Je, unalinda akaunti zako mtandaoni kwa usalama wa kutosha?

Je, unalinda akaunti zako mtandaoni kwa usalama wa kutosha?

Joined
Aug 23, 2025
Posts
66
Reaction score
109
Leo dunia ipo kwenye mfumo wa kidigitali kuanzia mitandao ya kijamii, benki, barua pepe, hadi mifumo ya kazi. Lakini pia uhalifu mtandaoni umeongezeka.

Njia rahisi ya kujilinda ni kwa kuwezesha Mfumo wa Uthibitisho wa Ziada (Multi-Factor Authentication MFA / Two-Step Verification).

Hii inamaanisha hata kama mtu akipata password yako, bado hatoweza kuingia kwenye akaunti zako bila uthibitisho wa pili (mfano: SMS code, fingerprint au App ya uthibitisho).

Weka MFA kwenye:

Mitandao ya kijamii (Facebook, Instagram, TikTok, LinkedIn)

Barua pepe (Gmail, Yahoo, Outlook)

Mifumo ya kifedha (Mobile Banking, Payment Apps)

Akaunti za kazi na biashara

Kumbuka usalama wako mtandaoni ni jukumu lako. Chukua hatua leo
 
Back
Top Bottom