Je unalifahamu kaburi la vyombo vya anga ya mbali?

Je unalifahamu kaburi la vyombo vya anga ya mbali?

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Katika Bahari ya Pasifiki Kusini kuna makaburi ya mamia ya vyombo vya angani vilivyoanguka.

Sehemu hiyo inajulikana kama "Point Nemo" kwa lugha ya Kilatini ikimaanisha "Hakuna Mtu" au "No One" yenye kina karibu kilomita 4 kwenda chini ya bahari.

'Point Nemo' ni eneo ambalo lipo mbali na ardhi au kisiwa chochote katika Dunia na kufanya kuwa mahali pazuri pa kuangusha roketi na setilaiti zilizokufa.

Mahali: 48°52.6′ latitudi ya kusini, longitudo 123°23.6′ magharibi

Umbali kufikia ardhi iliyo jirani ni takriban kilomita 2,688 (maili 1,670).

Endapo itatokea umefika 'Point Nemo', basi watu pekee watakao kuwa karibu zaidi na wewe ni Wanaanga katika Kituo cha kimataifa cha Anga (ISS) ambayo itakuwa inapita kilomita 400 juu yako kila baada ya dakika 90.

Chapisho;


FB_IMG_17306539899611710.jpg
 
Back
Top Bottom