Kuna myanaume hata ipatiwe mke mwema kiasi gani haioni kabisa.
Kila Mke ni mwema na ametoka kwa Mungu.
Wake wengi wamekuwa walivyo ni kutokana na walivyotendwa.
Thamani ya kitu inakuja pale unapokikosa.
MKE MWEMA NI YUPI??
Kila mmoja anahitaji lake, WANAUME wengi wanafikiri mke mwema ni yule asiyehoji chochote hata akitendewa vibaya. Asipatiwe matunzo na asiulize, mme arudi md-night mke asiuleze, mme akihitaji huduma husika apatiwe bila hata kumwandaa mkewe, mke asiyejua kipato na matumizi ya mmewe.
Je huyo ndo mke mwema unayemtaka???
Mpende mkeo, mpe uhuru wa kukujua, usimfiche mambo yako, mke ni rafiki yako, mpende. Utaona jinsi naye anavyokujali na kukuheshimu. Ukianza kumvunjia heshima, mke ni kiumbe mbaya sana. She plays back very rough.
WITO: MPENDE MKEO ATAKUWA MWEMA DAIMA, USIKOSE KUMWOMBA MUNGU PIA.
Mke mwema ni wewe utamtengeneza kwa jinsi unavyomjali na kumpenda.