Mmh kweli hilo mkuu?Biblia ni kitabu cha kwanza kuandikwa kabla ya vitabu vingine vyote vya kidini duniani. Sehemu ya kwanza ya Biblia — yaani Agano la Kale — iliandikwa maelfu ya miaka kabla ya vitabu au maandiko mengine ya kidini. Hii inatufundisha kuwa Biblia ndiyo chanzo cha kwanza kabisa cha ufunuo wa Mungu kwa wanadamu.
Na hii ndiyo sababu, Biblia imekuwa msingi wa maadili na sheria nyingi duniani. Amri Kumi za Mungu, (Kutoka 20:1–17) ni "uti wa mgongo" wa sheria za mataifa mengi, zikikemea wizi, uongo, uzinzi, uuaji, na ibada ya sanamu. Hata watu wasio na dini wanakiri kwamba mafundisho ya Biblia yana busara na nguvu ya kuongoza maisha yenye haki.
Kwa hiyo, kwa kuwa Biblia ni ya kwanza, ina ukweli wa kwanza na wa mwisho. Kuiweka pembeni na kuamini vitabu vingine, ni sawa na kumweka Mungu pembeni.
Katika Yohana 12:48 tunaambiwa kwamba anayemkataa Yesu na kuyakataa maneno yake; maneno aliyoyasema Yesu yenyewe ndiyo yatamhukumu siku ya mwisho.
Moja kati ya maneno aliyosema Yesu - katika Biblia ni kwamba ,Yeye(Yesu) ndiye njia, kweli na uzima. Hakuna awezaye kwenda mbinguni kwa Baba, bila kupitia kwa Yesu.
Na tukumbuke kuwa Yesu Kristo ndiye atakayewahukumu wanadamu wote siku ya mwisho — siku ambayo imekaribia sana kwa jinsi dalili zinavyoonyesha. Shetani anaujua ukweli huu, ndiyo maana anahangaika mchana na usiku kuwashawishi watu wasisome Biblia. Anajua kwamba wakiisoma wataujua ukweli, na ukweli huo utawaweka huru na kuwaokoa kutoka dhambini na kwa njia hiyo watapata tiketi ya kuingia mbinguni. Shetani anataka watu waangamie pamoja naye motoni.
Usimpe nafasi Shetani. Kataa uongo wake na maajenti wake wanaopindua ukweli wa Biblia. Soma Biblia, na uishi kulingana na yote aliyoyaagiza Yesu. Kumbuka tena: Biblia ndiyo itakayokuhukumu siku ile ya mwisho.
Yohana 12:48
"...yule anayenikataa mimi na kuyakataa maneno yangu; yale maneno niliyoyasema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho."
Vitabu havikushushwa, my friend. Soma historia. Biblia iliandikwa na watu lakini kwa uongozi wa Mungu.Vitabu alivyoshusha
Mungu muumba wa mbingu na Ardhi na vilivyomo,Mungu Mkuu ambaye hana mfanano na chochote katu hajawahi kuleta kitabu kinaitwa Biblia/Bible.
Vitabu alivyoshusha ni Zaburi,torati,Injili org na Quran tukufu.
Hiyo biblia/bible kaja nayo Mtume yupi?
Allau wakubar .Makobazi watakuja kusema lile daftari ndio lilitangulia.
Takbiiiiir.
Teh! We jamaa unachokitafuta utakipata.Makobazi watakuja kusema lile daftari ndio lilitangulia.
Takbiiiiir.
Asante kamwamu kwa maoni yako. Ngoja nikudadavulie utaelewa tu.Umekaririshwa, au hujachimba historia ya dini. Umewahi kusoma kiitabu cha ' the book of the dead' ? Kimeandikwa miaka mingi kabla ya hiyo biblia uisemayo. Hata Musa yajulikana amri 10 alizitoa humo.
Shida yako ume-copy na ku-paste aliyokuandikia chatGPT bila kutafakari ameandika nini. Mimi mada yangu haizungumzii dini za kale. Nimezungumzia kitabu cha kwanza cha kidini chenye mafundisho mazito kwa jamii na ambacho kimetumiwa na mataifa mbalimbali kuandika sheria.Kwa kukusaidia tu, dini za kwanza na mwanzo kabla ya hiyo dini yako kuundwa kuna hizi
1.Anciet Mesopotamian religion (3500-500BCE)
2- Ancient Egyptian religion (3100-300 BCE)
Dini iliyohusu Miungu ya kimisri kama Ra (Sun God au original God ambaye wagiriki na warumi walibadiri stories za huyu Mungu mwana jua na kuunda kiumbe yesu/jesus miaka ya baadae sana)
Pia ktk dini hii kuna Miungu mingine kama Osiris na ISis.
3. Hinduism (1500BCE - till today)
4. Zoroastrianism (1200 - 600 BCE)
5. Judaism (1000- 500BCE)
6. Greek&Roman ( 800 BCE-400)
7. Buthism (500BCE)
8. Taoism (500BCE)
Na hapo sijaorodhesha dini na mafundisho mengine mengi ambayo si famous sana ulimwenguni na yalishakuwepo kabla ya kuundwa kwa biblia na ukristo kiujumla.
Dini ya ukristo imekuja juzi tu wakati huo kuna mamia ya imani na nakala zao zilishakuwepo zamani sana, huo uislamu ndio wakae kimya kabisa maana hawa kila mtu anajua wamekuja juzi juzi hapo baada ya urumi kushirikiana na muarabu kuunda hiyo dini mpya ya uislamu.
Dunia ya sasa si ile ya wajinga ambao mliwaaminisha kila takataka zenu za kidini kuwa ni sahihi, wakati huu kuna sources nyingi za kupata information za mambo ambayo yalifichwa, nawashauri wafia dini, someni sana msitegemee uongo wa vitabu vyenu ufunge fahamu zenu kuyajua mambo nje ya dini zenu.
Ukristo na hiyo biblia umecopy hadithi kutoka ktk asili ya imani za kimisri au Afrika ya kale, na kuunda huo upuuzi wa akina yesu sijui akina yehova na TAKATAKA zingine mnazoka
lilishana makanisani.
Hahahaaa, takbiiiirAllau wakubar .
Adam alikuwa Muislam pia 😂😂😂