Je, unaifahamu historia ya kuanzishwa kwa vitambulisho vya taifa (NIDA)?

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Historia ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

1986 – Wazo lilizaliwa katika kikao cha ‘Interstate Intelligence Gathering’ ambapo iliazimiwa Tanzania na Uganda kutoa vitambulisho vya taifa kama ilivyokuwa kwa Kenya na Zambia ili kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa Sheria katika nchi hizo nne. Jitihada hazikuzaa matunda, Serikali ilitunga Sheria ya Vitambulisho vya Taifa ambayo haikutumika.

2006 – Upembuzi yakinifu ulidhihirisha kuwa mradi wa NIDA unatekelezeka. 2007 – Baraza la Mawaziri liliagiza kuundwa Kamati ya Usimamizi yenye jukumu la kutoa mwongozo na mwelekeo wa programu za mradi.

kuanzishwa kwa chombo cha kusimamia Vitambulisho vya Taifa​

1755932164300.jpeg

2008 – Rais Jakaya Kikwete alisaini hati ya kuanzisha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali GN No.122 la tarehe 1 Agosti 2008
​
2011 – Usajili na Utambuzi wa Watu ulianza kwa watumishi wa umma na majaribio Kilombero, Morogoro. Juni 2012 ulianza rasmi Dar es Salaam, kisha kusambazwa nchi nzima. Kwa sasa NIDA ina ofisi 151 za usajili wilayani Tanzania Bara na Zanzibar

Kuanza kwa Shughuli ya Usajili na Utambuzi wa Watu​

1755932200718.jpeg

Una kitambulisho chako cha NIDA?

Chanzo: NIDA | MWANZO
 
NIDA ilianzishwa kwa mapenzi mema ya Taifa. Baadae wanasiasa wakauingilia kuutumia katika manufaa yao..
 
Back
Top Bottom