Ni sawa hiyo biologia yake ila imani inayoingizwa hapo ni ya kizamani na kwa watu wasio na uelewa mkubwa wa mambo. Ni kweli bleeding ni kitu kisichopendeza iwe ni mdomoni, puani au wapi. Hedhi ilikuwa changamoto zamani na hasa kwa wale ambao hawakuweza kujiweka katika hali ya usafi, inaleta tu kero kama vile mtu anshindwa kufuta kamasi analeta kero naye si vema akaongoza ibada. Ila kama anajisafisha hakuna shida yoyote. Jambo kubwa hapa ni usafi. Watu wote huenda chooni lakini hoja sio kwenda chooni, hoja ni kujiweka safi baada ya kwenda chooni. Mwanamke ajiweke safi wakati wa hedhi ndio jambo la msingi.