GE2025 Je, unapoenda kupiga kura, unazingatia mtu unayemjua binafsi au mgombea anayetoa sera bora?

GE2025 Je, unapoenda kupiga kura, unazingatia mtu unayemjua binafsi au mgombea anayetoa sera bora?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wakuu!

Tunapoelekea kwenye uchaguzi, kumekuwa na harakati nyingi za kisiasa ambapo wagombea wanachuana vikali. Mara nyingine wananchi wamekuwa wakiwapinga au kuwakataa baadhi ya wagombea walioteuliwa na vyama.

Swali linalojitokeza ni: Je, wajibu wa mwananchi ni kumchagua mtu anayemjua binafsi kwa misingi ya ukaribu na urafiki, au kumchagua yule anayetoa sera bora na zenye tija kwa maendeleo ya taifa?

1756121793619.png
 
Kwa mujibu wa ibara ya 5 ya katiba, mtu yuko huru kumchagua yeyote anayempenda, awe na sababu au hana.

Mtu huyu akipatiwa sababu kwanini amchague huyu na sii yule, hapo anakuwa ni amefanya informed decision.
P
 
Kwanza, katika siasa za kidemokrasia kuna mambo mawili makuu ambayo wananchi huangalia wanapochagua kiongozi:

1. Mtu binafsi ( kama mtu anayeonekana unaeweza kumwamini)

Hapa wananchi huangalia utu, historia ya maisha, hulka, uadilifu, hulka ya uongozi na jinsi mtu huyo alivyo karibu na wananchi.

Wapo wagombea ambao hata kama chama kimewateua, wananchi huwapokea kwa mikono miwili kwa sababu mtu mwenyewe tayari ana mvuto binafsi na anaaminika.

2. Mtu anayetoa sera bora

Sera ndizo dira ya maendeleo. Hata kama mgombea hana jina kubwa, akija na sera madhubuti zinazogusa maisha ya wananchi (uchumi, elimu, afya, ajira n.k.), huweza kuvutia kura nyingi.

Wakati mwingine mtu binafsi anaweza kupendwa lakini akakosa sera zenye mashiko, na hivyo kushindwa kushawishi wananchi waelewe mabadiliko wanayoweza kupata.
 
Back
Top Bottom