Je unajiandaa na interview!? Fahamu vitu vya kuzingatia

Je unajiandaa na interview!? Fahamu vitu vya kuzingatia

trojan92

Member
Joined
May 18, 2024
Posts
91
Reaction score
276
Leo tujifunze kuhusu interview au usaili
1000169012.jpg

Wengi wetu tumeshawahi kudhuria interview na tunajua kabisa mziki na mtiti wa interview sio wa kitoto hasa ukiwa huna uzoefu na namna ipi ya kukabiliana na interview.

Interview inaweza kukupanikisha kiasi cha kukosa amani kabisa na kukufanya ujihisi yale yote uliyosoma ni kama hayajakusaidia.

Twende pamoja 👇👇👇
Kuna wengine hupata homa kabisa maarufu kama interview fever na hujikuta wanaharibu na kukosa kazi ili hali sifa za kufanya kazi hiyo wanazo ila tu wanashindwa interview.

Ifahamike kuwa panelist wanao ongoza interview wanataka kukuona ukijibu kwa ufasaha na kujiamini ili kukupa nafasi ya kazi katika taasisi au kampuni yao.
Hivyo ni muhimu kujiandaa vizuri kabla ya interview ili uwe miongoni mwa wachache wataochaguliwa kuanza kazi

Mambo ya kuzingatia/kujiandaa kabla ya usaili

✅1: Itambue kampuni au taasisi unayoenda kufanya interview! Jifunze na peleleza mambo yao ya kazi yakoje, hii itakuongezea mwanga wa jinsi hali ilivyo katika taasisi husika. Aidha utajua wanalipa vipi., wanaongoza vipi na wanalipa vipi. Utajua pia sababu za wenzako kuacha au kuachishwa kazi ili usiingie kwenye mtego wa kuingia kwenye kazi isiyofaa.

✅2: Andaa vyeti vyote, copy na original ili
ikitokea wamependezwa na wewe
uwaoneshe vyeti org! Itakupa credit sababu wengi huenda na copy tu ili hali vyeti original ndio vinavyotakiwa


✅3: Fika mapema/nusu saa kabla ya interview! Kuwah ni muhimu ili uzoee mazingira! Pia itakupa confidence na kukufanya urelax, sio unafika umekimbia mijasho kama umetoka kufukuza mwizi, kuwahi hupunguza uoga na kukufanya uyajue mazingira vizuri. Pia inakupa utulivu wa akili kwani utafanya maandalizi yote muhimu na kukufanya uwe na utulivu wa akili na mwili.

✅4: Vaa kwa heshima na unadhifu kulingana na maadili ya kazi yako, fuata profession code of wearing! Usivae vinguo vya kubana,, maurembo mengi, makeup iliyopitiliza, high heels au nguo zisizofaa siku ya interview.
Weka mtindo wa nywele unofaa, nywele ziwe safi na nadhifu. Kulingana na aina ya kazi mavazi yako yasikikuke utaratibu wa kazi

✅5: Jiamini (self confidence), acha uoga na usiogope sababu interview sio kifo, sio kuwa unauliwa, panelist ni watu kama wewe, hivo jijengee confidence ya kutosha ili ufanye vema! Vuta pumzi na kuachia kidogo kidogo kutengeneza utulivu na kujiamini. Usijiamini kupita kiasi sababu utaonekana arogant! Ongea kwa kujiamini, kwa sauti ya kusikika na isiyoenesha uoga. Uwe na umakini wa hali ya juu. Ukiulizwa swali jipe sekunda hata 15 kufiriki na kujibu kwa utulivu hata kama swali ni gumu sana.

✅6: Zingatia alama, usifanye chochote bila ruhusa ya panelist. Ukingia kwenye chumba cha usaili utakuta kiti chako kimeweka ila usikae kama hujaambiwa! What if kuna boss anakuja kukaa na wewe ushakaa!? Unakuwa umefeli! Wanaweza kukukaribisha kahawa, soda nk, Shukuru! Usifakamie
subiri interview iishe ndio utumie hivyo vitu! Logic yake ni kuwa utaongeaje huku unakula!? Utaonekana hujui na hujafunzwa maadili mema. Kila kilicho kwenye chumba cha interview kina maana yake.


✅6: Jishushe na uwasikilize, licha ya kuwa unaweza kuwa umewazid elimu na mengine, ila itabidi uwasikilize panelist vyema kabisa na kuwaheshimu. Elimu yako na uwezo wako viweke pembeni ili ufaanye usaili.

✅7: Zima simu yako ili isisumbue wakati wa interview! Interview ni suala la kiofisi hivyo nidhamu ya juu inahitajika! Sio busara watu wazima wanakufanyia usaili alafu simu yako inakatisha mchakato! Kama huwezi zima basi unashauriwa kuweka katika mfumo wa do not disturb au silent Mode.

✅8: Jitahidi kujibu maswali kwa ufasaha, toa majibu yasiyoleta uwalakini! Usitoe majibu mepesi kwa maswali magumu!

Fikiri vizuri kabla kufumbua mdomo wako na kama utakuwa hujaelewa swali omba walirudie au waliweke kwa mfumo mwepesi! Tumia lugha fasaha na sanifu muda wote wa kujibu maswali.

9: Katika kujieleza kwako, jitahidi kuonesha upekee wako ( areas of exceptional) ili uuzike, sera zako na uwezo wako katika fani mbali mbali viweke hadharani, sema kitu gani kipya utakifanya ikiwa utapata nafasi ya kazi katika taasisi yao. If you want to be unique then come with new ideas

10: Tabasamu na kuwa mchangamfu: create first impressions kwa kuwa mcheshi na mchangamfu! Usinune na kuwa serious sana like the whole world is watching you, be humorous, funny and humble! Ila sasa usizidishe. Kila kitu kiwe na kiasi. Hii itakupa credit sababu hata ukiulizwa swali gumu hutaogopa na utazid kujiamini

Kesho nitakuletea maswali 15, ambayo mara nyingi huulizwa kwenye interview na namna bora ya kujibu ili ufanikiwe

Worth to share!?
Umejifunza!?
Watagi na wengine wapte elimu hii
Usisahau kunifoloow
 

Attachments

  • 1000169013.jpg
    1000169013.jpg
    44.4 KB · Views: 8
Back
Top Bottom