Je, unajua Nini kuhusu matibabu ya mpangilio wa meno?

Je, unajua Nini kuhusu matibabu ya mpangilio wa meno?

Zirconium

Senior Member
Joined
Feb 1, 2025
Posts
196
Reaction score
254
Meno yaliyopangwa vibaya siyo tiba yake kuyang'oa kienyeji.

Meno yenye mpangilio usio sahihi yanaweza kurekebishwa kwa njia ya kitaalamu iitwayo Orthodontic Treatment (Matibabu ya Mpangilio wa Meno).

Matibabu haya hufanyika kwa kuweka brackets (vichuma maalumu) kwenye meno na kuunganisha kwa wire maalumu ambayo, kwa kutumia nguvu zinazodhibitiwa kitaalamu, husaidia kuyasogeza meno taratibu hadi kufikia mpangilio sahihi.

Muda wa matibabu hutegemea aina na ukubwa wa tatizo la kila mgonjwa, hivyo unaweza kutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

Usifanye uamuzi wa kung'oa meno yaliyopinda au yaliyoota vibaya bila ushauri wa daktari wa kinywa na meno. Fika kwa mtaalamu ili ufanyiwe uchunguzi na upate ushauri wa tiba inayokufaa.

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp: 0658950085
7ece505d-765b-4d7f-ae76-e9a4137f8605-jpeg.3636138
IMG_8498.jpeg
 

Attachments

  • 7ece505d-765b-4d7f-ae76-e9a4137f8605.jpeg
    7ece505d-765b-4d7f-ae76-e9a4137f8605.jpeg
    98.6 KB · Views: 30
Mmmh! Miaka nane na yametoboka.🥶

Ndyo inawezekana kabisa meno kutoboka / kuoza kwa mtu mwenye miaka 8 ambapo sababu kubwa ni

  • Matumizi ya dawa zenye sukari hasa ( syrup )
  • Matumizi ya vyakula vyenye sukari kama pipi, biskuti , ice cream, Ufresh
  • kutosafisha kinywa angalau mara mbili kwa siku
  • Mtoto kunyonya kwa kutumia mrija ( bottle feeding )


Hizo ni baadhi ya sababu ambazo zinaweza sababisha mtoto kuoza meno / kutoboka kwa meno
 
Back
Top Bottom