Je, unajua matusi na udhalilishaji mtandaoni inaweza kukugharimu mamilioni?

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Mahakama Kuu ya Tabora iliamuru muathirika wa udhalilishaji mtandaoni kulipwa Tsh 3,500,000/= kama fidia kutokana na jumbe (SMS) za matusi alizotumiwa.

Unafahamu namna ya kuripoti unapokutana na udhalilishaji mtandaoni?
==
Hawa Selemani @ Ramadhani v. Zuena Ramadhan [2014] Kesi hii ilikuwa kuhusu matusi makali yaliyomdhalilisha mjibu-rufaa. Mahakama Kuu ilithibitisha kuwa madai yalithibitishwa, na hukumu ya kesi ya jinai iliyotokana na matusi hayo ilikuwa ushahidi muhimu.

Mahakama ilisisitiza kuwa matusi yanayodhalilisha heshima na utu wa mtu yanaweza kuzaa madai ya fidia. Iliunga mkono fidia ya Sh. 3,500,000, ikiona kuwa ilikuwa ya haki na inafaa kwa mazingira ya kesi.
 
Wanawake waves madela ndio zao hizo.
 
Mbona hujasema namna ya kuripoti udhalilishaji wa mitandaoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…