Je, unamfahamu Glenn Cunnigham? Kutoka kuwa mlemavu mpaka Mwanariadha maarufu

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,278
Reaction score
956
Glenn cunnigham alipokuwa mwanafunzi , aliteuliwa kuwa mtu ambaye atakuwa anawasha moto katika kipindi cha baridi ili watoto wenzake waweze kupata joto. Siku moja katika harakati zake za kuwasha moto , kumbe dumu la mafuta ya taa mwenzake akaweka petroli . glenn cunnigham alipoenda kuwasha moto aliungua mwili mzima na hata ndugu yake aliyekuwa naye , huyo ndugu yeye aliungua mpaka kufa .

Glenn cunnigham alikimbizwa hospitali , akiwa ameharibika sana na kuonekana kwamba hataweza kutembea maisha yake yote , na kushauriwa mguu mmoja ukatwe , wazazi wa glenn walikubali lakini yeye mwenyewe alikataa kwani aliwaambia nina ndoto ya kuwa mwanariadha mkubwa licha ya hali hii . Madaktari walimshauri awe anatembelea wheel chair na kujitahidi kutia nguvu miguu kwa kuanza kutembea kwa support kama itawezekana .

Kwa takribani miaka kadhaa glenn alianza kupata nguvu na hatimaye siku moja glenn aliweza kusimama na kupiga hatua bila support. Baada ya kuweza kusimama akajiwekea bullet journal , kila siku anakimbia kidogo kidogo na hakuacha .

Baada ya kuwa fit na muendelezo wa mazoezi ya muda mrefu, mwaka 1934 madison square garden , ndiye mwanariadha pekee aliyeweza kumaliza mbio ndefu zaidi na kuweka record , na baada ya hapo alishiriki Olympic mara nyingi zaidi na zote kushinda kwa kuvunja record .
Kwa sasa anajulikana kama the greatest American miler of all time .

Glenn cunnigham hadithi yake ni chachu kwetu tukiwa katika kipindi cha matatizo . kama una shauku , dhamira ya dhati hakuna kinachoweza kukushinda .

Daima kumbuka kuwa when you are down or feel like you are stuck in a hopeless situation , remember the story of glenn cunnigham , all you have to do , is commit to doing it.

Biblia inatuambia Wakolosai 3:23 ….. lolote mfanyalo lifanyeni kwa moyo kama kwa bwana wala si kwa wanadamu .


Lakini mtumishi wa Mungu ninaye muheshimu sana TD JAKES anasema NEVER GIVE UP HOPE , IT IS ALWAYS DARKEST BEFORE THE DAWN. Yaani kwa maana nyingine unapokaribia kukata tama ndipo upenyo ulipo.

Be inspired
kihiga@zoho.com
 
Duuh madini kama haya tuliyamiss kwa muda mrefu,huko Instagram kuta kuchwa wanajadili reality show ya wasafi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…