu yako na mahitaji yako kua unataka kuwa mtu mpya, mambo mabaya hutaki kushirikiana nayo. Piga sala sana na ibada kadri uwezavyo. Almighty atakuelewa na kukusafisha uwe mpya.

Maisha bana is all about determing yourself waganga, manabii na mashehe Sharifu wanatuibia tu kwa kuwa wanajua elimu tunayo kidogo, hatujitambui. Tujifunzeni kujitambua hatutasubiria kuombewa na nabii. Wao wanacheza na Psychology ambapo huko watu wengi ni watupu sa tunapigwa tuuu!!!

NOTE. Ahsante Mungu kwa yote uliyonijalia hasi umeniwezesha kuandika mada hii.
End....

Kama umepende Like, Comment then share kwa wenzio.

~Da'Vinci
el maestro.
View attachment 2217103
Huu uzi nimeusoma wote na nimeuelewa kwangu ni post nzuri ya zote kwa huu mwaka.
Umetumia lugha rahisi sana na clear kwa makundi yote ya wasomi na wasio.
Big up!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi nimeusoma wote na nimeuelewa kwangu ni post nzuri ya zote kwa huu mwaka.
Umetumia lugha rahisi sana na clear kwa makundi yote ya wasomi na wasio.
Big up!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks for compliments sir, natumaini umejifunza kitu kutoka kwenye mada hiii. If yes, then I'm honored coz that's my primary mission.
Ps. Mada hii nimeiandika kwa mfululizo/sequels/Series wa topics kadahaa. Kama utapenda unaweza kuzipitia pia. I assure you won't be dissapointed
Si nilikwambia mimi! 😀
 
Back
Top Bottom