WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Mke ni bidhaa hadi atafutwe kama vile ni kuku au ng'ombe?
Nimekuwa nasikia watu hasa wanaume wakiomba watafutiwe wake na dada au mama zao.Tena wengine hudiriki hata kwenda vijijini kwa ajili ya kusaka mke.JF katika thread mbalimbali kumekuwa kunatolewa ushauri kwa akina kaka wenye kutafuta wake kuwa waende vijijini.
Swali:
Wewe kaka huoni ni hatari kutafutiwa mke tena kijijini ambako wewe labda hujakaa au umetoka siku nyingi?
Je unapoletewa ina maana moja kwa moja unaenda kufunga ndoa au ndio mambo ya kutest kwanza kama mali iko sawa kufuatana na matarajio yako?
Wanawake na wanaume wote mnakaribishwa kuchangia.
sawa kabisa mkuu Sophist...naomba maoni yako kuhusu hili la kutafutiwa mke.
- Kufunga ndo siyo sawa na kuoana.
- Kuoa hakuna cha kuonja maana ndoa, mke/mme, siyo ngono wala mapishi.
Mke ni bidhaa hadi atafutwe kama vile ni kuku au ng'ombe?
Nimekuwa nasikia watu hasa wanaume wakiomba watafutiwe wake na dada au mama zao.Tena wengine hudiriki hata kwenda vijijini kwa ajili ya kusaka mke.JF katika thread mbalimbali kumekuwa kunatolewa ushauri kwa akina kaka wenye kutafuta wake kuwa waende vijijini.
Swali:
Wewe kaka huoni ni hatari kutafutiwa mke tena kijijini ambako wewe labda hujakaa au umetoka siku nyingi?
Je unapoletewa ina maana moja kwa moja unaenda kufunga ndoa au ndio mambo ya kutest kwanza kama mali iko sawa kufuatana na matarajio yako?
Wanawake na wanaume wote mnakaribishwa kuchangia.
Huko kutafutiwa ndio sijaelewa mchakato unavyokwenda,Ina maana wanakutambulisha au ndio wanafanya negotiations zote kwa niaba yako?...VeraCity, hata mimi ningeweza rudisha nyuma miaka, ningewaomba dada zangu na kina mama ninaowajua wanisaidie kutauta mke atayenifaa... Haya mambo ya u-Girlfriend wengine wanaficha sana makucha yao bana...
Lol!VeraCity kwa nini umebadilisha jina bana? Mimi nilikuwa nashinda kupekenyua tu mabandiko yako. Sasa hili jina jipya lilinifanya unipige chenga kidogo. Lakini mzungu si athumani nimekukamata....
Mada husika....
Kuna sababu nyingi zinazoweza kumfanya mwanaume akabidhi mtu mwingine zoezi la utafuta mke:
1) Kutojua mbinu za kusogea karibu kwa wadada
2) Kutokuwa na muda wa kusogea karibu kwa wadada
3) Kuvunjika moyo na kukata tamaa na mambo ya mapenzi
4) Mila na desturi za ukoo
5) Nk nk
Mara nyingi hawa wachumba wa vijijini wana heshima na kwakweli wana malezi na hufunzwa kuheshimu mume na wazazi. Hata kama ukimkuta na tabia za kishamba inakuwa ni rahisi kumrekebisha aende vile unavopenda wewe mume. Hawa wanakuwa wanatii amri za mume,na sababu nyengine ni fitina za mjini, asilimia kubwa ya wanawake wa mjini si kutwa ukakuta wana historia ambayo mara nyingi hata ukimuomba akueleze ukweli atakuficha, matokeo unakatiza mitaa watu waakudiscuss . Huyu wa kijijini hawamjui na hakuna atakaekuja na uzushi wowote, na asilimia kubwa ya hawa kuku wa kienyeji mchinjaji unakuwa wewe mwenyewe, kwahio unakuwa umeua uzushi.
Huko kutafutiwa ndio sijaelewa mchakato unavyokwenda,Ina maana wanakutambulisha au ndio wanafanya negotiations zote kwa niaba yako?
Kuhusu kuficha makucha hata hawa wa kutafutiwa huweza kuficha.Isitoshe ukimtoa mtu kijijini akaja mjini ujue akishauzoea mji, kuna uwezekano akagundua hukuwa chaguo lake akakutoroka na kukuacha kwenye mataa.
Huenda kuna uzuri wake..... kama unatoa vigezo vyako na hatimaye kufanya uchaguzi, basi safi sana hiyo!...la hasha!
kutafutiwa ninakomaanisha mimi ni ...
-Unawaeleza (wapelelezi wako) dada/mama zako unataka mke wa aina gani; i.e -umri, -tabia, -wajihi/maumbile, -elimu, -nk...Wao wanagawana majukumu nyumba zipi wakachungue binti anayefaa au anayekaribiana na vigezo.
-Wanakuletea feedback ya uchunguzi wao, i.e mabinti waliofanikiwa kukidhi vigezo, kisha mnakaa chini kuwajadili na wewe unachagua yupi anayeonekana ana mvuto zaidi kwako.
-Unawatuma wakusanye nguvu na busara kumshawishi huyo binti awe mchumba'ko... kisha posa inapelekwa, ...kisha mahari, ..harusi, halafu unajilia 'honeymoon' ya kiukweli ukweli.... π
I too like Quemu prefer WoSπMkuu,
nimekusoma = wanaotaka kutafutiwa wanahitaji heshima, utii na kuwa wa kwanza....
Sasa ndugu yangu inategemea ni vijiji vipi maana kuna vijiji navijua mie, hakuna tofauti na mijini.
Na je, muoaji naye yuko tayari kutoa heshima, na kuwa mtiifu na mwaminifu au ni upande mmoja tu?
Mke ni bidhaa hadi atafutwe kama vile ni kuku au ng'ombe?
Nimekuwa nasikia watu hasa wanaume wakiomba watafutiwe wake na dada au mama zao.Tena wengine hudiriki hata kwenda vijijini kwa ajili ya kusaka mke.JF katika thread mbalimbali kumekuwa kunatolewa ushauri kwa akina kaka wenye kutafuta wake kuwa waende vijijini.
Swali:
Wewe kaka huoni ni hatari kutafutiwa mke tena kijijini ambako wewe labda hujakaa au umetoka siku nyingi?
Je unapoletewa ina maana moja kwa moja unaenda kufunga ndoa au ndio mambo ya kutest kwanza kama mali iko sawa kufuatana na matarajio yako?
Wanawake na wanaume wote mnakaribishwa kuchangia.
mhhh!! Interesting aspect.i too like quemu prefer wos:d
na sio jambo la kupingika kwamba "women knows better about women", m/ke anaweza kumsoma m/ke mwenzie within days tofauti na wanaume, na ndio sababu mtu huamua kumtumia dada/mama kwa uzoefu/umakini wao.
.
I too like Quemu prefer WoSπ
Kweli kuna vijiji ni afadhali ya mjini, sio kwamba wa vijijini wote wana tabia nzuri ndio nikasema asilimia kubwa = sio wote.
Na sio jambo la kupingika kwamba "women knows better about women", m/ke anaweza kumsoma m/ke mwenzie within days tofauti na wanaume, na ndio sababu mtu huamua kumtumia dada/mama kwa uzoefu/umakini wao.
Nadhani mara nyingi ikiwa mouaji kaamua kuwashirikisha wazazi kuchagua mke anakuwa tayari kutoa heshima, kwani kama angalikuwa hachukulii serious na kuchelea kuwapa aibu dada/mama asingechukua hatua hii, angalitafuta mitaani mwenyewe.
Lol!
Basi kauka ivo ivo!!!
Asante kwa mchango wako.Mimi nimejikuta nakabiliwa na wakati mgumu pia pale mtu anapokuomba kabisa kuwa naomba unitafutie mchumba maana naogopa likija kuharibika lawama nitabebeshwa.Yakinyooka basi hapo ni kicheko.Dhamana ya kumtafutia mtu mchumba ni kubwa mno na siyo kitu kidogo eti!Fikiria umemtafutia mtu halafu anakuja kulikwaa gonjwa la UKIMWI!
Mtu yoyote yule awe mwanamke au mwanaume ana paswa kutafuta mwenza wake mwenyewe. Ukitafutiwa mke na mtu mwingine huyo mtu ata kutafutia mwanamke kwa kulingana na preference zake na si zako. Bora tafuta mwenyewe anaye kupindeza ili mwisho wa siku usianze kulaumu kuwa umetafutiwa mke ambae siyo. Na siku hizi siyo kama zamani. Hakuna atakaye vumilia ndoa na mtu asiye mpenda kisa tu ime pangwa na familia.
By the way ukisha letea mwanamke na usimpendee uta tafutiwa wangapi? Si chanzo cha kuonekana mhuni tu?