Imani rubaba
JF-Expert Member
- Dec 31, 2013
- 254
- 350
Badilika leo, ongeza mavuno kesho! Kilimo ni Biashara – Tuchukue Hatua.
Umesoma vizuri kilichoandikwa? Au umekimbilia kubisha tu 😅Kwenye makaratasi hata gunia 100 unavuna mbona!
Da... umeniwahi lakini bado umenichekesha sana. Ni kweli. Na ndilo tatizo kubwa la sisi watanzania. Unakuta watu wanalima kwa kutumia makundi ya Whatsup. Mimi nadhani njia nzuri sana ya kufundisha watu ni kuanzisha mahamba ya mfano na siyo makundi ya Whatsup.Kwenye makaratasi hata gunia 100 unavuna mbona!
Umesoma vizuri kilochoandikwa?Da... umeniwahi lakini bado umenichekesha sana. Ni kweli. Na ndilo tatizo kubwa la sisi watanzania. Unakuta watu wanalima kwa kutumia makundi ya Whatsup. Mimi nadhani njia nzuri sana ya kufundisha watu ni kuanzisha mahamba ya mfano na siyo makundi ya Whatsup.
Hebu tuone mashamba yako ya mfano.Umesoma vizuri kilochoandikwa?
Kilimo chochote kile chenye mafanikio. Kitu cha kinaanza na kujifunza kwa wataalamu, wakulima waliotangulia na wadau kabla ya kwenda field na hii ndio kazi ya group letu
Huwa mnajua aana kupanga watu kama maweView attachment 3348433
Tofauti ni mbinu tu, si muujiza!
Wakulima wengi wa mpunga hapa Tanzania huvuna gunia chache sana kwa ekari – na kwa bahati mbaya, wengi huamini kuwa hilo ni jambo la kawaida. Lakini je, unajua kuna wakulima wanaovuna hadi gunia 40 kwa ekari moja?
Ndiyo! Wakati wewe unavuna gunia 5 au 7, mkulima mwenzako anakusanya gunia 35 hadi 40 kutoka kwenye ekari hiyo hiyo.
Sasa swali ni moja: Tofauti iko wapi?
Tofauti haiko kwenye hali ya hewa, haiko kwenye udongo tu, bali iko kwenye maarifa na mbinu za kilimo. Kuna aina tatu kuu za mbinu ambazo wakulima hutumia, na kila moja huleta matokeo tofauti kabisa:
1️⃣ Kilimo cha Mazoea
Hiki ni kile kilimo cha “baba yangu naye alikuwa analima hivi.” Hakuna kupima udongo, hakuna kutumia mbegu bora wala mbolea ya uhakika. Wakulima wa aina hii huvuna gunia 5 hadi 10 tu kwa ekari — na mara nyingi huingia hasara.
2️⃣ Kilimo Bora kwa Ushauri
Hapa mkulima anatumia mbegu bora, anafuata ushauri wa wataalamu, na hutumia mbolea kulingana na ushauri wa msingi (japo si lazima awe amepima udongo). Hapa mkulima anaweza kupata gunia 15 hadi 25 kwa ekari. Si pabaya — lakini bado kuna nafasi ya kuboresha zaidi.
3️⃣ Kilimo cha Kisasa
Hii ni ngazi ya juu zaidi. Mkulima anapima udongo kabla ya kupanda, anachagua aina sahihi ya mbegu kulingana na udongo wake, anatumia mbolea na virutubisho kulingana na mahitaji halisi ya udongo, na pia hutumia mfumo wa umwagiliaji au udhibiti mzuri wa maji. Huyu anaweza kuvuna hadi gunia 30, 35 au hata 40 kwa ekari moja.
Chaguo ni lako sasa mkulima:
Je, utabaki kwenye kundi la kilimo cha mazoea kinachokuletea gunia 5, au utapanda ngazi hadi kilimo bora au cha kisasa?
Kumbuka: Mpunga hauhitaji nguvu sana, bali unahitaji maarifa sahihi.
📢 Jifunze Zaidi – Lima Kibiashara!
Usiruhusu miaka iendelee kupotea bila tija. Jiunge nasi leo kwenye jumuiya ya wakulima wa kisasa. Tunakupa maarifa, mbinu, na ushauri wa kitaalamu kila wiki.
🟢 Bonyeza hapa kujiunga WhatsApp na Jumuiya Yetu:
👉 Rubaba Media
Acha utani wewe....wataalamu ni ninyi wazee wa group la WhatsApp?Umesoma vizuri kilochoandikwa?
Kilimo chochote kile chenye mafanikio. Kitu cha kinaanza na kujifunza kwa wataalamu, wakulima waliotangulia na wadau kabla ya kwenda field na hii ndio kazi ya group letu
Ndio sisi ndil wataalamu.Acha utani wewe....wataalamu ni ninyi wazee wa group la WhatsApp?
Pia unaweza kutazama kazi zetu utufahamu zaidiHebu tuone mashamba yako ya mfano.
Ndugu viti vingine haina haja ya kua na shingo ngumu kama unahitaji mafanikio.Huwa mnajua aana kupanga watu kama mawe
Mtu akikutafuta tu unaanza na soil testing (pesa), then sampling sijui ya nini (pesa) hadi unafika kwenye kukamilisha maandalizi ya ekari moja unajikuta ulishalima ekari 10…. Na ukitafuta wataalam waliokuja sa huwaoni
Tuoneshe yako kuanzia hatua ya awali hadi unakuja kuvuna gunia 40+
Nawajua sana nyie nsio maana nikaanza na hiloNdugu viti vingine haina haja ya kua na shingo ngumu kama unahitaji mafanikio.
👉Soil testing inafanyika mara moja na itakusaidia wakati wote kufahamu udongo wako, sasa unaona gharama kumuita mtaalamu
📌Hili swali linaweza kutoka kwa watu wa aina mbilo tu ( wenye roho mbaya na wavivu)Tangazo zuri kwaajili ya kilimo cha Whatsapp, kuna mdau kasema vizuri hapo, badala ya juwaita watu Whatsapp wakaribishe shambani waone kwa mifano.
( 😅 Ni sawa unamuuliza daktari, nioneshe kama na wewe unaumwa kabla ya kunitibu)Tuoneshe yako kuanzia hatua ya awali hadi unakuja kuvuna gunia 40+
Inaonekana hata ujaelewa kabisaNawajua sana nyie nsio maana nikaanza na hilo
Baada ya kilimo cha wosapu kuanza kushtukiwa, sasa Mmekubalianaje kivingine
Tuambie twende wapi tukaone hiyo productivity…. Tutakwenda Kwa pesa zetu