Je, Unajua Umuhimu wa Recreational Pond Nyumbani Kwako?

Je, Unajua Umuhimu wa Recreational Pond Nyumbani Kwako?

BwanaSamaki012

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2023
Posts
212
Reaction score
250
Habari! Nina wasalimu kwa unyenyekevu mkubwa

Recreational pond ni aina mpya ya bwawa yanayofanana na mabwawa ya asili ambayo yanaweza kutumika kwa madhumuni mbalimbali, kama vile kuogelea, kufugia samaki wa mapambo n.k. Tofauti na mabwawa ya kawaida, aina hii ya mabwawa yanaundwa kwa maumbo na muonekano wa kipekee zaidi

Napenda kuwashirikisha jambo hili muhimu kuhusu jinsi unavyoweza kuboresha mazingira yako, kuongeza kipato chako na kujipatia kitoweo safi kwa kufanya ufugaji wa samaki kupitia mabwawa ya kisasa (recreational pond). Aina hii ya bwawa ni safi na rafiki wa mazingira.

Ni vizuri kuendeleza utamaduni wa kutumia tunachozalisha wenyewe badala ya kuwa wanunuzi, ni fahari kula unachozalisha mwenyewe. Faida za ziada za ufugaji wa samaki, unapunguza gharama ya kununua kitoweo, inakufanya uonekane tofauti katika jamii yako kwa sababu kuna watu wachache wanaofanya shughuli hii. Pia husaidia kupunguza msongo wa mawazo, kuona jinsi samaki wanavyosonga ni raha sana.

Mimi binafsi natoa huduma ya kutengeneza aina hii ya bwawa la kujiburudisha na kutoa mwongozo wa kitaalamu kuanzia siku unapoanza kuhifadhi samaki wako hadi siku ya mwisho unapovuna samaki wako.

Kwa wale wasiopenda ufugaji wa samaki, wanaweza kutumia mabwawa ya burudani kama sehemu ya bustani

Ikiwa una nia ya huduma yangu, nipo tayari kukutumikia

Bwana Samaki
Mawasiliano: +255758779170
1727450986908.png


1727450414513.png

1727450507725.png
1727450868163.png
 
Habari! Nina wasalimu kwa unyenyekevu mkubwa

Recreational pond ni aina mpya ya bwawa yanayofanana na mabwawa ya asili ambayo yanaweza kutumika kwa madhumuni mbalimbali, kama vile kuogelea, kufugia samaki wa mapambo n.k...
Kwa sisi wenye viwanja vya 20 x 14 hali ikoje?
 
Swali la haraka haraka, hawa viumbe wakiutwa m-mbu na vyura kelele zao usiku inakuaje?
 
Hachana na hizo picha za kugoogle mzee hebu weka kazi zako za kibongo bongo.
 
Swali la haraka haraka, hawa viumbe wakiutwa m-mbu na vyura kelele zao usiku inakuaje?
Mbu wanakaa kwenye maji yaliyotuama bwawa la aina hii linakuwa na earators kwa ajili ya kuongeza hewa kwenye maji hivyo muda wote waji yanakuwa yanamove, kuhusu vyura nitapandikiza kambale ambao watakula vyura na mazalia yao
 
Hayo kwenye picha ni kama ya ufugaji wa urembo kwasie tunaotaka kufuga samaki wakubwawakubwa inafaa hii???
 
Hayo kwenye picha ni kama ya ufugaji wa urembo kwasie tunaotaka kufuga samaki wakubwawakubwa inafaa hii???
Kama unataka ufugaji wa samaki wa kibiashara usiohitaji urembo ni vizuri ukajimba/ukajenga bwawa kubwa, ninaweza nikakupa muongozo
 
Back
Top Bottom