Je, unafahamu sehemu salama za kuhifadhi wosia?

Je, unafahamu sehemu salama za kuhifadhi wosia?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Japo sheria haisemi juu ya wapi pa kuhifadhi wosia, kivitendo na ilivyozoeleka kwa walio wengi sehemu zifuatazo zinaweza kutumika katika kuhifadhi wosia:

1. Benki
2. Mahakamani
3. Kwenye ofisi ya mwanasheria
4. Kwenye ofisi ya kabidhi wasii mkuu- RITA

Inashauriwa kuhifadhi katika mojawapo ya sehemu hizi kwa kuwa ni sehemu salama na si rahisi kubadilishwa kwa njama zozote na mtu tofauti na vile vile si rahisi kupotea.

Wosia ni nini?
Ni tamko au maandishi anayotoa mtu wakati wa uhai wake akielezea mazishi yake yatakavyofanyika likionyesha mahali atakapozikwa au jinsi mali zake zitakavyogawiwa kwa warithi wake baada ya kifo chake.

Aina za Wosia:
Wosia wa maandishi
Wosia wa mdomo/matamshi


MASHARTI YA WOSIA
• Mtoa wosia lazima awe na akili timamu.
• Awe ametimiza miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
• Uonyeshe tarehe,mwezi na mwaka ulioandikwa.
• Uonyeshe majina ya warithi.
• Mtoa wosia ahusishe mali zake binafsi na si za mtu mwingine.
• Wosia ni siri wanufaika hawatakiwi kuujua.
• Ushuhudiwe na mashaidi wawili, kwa mtoa wosia anaye jua kusoma na kuandika na kwa yule asiye jua kusoma ua kuandika mashuhuda wake lazima wawe wanne na wajue kusoma na kuandika.
• Mtoa wosia lazima aweke saini yake,na kama hajui kusoma na kuandiaka aweke alama ya dole gumba la mkono wa kulia.
• Mashuhuda lazima waweke saini zao tena kwa wakati mmoja.


Pia soma: Wosia: Jambo la Muhimu Linalosahaulika/Kupuuzwa na Wengi
 
Je, mtu anaweza kuita watu wake wa karibu na kuwasomea wosia au ni Siri haitakiwi kila mtu ajue?
 
Wosia jambo muhimu sana,
Asante kwa mada,
Sasa nauliza ili uwache wosia ni lazima uwe na mali au hata kama ni kapuku pia unawacha wosia?
 
Na je hizo sehemu utapohifadhi utalipia au ni bure?
Na umesema ni siri sasa je watajuaje kama sikuwaambia?
 
Wosia jambo muhimu sana,
Asante kwa mada,
Sasa nauliza ili uwache wosia ni lazima uwe na mali au hata kama ni kapuku pia unawacha wosia?
Unwaachia wosia wagawane umaskini wako, kwa kulipa madeni unayodaiwa kama yapo,
Kama ni vijana waambulie hata nguo zako na viatu,
Urithi wa walishapata mapema ni ELIMU.
 
Back
Top Bottom