Je, unamfahamu Aziz Ally, aliyechochea kuwepo kwa eneo la Mtoni kwa Aziz Ally?

Je, unamfahamu Aziz Ally, aliyechochea kuwepo kwa eneo la Mtoni kwa Aziz Ally?

Waterloo,
Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nimejiuliza mimi mwenyewe maswali mengi sana ambayo sikuwa na majibu na sikuweza pia kumuuliza mwingine yeyote kupata majibu kwani ithibati ya jibu la swali kama hilo lako kuwa iweje Dossa hakutambuliwa lisingeweza kutolewa na yeyote awae yule ila mwenyewe anaetoa hizo medali.

Lakini mimi nilikwenda mbali zaidi ya Dossa kwani walikuwapo wengi ambao michango yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa ya kutukuka sana.

Hawa walikuwapo TANU HQ New Street na wengine walikuwapo katika majimbo mbalimbali ya Tanganyika.

Hawa wote hawakuwapo katika orodha ya kupewa medali.

Hata hivyo nilibahatika kupitia mtu wa kati kumjua Mwenyekiti wa Kutunuku Medali na kuuliza kuhusu utoaji wa medali kwa wazalendo waliotoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Jibu nililopokea kutoka kwa mpashaji wangu kutoka kwa Mwenyekiti wa Medali lilinishangaza sana.
Mnataka kila mtu atambuliwe katika harakati za kudai uhuru si inabidi pia muweke mchango wa wakoloni kutuwekea barabara maana nyerere kukosa hizo barabara walizojenga wakoloni asingeweza kufika dar.

Ni kama kipindi hiki kila kitu tunasema chini ya uongozi wa magufuli,ndege ,barabara ni chini ya chuma anko magu kwani ina maana ni yeye peke yake ndio anafanya kila kitu? Kwani baraza la mawaziri hawafanyi chochote?
 
Waterloo,
Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nimejiuliza mimi mwenyewe maswali mengi sana ambayo sikuwa na majibu na sikuweza pia kumuuliza mwingine yeyote kupata majibu kwani ithibati ya jibu la swali kama hilo lako kuwa iweje Dossa hakutambuliwa lisingeweza kutolewa na yeyote awae yule ila mwenyewe anaetoa hizo medali.

Lakini mimi nilikwenda mbali zaidi ya Dossa kwani walikuwapo wengi ambao michango yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa ya kutukuka sana.

Hawa walikuwapo TANU HQ New Street na wengine walikuwapo katika majimbo mbalimbali ya Tanganyika.

Hawa wote hawakuwapo katika orodha ya kupewa medali.

Hata hivyo nilibahatika kupitia mtu wa kati kumjua Mwenyekiti wa Kutunuku Medali na kuuliza kuhusu utoaji wa medali kwa wazalendo waliotoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Jibu nililopokea kutoka kwa mpashaji wangu kutoka kwa Mwenyekiti wa Medali lilinishangaza sana.
Jibu nililopokea kutoka kwa mpashaji wangu kutoka kwa Mwenyekiti wa Medali lilinishangaza sana

Mohamed Said kama haoutojali tuambie ulipewa jibu gani?
 
Waterloo,
Fikra nzuri sana.
Napendekeza tupige video nadhani tutapata kipindi kizuri sana.

Nimeweka hapa baadhi ya nyumba zilizokuwa Dar es Salaam ya miaka ya 1950 na hizi ni nyumba za wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Chini ya kila paa kuna historia.

Siku tutakapojaaliwa kutembea sehemu za Dar es Salaam nitakuonyesha sehemu zilipokuwapo nyumba za wazalendo ambao unawasoma hapa Barzani.

Nyumba mbili za akina Sykes ile ya Kipata ambapo akiishi Ally Sykes na ndimo alimoficha cyclostyle aliyokuwa akichapa makaratasi ya ''uchochezi,'' haipo badala yake kuna gorofa refu hali kadhalika nyumba ya Abdul Sykes ambayo ndipo alipoishi na Mwalimu Nyerere Mtaa wa Stanley pia haipo badala yake lipo gorofa refu.

Bahati mbaya sana hivi sasa kwetu sisi kuwa nyumba hizi hazipo tena badala yake kuna magorofa marefu lakini yale ambayo yamepitika katika nyumba hizi kumbukumbu zote bado katika vichwa vya wengi.

Kuna picha ya Alexander Thobias hapo chini kachero wa Waingereza ndani ya TAA.
Huyu aliajiriwa na TAA 1950.

''On his return to headquarters Abdulwahid recommended the establishment of a permanent secretariat at TAA New Street office to deal with routine duties of the Association.

TAA employed a Makerere graduate, Alexander Tobias, as its first salaried executive staff.''

Katika picha Alexander Thobias ni huyo aliyeinama alikuwa kajiriwa na Sauti ya Dar es Salaam kama Program Officer.

TAA waligundua usaliti wake na akafukuzwa kazi katika mkutano wa TAA wa 1954 uliounda TANU.
In shaAllah ipo siku tutatembea wote mjinii.
 
Historia ya Tanganyika ni tamu sana
 
Tatizo la matajiri wengi wa kiafrika, utajiri wao unahusishwa na majini.....mwenye mali akifa tu na kila kitu kinakwenda naye.
Sio majini bali hao wanaomiliki utajiri hawawafundishi watoto wao jinsi wao wanavyofanya.
Ndo maana mwenye utajiri akiondoka utajiri unaisha.
 
Sio majini bali hao wanaomiliki utajiri hawawafundishi watoto wao jinsi wao wanavyofanya.
Ndo maana mwenye utajiri akiondoka utajiri unaisha.
Wanakuwa wanaogopa kuwafundisha watoto wao kuuana wenyewe kwa wenyewe au kushikwa uchawi na watoto wao
 
Dooohh bahati mbaya original history ya Tanganyika na Tanzania yetu haipo kabisa kwnye maktaba zetu.....sijui kwa nn
 
Sawa, huko america wako self made billionaires, lakini wapo pia matajiri ambao utajiri wao umerithishwa vizazi na vizazi.
kama akina rockfeller etc

hapa Tanzania wapo akina manji, akina Rostamu kwa mujibu wa maelezo yao.

Kizazi cha huyu jamaa ni kina nani, haiwezekani ukwasi wote huo upotelee kwenye historia.
Swali zuri sana hili mkuu
 
Rafiki zake wanasema walikuwa wakimuona Dossa ameingia kila mtu anapumua kwani watakula na kunywa kwa furaha. Dossa alikuwa mtu karimu sana. Rafiki zake wa karibu sana walimpa jina la utani, ‘’The Bank.’’
Ukarimu kama huu mimi siutaki kabisa katika maisha yangu. Yaaani wao wanafurahi kula na kunywa kwa pesa zangu alafu pesa zao wanapeleka katika shughuli za ujenzi na maendeleo
 
Mwalimu Nyerere alipokuwa anastaafu alitoa medali 3979 kwa Watanzania walioitumikia nchi hii. Jina la Dossa halikuwapo katika orodha ile…''
Ninatamani sana kama tungepata pia fursa ya kusikiliza upande wa pili wa story kutoka kwa mwalimu JK Nyerere binafsi (a well-balanced story), basi tungeweza kufahamu kwanini mzee Dossa hakuwa katika orodha ile ya wapewa medani.

Si sahihi kufanya hitimisho la maamuzi kwa kuegemea maelezo ya mtu mmoja pekee.
 
Ukwasi umekwenda na Marehemu hao.Nadhani limebakia jina tu pale kwa Azizi Ally.
Mana kwa Utajiri huo uliotajwa hapo kwa miaka hiyo Labda kwasasa familia hii ingekuwa moja ya Matajiri wakubwa Tanzania na Africa Mashariki.
Naam
 
Tajiri...
Nimeona mara kwa mara zinakuja post zinazomhusu Dossa Azizi au baba yake Aziz Ali.
Katika miaka ya 1930s babu yangu Salum Abdallah alikuwa na nyumba Mtaa wa Mbaruku, mtaa ambao Aziz Ali alikuwa anaishi.

Kwa ajili hii kwangu mimi ukoo wa Aziz Ali ukawa ni watu nawajua kwa kuwasikia kwanza kisha nikaja kufahamiana na baadhi ya wanae lakini aliyekuwa karibu sana na mimi na katika mapenzi makubwa baina yetu ni Hamza Aziz ambae alipata kuwa Inspector General of Police (IGP) katiika miaka ya 1970.

Dossa Aziz nilikuja kufahamiananae baadae sana na kitu ninachokumbuka alipojulishwa kuwa mimi ni mtoto wa Said Salum akafurahi sana na kunambia kuwa baba yangu alikuwa mtu mpole sana.

Ally Sykes ndiye aliyenipeleka kwake na ndiye aliyenitambulisha kwake.
Nakukaribisheni katika safari yangu na Ally Sykes siku aliponipeleka kwa Waziri Dossa Aziz wakati wa TANU alipokuwa mfadhili mkubwa wa chama wapenzi wake walimpa jina, ''The Bank,'':

''Ilikuwa katika miaka ya 1980 mwishoni siku mimi na Ally Sykes tulipokwenda kumtembelea Dossa Aziz. Wakati ule nilikuwa nafanya utafiti kuandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kaka yake Ally Sykes. Tulikuwa tuko mbali katika kazi ile na siku moja nikamuomba Ally Sykes anipeleke kwa Dossa Aziz nikamfanyie mahojiano.

Ilikuwa siku ya Jumapili na nilimsubiri Ally Sykes Mbuyuni katika kituo cha basi mimi nikitokea Masaki. Hapa ni barabara ya Ali Hassan Mwinyi zamani ikiitwa (Upanga Road). Huu Mbuyu ulikuwa unaitwa Mbuyu wa Kigwe lakini si wengi walikuwa wanajua jina hili. Jina hili mimi alinipa Mzee Jimpota ambae yeye na baba yangu walikuwa pamoja katika Dar es Salaam ya 1950 na akaniambia kuwa hilo jina la Kigwe ni Mzee Mwinyikhamis Kigwe wa Msasani ambao wote wakijuana toka utoto wao. Mwinyikhamisi Kigwe akitoka kwao ni Msasani kuja kusoma shule ya Kitchwele Government School pamoja na baba yangu, Ally Sykes kaka yake Abdul na vijana wengine wa Dar es Salaam.

Jimpota yeye alikuwa fundi cherehani, siku moja katika mazungumzo ndipo akaniambia kuwa ule Mbuyu waliupa jina wao wakauita, ‘’Mbuyu wa Kigwe.’’

Ally Sykes ainipitia pale na Mercedes Benz yake mpya, nyeusi inang’ara kama kioo. Alikuwa na mama mmoja Mmarekani Mweusi akanitambulisha kuwa ni mwandishi wa ‘’Washington Post,’’ Ally Sykes akipenda muziki na safari kwenda Mlandizi ilikuwa ya raha sana muziki uliokuwa ukitoka katika spika za lile dude haukuwa wa kawaida. Unasikia kila chombo. Tulipofika Mlandizi tukasimama ofisi ya CCM kuuliza nyumbani kwa Dossa Aziz. Nilipata mshtuko mkubwa pale tulipojibiwa kuwa hawamjui Dossa Aziz. Tuliondoka na tukauliza mbele watu wawili, watatu hivi mwisho bwana mmoja akatuelekeza akatuambia tuifuate njia ya majani iliyokuwa pembeni yetu itatufikisha hadi nyumbani kwa Dossa.

Tulimkuta Dossa amekaa barazani kwake ilikuwa kiasi cha saa tatu asubuhi hivi mkononi ameshika radio ya kizamani kidogo na amefungua BBC anasikiliza. Alipomwona Ally Sykes, Dossa aliweka radio yake chini akapiga ukelele, ‘’Ally ndugu yangu karibu karibu…’’ Kwa jinsi walivyosalimiana na mazungumzo yao yalivyokuwa nilijua kuwa wawili hawa hawajaonana kwa miaka mingi. Pale pale Dossa akamuita mkewe akaja pale barazani. Dossa akamwambia, ‘’Huyu ni Ally kaka yake Bwana Mzuri.’’ Nikajakujua kuwa huyu, ‘’Bwana Mzuri,’’ ni Abbas Sykes ambae yeye alikuwa kila akija Dar es Salaam kutoka Ulaya alipokuwa balozi alikuwa lazima aende Mlandizi kumjulia hali Dossa. Baadae Dossa atanieleza mapenzi yake na Abbas yalianzaje na lini.

Ally Sykes akanijulisha kwa Dossa, ‘’Huyu Mohamed, mtoto wa Said,’’ Dossa akauliza, ‘’Said yupi?’’ Jibu likatoka, ‘’Said Popo.’’ Dossa akanipokea kwa tabasamu kubwa kabisa, ‘’Namjua baba yako alikuwa mpole sana…’’ Dossa akaagiza tuchinjiwe mbuzi lakini Ally Sykes akamwambia Dossa hatukuwa na muda. Ally Sykes akamweleza sababu ya mimi kumfuata.

Dossa alizungumza kwa kama saa moja hivi akianza mapinduzi waliyofanya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kuchukua uongozi wa TAA 1950 na vipi walijuana na Nyerere alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952 na vipi walimchagua kuwa rais wa TAA 1953 chama kikafa. Dossa akanieleza kwa kirefu sababu ya TAA kufifia na nini walifanya kukirudishia chama nguvu yake.

Dossa akanieleza maisha ya utoto wake na jinsi alivozuiwa na baba yake kuanza shule hadi awe amehitimu Qur’an kwanza hivyo ikawa yeye kaanza darasa la kwanza akiwa na miaka 14 na ndiyo sababu ya kuanza darasa la kwanza na Abbas ingawa Abbas ni mdogo sana kwake.

Mbele ya nyumba yake kulikuwa na mabaki ya Land Rover. Dossa akanyoosha kidole chake cha shahada akasema, ‘’Unaona gari hiyo hapo. Nimetembea na Nyerere Tanganyika nzima na gari hii tukiwaamsha wananchi waingie TANU tumtoe Mwingereza nchini kwetu. Tulikuwa tunakwama kwenye barabara mbovu na inabidi tushuke tusukume gari na Nyerere na yeye akipiga kibega kusukuma. Usimuone mwembamba vile ana nguvu yule…’’

Hili neno ‘’kupiga kibega,’’ lilinidhihirishia kuwa kweli Dossa ni mtoto wa Gerezani kabisa kwani ni lugha ambayo mimi nimeizoea kuisikia kwa wazee wengi wakati ule. Ally Sykes alikuwa kimya, mimi niko kimya sote tunamsikiliza Dossa akizungumza kwa taratibu tena bila ghadhabu. Nimefanya mahojiano na wazalendo wengi na huwa itafika mahali katika maelezo yake utaona ameghadhibika kwa yale ambayo yeye anaona hakustahili kutendewa. Dossa hakuwa hivyo alikuwa ametulia tuli akizungumza kwa upole.

Dossa alikuwa kachoka ufukara umempiga pasi na kiasi. Sifa za utajiri wa baba yake Aziz Ali na sifa zake mwenyewe Dossa zilikuwa zinafahamika. Rafiki zake wanasema walikuwa wakimuona Dossa ameingia kila mtu anapumua kwani watakula na kunywa kwa furaha. Dossa alikuwa mtu karimu sana. Rafiki zake wa karibu sana walimpa jina la utani, ‘’The Bank.’’

Mimi nilikuwa namwangalia huku nikishusha pumzi kwa huzuni. Katika miaka ya 1920 babu yangu alikuwa na nyumba Mtaa wa Mbaruku jirani na nyumba ya Aziz Ali. Sifa zao zikijulikana na wote. Mwisho Dossa akanieleza safari yake ya Nairobi alipokwenda kufanya usaili wa kozi ya urubani na jinsi Wazungu wakakataa kumfanyia usaili juu ya kuwa walimwita wenyewe yeye na mtoto wa Ali Mmanga aliyekuwa kati ya matajiri wakubwa wa Dar es Salaam miaka ile. Jumba lake la fahari bado lipo hadi leo pale Kisutu.

Dossa akanieleza alivyomkuta Ally Sykes Nairobi mwaka wa 1947 tayari keshajiingiza katika siasa za akina Kenyatta. Dossa akanieleza kuwa baada ya kukataliwa alipiga simu Dar es Salaam kwa baba yake huku analia. Baba yake kwa huruma siku ya pili akampelekea fedha akamwambia basi anunue gari kama kifuta machozi. Dossa akanyanyua uso akaniangalia akasema, ‘’Nilikwenda Nairobi na basi nikarudi Dar es Salaam naendesha gari yangu mwenyewe tena mpya. Gari hii ndiyo ikajakuwa gari ya kwanza ya TANU…’’

Mwalimu Nyerere alipokuwa anastaafu alitoa medali 3979 kwa Watanzania walioitumikia nchi hii. Jina la Dossa halikuwapo katika orodha ile…''
Umeandika vizuri sana na katika mtiririko mzuri ila umemalizia na kachuki kidogo.
 
Back
Top Bottom