Je, unafanyaje ukiwa umepigiwa full light barabarani?

Mkuu nipo unguja nami iyo ni changamoto kubwa kwa huku
Ila na mimi hua namuwashia full halafu napunguza mwendo
 
Udereva wa kujihami ni muhimu maana unaweza kukuta unaepishana nae yuko macho ila akili imeshalala.
Kuna hizi gari za miaka ya karibuni zenyewe unaweka automatic tu kwenye taa inafanya kazi yenyewe ya kuongeza na kupunguza mwanga unapopishana na gari na hata ukiwa unafata gari kwa nyuma inapunguza mwanga
 
Hapo unaongelea range,Lc,Bmw, etc mkuu.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Binafs huwa napigiwa pass yakupunguza mwanga ilihali nimewasha mwanga mdogo hii kitu inanichanganya sana ilinibidi niende kwa fundi akanambia ukipigiwa pass ww washa taakubwa in second kisha zima ili ajue kuwa ww hapo ndo upo kwenye mwanga mdogo, sasa nashindwa kuelewa kuwa nibadili bulb ama vipi mana nafeel ninavyowakera watu, gari yenyewe ni HILUX nimeipata hivi karibuni
 
Hilux ipi mkuu kama ni hizi new model zina taa Kali Sana ndio maana narudi kwenye point wengine Wana mtatatizo ya macho we unaona unamewasha taa ndogo kumbe kwa wenzio ni Kali.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Hakika ni changamoto sana, kipindi hiki, wengi wenye magari madogo hufundishwa pasipo kwenda kwenye vyuo vya udereva, wengi wao hata aina za mwanga kwenye magari yao hawafahamu!
Aidha, baadhi wanafunga taa kana kwamba, anatembea mwenyewe barabara nzima! Hawazi kuhusu mwenzake!
Tathmini yangu inaonesha kwamba, asilimia kubwa ya madereva wa malori ni wastaarabu, hupunguza mianga pindi inapohitajika. Tatizo ni hawa wenye magari ya kati, kuanzia mafuso kushuka chini[emoji29]
 
Kama kuna madereva wa Ma bass ya Abood na Bm safari za Moro Dar.
Hawa ndio huwa wana mwanga mkali sanaa na hawaeshimu magari madogo
Mfano ist au hivi baby Walker ukipima distance ya gari ndogo na kubwa gari kubwa inakuwa ipo juu kidogo so anapopiga full mwanga wote unamwagikia kwenye uso wako Hawa jamaa wa mabasi,STL,stk,su baadhi ni wababe road.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Madereva malori ni waungwana Sana mkuu nawapongeza shida Iko kwa Hawa wa mabasi na wengineo alafu Kuna umuhim watu wapewe elimu juu ya aina na matumizi wa hizi taa.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Hizo taa za pembeni bado tutaziiba tu
 
Madereva malori ni waungwana Sana mkuu nawapongeza shida Iko kwa Hawa wa mabasi na wengineo alafu Kuna umuhim watu wapewe elimu juu ya aina na matumizi wa hizi taa.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
Ofocoz, kuna hizi gari za kati zina mianga mikali na ziko juu, hivyo ukiwa na saloon cars, ule mwanga unapiga straight kwenye kioo! Ila ni ushamba, unawezaje kumtambia mtu ambaye unapishana nae? What is akakuvaa uso kwa kukosa kuona ama kuweweseka! Unadhani utatoka salama!?
Anyways, barabarani hususan Tanzania inahitaji hekima sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…