Je Unatafuta Ufadhili wa NGO

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574
Wasalaam,

Kwa wale wanaotaka kuanzisha NGO ama zile zilizokwisha kuanza ipo changamoto moja kubwa ya kupata ufadhili wa miradi.

Hata hivyo kabla ya kuwaza ufadhili, Suala la mifumo linaanza kwanza. Sababu ni kuwa hamna mfadhili ambaye yupo tayari kutoa pesa yake wakati anajua hakuna usimamizi na uwajibikaji wa kikanuni na taratibu kwa fedha atakayo toa. Maana yake ni kuwa, pesa italiwa na hakuna atakaye wajibishwa maana hamna taratibu za kumwajibisha mhusika.

Hivyo basi ni muhimu kila asasi ikawa na sera, kanuni na taratibu katika maeneo yote kabla ya kuanza kutafuta wafadhili. Hii ndiyo tunaita mifumo. Ikiwa utawaza kutofanya hivi na kisha uombe ufadhili kupitia andiko lako zuri sana uliloandikiwa na mtaalam wa 'proposal writing ' shida itakayokupata ni wakati wa ukaguzi au 'organisation capacity assessment ' OCA. Hapa lazima unyooshwe kama hauna mifumo.

Baada ya mifumo, suala la kutafuta ufadhili ni muhimu sana. Zipo namna mbalimbali za kutafuta ufadhili. Wapo wafadhili wa ndani na wafadhili wa nje ya nchi.

Wafadhili wanaweza kuweka tangazo la kuita wenye maandiko (proposal) au mawazo (concept note) wayawasilishe kwao. Lakini yapo mashirika hawatangazi, wao wapo open kwa idea yoyote au kulingana na kazi zao wanaruhusu ulete wazo lako.

Wafadhili wa ndani mara nyingine hasa kwa siku hizi ambazo NGO ni nyingi ushindani ni mkubwa sana. Hapa inabidi uwe andiko zuri sana na pia LABDA kumjua 'MTU'. NGO ikiwa well established ni rahisi kupata ufadhili wa ndani. Ila kwa NGO changa hili lina ugumu kdg unless ufadhili huo unahusu asasi ndogo specifically.

Kwa ufadhili wa nje kwa maoni yangu hasa kwa NGO ndogo zilizotimiza Sharti la kwanza la mifumo ni rahisi zaidi. Shida kubwa hapa ni kupata taarifa yaani 'call for proposals' na muandishi wa hizo proposal. Si kweli kuwa kila andiko unalopeleka utapata, kumbuka pia ushindani hata huko upo pia hivyo basi utatakiwa kuandika proposal na concept note nyingi kadri iwezekanavyo.

Je unahitaji mifumo katika asasi yako inayoanza AMA asasi yako ndogo ?

Tutakutengenezea mifumo mfano, sera mbalimbali, usimamizi wa rasilimali watu, majukumu/kazi za wafanyakazi na pia tutakuandikia na kuwasilisha maandiko ya miradi na mawazo ya miradi kwa wafadhili wa ndani na nje.

Interested??

emicoltd80@gmail.com
 
Nina ndoto ya muda mrefu juu ya kufungua NGO je ni mambo gani nizingatie ili niweze kufungua NGO
 
Nina ndoto ya muda mrefu juu ya kufungua NGO je ni mambo gani nizingatie ili niweze kufungua NGO

Katika masuala ya NGO, kuwa na ndogo ni jambo la kwanza ila kuwa na sababu na nia ni muhimu kuliko ndoto.

Kwa nini ninasema hivyo? Sababu kubwa ni namna namna unavyoweza kuitegemeza asasi yako katika kipindi kigumu cha kusubiri.

Unapoanzisha asasi ndogo unapaswa kujua siku za mwanzoni itatumia gharama nyingi za msingi ambazo zitatoka kwa waanzilishi.

Sasa kwa kuwa umeuliza mambo ya kuzingatia naomba niyaweke katika makundi mawili.

Kundi la kwanza ni mahitaji ya kisheria, taratibu na miongozo.
1. Unapaswa usajili asasi yako serikalini. Hapa unaweza usajili kwa level ya wilaya, mkoa, au nchi. Zoezi la usajili ni zoezi lenye changamoto zake maana utapitia mlolongo wa ofisi za serikali za mitaa hadi wizarani. Zoezi gumu la wizarani ni katiba kuwa sawa na viwango vyao. Hapa unaweza kurudi mara kadhaa.

2. Baada ya usajili, sasa unaingia katika ulimwengu halisi wa asasi za kiraia. Hapa utatakiwa kuhakikisha kuwa mifumo yako IPO sawa. Sera na miongozo mbalimbali mfano HR manual, sera za fedha manunuzi, za mazingira, za watoto ni nyingi kulingana kazi zenu. Zote zinatakiwa ziwepo. Pia job descriptions na mafail ya staff, barua za Ajira na terms zao za ajira.

3. Baada ya hapo sasa ni utafutaji wa ufadhili. Hapa waweza tafuta ufadhili wa ndani au nje ya nchi. Hili nimelieleza vzr katika mada yangu iliyopita.Ila vitu muhimu hapa ni
a.Kupata taarifa sahihi za ufadhili.
b. Networking ukitaka uwe na mafanikio ni muhimu uwe vzr hapa.
c. Muandishi mzuri wa proposal
d. Lobbying - Technical know who & how

Nadhani maelezo haya yatakusaidia.
 
Nashukuru sana walau nimepata mwanga wapi pakuanzia
 
Nina ndoto ya muda mrefu juu ya kufungua NGO je ni mambo gani nizingatie ili niweze kufungua NGO
Plain n clear Mkuu....hakuna Cha Nini Wala Nini....hakikisha una mtu pale Foundation for Civil Society....la sivyo utaandika Sana....utaandika proposals nzuri lakini wapi??? Labda uje kupata za nje ambazo nazo zitataka kujua kazi ulizowahi kufanya na hela ulizo-manage ambazo huna.....

Kwa Leo naishia hapa
 
Ninahitaji msaada nipate mfadhili anisaidie kulipa ada ya masomo yangu chuo kikuu unaweza kunipa direction mkuu
 
Ninahitaji msaada nipate mfadhili anisaidie kulipa ada ya masomo yangu chuo kikuu unaweza kunipa direction mkuu

Kiongozi, sina deal za kulipiwa ada moja kwa moja na mfadhili ila nina connection na watu wa China, unalipa ada kiasi lakini unaweza kupata ufadhili. AMA ukawalipa wao wenyewe wakakutafutia ufadhili lakini ni China.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…