Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Habari wanaJF wakulima,

Hii ni mada mahususi itakayotoa elimu na maarifa kuhusu kilimo cha mazao ya mbogamboga na matunda kwa ujumla.

Watu wengi wanatamani sana kulima ila wanakosa maarifa mbalimbali hivyo kupelekea kushindwa na kukata tamaa.

Kupitia mada hii nawakaribisha tushauriane.

Pia soma => Kilimo cha MbogaMboga - Kanuni za Kukuza Mboga

homepage-banner-tomatoes.jpg
 
Ahsante,mie naomba unishauri juu ya kilimo cha giligilani,
juu ya magonjwa na namna ya kupata mbegu zake.
 
Naomba maelekezo ya nyumba kitalu. nilikuwa na mpango wa kujenga banda la makuti mfano wa namna bar zinavyojengwa ilihali nizuie jua na mvua. je wazolangu unalionaje?
 
Kiongozi asante sana

1 Kuhusu jua kali, na Mvua kali

a. Ni muhimu kujua majira gani unataka kuzalisha hilo zao ili uchukue tahadhari kama hizo za mvua na jua kali, na pia ni muhimu sana kujua mahitaji ya mmea wako... je unahitaji mwanga kiasi, au mvua kwa wingi na kadhalika.

b.-Kama kipato chako ni kikubwa mkuu unaweza kujenga nyumba kitalu, ambacho ni maarufu kama Green House, husaidia kiasi kikubwa katika kupunguza mionzi ya jua na mtone ya mvua. Au kwa maeneo ya jua kali sana kama dar ni vizuri ukatengeza shade house kwa ajili ya kupunguza mionzi ya jua

c. Kwa upande wa madawa ni muhimu sana unapoona muda mwingi kuna mawingu na mionzi ya jua ni hafifu, basi ni muhimu sana kutafuta dawa zenye kiambata cha KOPA (Copper) mfano Blue Copper, au Red Copper, au dawa kama Ivory, Ebony 72 WP, hizi dawa zoote zenye copper husaidia mmea kuwa wa moto, hivyo kupunguza fungus kujijenga, ni sawa na katika mwili fungus humea sehemu zinazoweza hifadhi unyevu kwa muda mrefu (mfano, mdomo, katika joint za mapaja, etc). Fungus hupenda hali ya unyevu unyevu.. kwa mfano katika zao la kahawa inashauriwa sana katika kuzuia ugonjwa unaoitwa Coffee Berry Diseases-CDB, ugonjwa wa kunyauka matunda, ni vizuri mkulima akapiga dawa za kuzuia ukungu mwezi mmoja kabla ya mvua kuanza, ili kuupa mmea moto, lakini wakulima wengi hawafanyi hivyo. Huwa wanasubiri hadi wavamiwe ndio wapige, lakini ugonjwa kama huo CBD ukivamia mkahawa hakuna jinsi utafanikiwa kuupunguza, maana lifecycle ya huyo mdudud inakuwa imefikia stage a maturity kabisa..

d. Ni muhimu pia, kama jua ni kali sana, jitahidi walau uumwagie mmea wako asubuhi na jioni, ili kupunguza water stress ambapo NI CHANZO KIMOJA WAPO huweza kusababisha ugonjwa wa Blossom end rot, kuoza kwa kitako kwa matunda mabalimbali, kama nyanya, matikiti, etc

KARIBU
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Nashukuru. Naomba maelekezo ya nyumba kitalu. nilikuwa na mpango wa kujenga banda la makuti mfano wa namna bar zinavyojengwa ilihali nizuie jua na mvua. je wazolangu unalionaje
 
Kiongozi karibu

Ntajitahidi kukueleza zile basics tu kwa sababu sijawahi kulilima

kuhusu giligilani (coriander)

AINA
ZIKO AINA 2

1FUPI-HIZI HUFAA SANA KAMA UNATAKA KUVUNA-MBEGU ZAKE, HUTOA MAUA IKIWA KIMO KIDOGO

2.NA AINA NDEFU-HIZI HUFAA KAMA UTAVUNA MAJANI

-Ni zao maarufu sana linatumika kama kiungo, kwa vyakula mbali mbali kama supu

-udongo

Jitahidi uwe tifutifu (Loam Soil)

Joto liwe la wastani 15-30 centgrade

Nafasi ya upandaji, ni sm 10 kwa 15 (shimo hadi shimo sm 10 na mstari hadi mstari sm 15), au kuweka nafasi vizuri na kupunguza uwezo wa fungus kummea, unaweza kupanda sm 15 kutoka shimo hadi shimo , na sm 20 mstari hadi mstari

Mbolea za kupandia
DAP, TSP, NPK zafaa sana

Badae utakuzia na CAN au Urea

KUOTA
-Huota baada ya siku 7-hadi 14 maximum


Mavuno ni baada ya siku 35 hadi 50

-Kama unalenga kuvuna majani, basi wahi mapema kabla maua hajaanza kutoka, maana baada ya hapo majani hayatakuwa partable (yatakuwa yamekomaa sana),
-
Kwa mbegu, subiri hadi zikomae kabisa, zile na rangi kama ya kaki hivi-kahawia, ng;oa mche na kisha hifadhi shemu ya baridi, kisha badae piga hizo mbegu, kisha fanya sorting hizo mbegu


MAGONJWA NA WADUDU
Ni muhimu kupiga dawa za kuzuia wadudu kabla ya maua kutoka (kama Match, duduall, Selecron, Evisect), na

kuikinga dhidi ya magonjwa ya ukungu au barafu kama vile POWDER MILDEW (Ubwiri poda) utailima wakati kunaunyevu mwingi dawa kama Ebony, au Blue copper , Ivory, Ridomil Gold zatosha sana kutibu na KUKINGA-ILI KUUKINGA PIGA DAWA ZENYE KIAMBATA CHA COPPER AU MANCOZEB MAPEMA KABLA UGONJWA HAUJAINGIA. Jitahid sana kama kuna mvua au ukungu mwingi epuka kumwagilia zaidi maji.

Mbegu'

Unaweza kuzipata, bila shaka Balton Tanzania, au East African seed (huenda wakawa nazo), jitahidi upate kwa wale mawakala wao kabisa, kuepuka udanganyifu

KARIBU
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Shukrani sana
kama nahitaji majani tu nadhani sina haja ya kupiga dawa ya maua,
ngoja nilime nitaleta mrejesho.
 
Mkuu naomba kufahamishwa kuhusu kilimo cha mbaazi. Gharama zake hadi mavuno, maeneo inapostawi, msimu wa kilimo, muda inaochukua toka kupanda hadi kuvuna na makadirio ya mavuno kwa eka kwa gunia.
 
Mkuu naomba elimu kuhusu kilimo cha parachichi, apple, maeneo yanayokubali kulimwa..n.k
 
Natamani kujua kiimo cha tikiti na butternut
Jr naweza Luanda vyote kwa pamoja
 
Mkuu Ahsante Kwa Elimu Yako,mimi Naomba Kujua Au Kupewa Elimu Ya Zao La Nyanya Hybrid Kwenye Open Space.
 
KIONGOZI
NTAKUELEZA ZAIDI KATIKA MATIKITI MAANA NIKO NA UZOEFU NAYO

KAMA MAZAO YOTE YANATAMBAA SI VIZURI SANA UKICHANGANYA

TIKITI,

UDONGO NA JOTO


Usiwe wa kutuamisha maji
Ukiwa Tifutifu, AU kichanga Tifutifu (Clay loam) na hali ya joto kiasi angalau 15- 35 degree inatosha sana
Linahitaji maji mengi mwanzoni lakini kadri linavyoendelea maji unapaswa kupunguza


MUDA WA KUOTA


Ukisia mbegu huchukua siku 5 hadi 10 kuota


KAMA SHAMBA LIKO TAYARI BY NOW, UKIPANDA SIKU 75 HADI 90 (AINA ZA MBEGU ZILIZOPO SOKONI KWA SASA NI HYBRID -ZEBRA, 1. SUKARI F1, 2. MSHINDI, 3. JULIANA ETC) UNAVUNA TIKITI KWA HIYO UNAMIEZI 3, OKT, NOV NA DEC WAKATI TUNAKABIA MWAKA MPYA UNAVUNA.


KWA TIKITI JITAHIDI SANA KUPANDA KWA NAFASI


KAMA UTALIMA MATUTA BASI TUTA LIWE LIMEINUKA KIASI KUJA JUU WALAU SM 20 HIVI LIWE NA UPANA WALAU WA SM 45 HADI 60, UPANDAJI, KUTOKA SHIMO HADI SHIMO SM 90 HADI 100, NA KUTOKA KATIKATI YA TUTA HADI TUTA LINGINE NI MITA 1.5=SM 150, KWA HIYO KWA MATUTA YANAYOFUATANA TIKITI ZIIKIANZA KUTAMBAAA UNAZILAZA ZINAKUTANA KATIKATI YA HIZO TUTA MBILI


KAMA UTAAMUA KUPANDA KWA MAJARUBA KAMA HAYA YA MPUNGA, AMBAPO WATU WENGI HUMWAGIA KWA KUTENGENEZA MITALO YA KIENYEJI YA UMWAGILIAJI BASI, JARUBA LAKO LINAPASWA KUWA NA UPANA WA MITA 3 NA UREFU WOWOTE ULE HATA WA MITA 5 ILI MRADI UWEZE KUMUDU KUINGIZA MAJI.


SASA KWA JARUBA TUNAPANDA PEMBENI KATIKA ANGLE HIZO. KUTOKA SHIMO HADI SHIMO NI HIZO SM 90 (=futi tatu), AMBAPO SASA YAKIAANZA KUTAMBAA UTAYALAZIA KATIKATI HAPO KATIKA HUO UPANA WA MITA 3, SO YA KULIA YATAKUJA HAPO CENTRE, YA KUSHOTO , KASK, NA KUSINI HIVYO HIVYO YANAKUJA KULALA HAPO


MBOLEA ZA KUPANDIA NI MUHIMU SANA


UKIPATA YARA MILA WINNER ( NAMBA HIZI 15:9;20 AINA YA NPK) ITAKUFAA KILA SHIMO UNALOWEKA MBEGU MOJA WEKA GRAMA 10 YA MBOLEA SWA NA KIJIKO KIMOJA KIKUBWA CHA WALI. ZITAOTA BADA YA SIKU 5 HADI 10


AFTER ONE MONTH, UTAWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KAMA CAN AU UREA


MAUA YAKIJA JITAHIDI UPATE BOOSTER (HIZO NI MAALUMU KWA AJIRI YA MAUA NA MATUNDA


ZIPO BOOSTER ZINAITWA STAARTER- MFANO HALISI ZILIZOPO MADUKANI NI POLYFEED STARTER-HIZO HUTUMIKA KUPIGA MAUA WAKATI WA MAUA


MATUNDA YAKIJA UTAWEKA POLYFEED FINISHER-HIYO NI KUIMARAISHA MATUNDA, NA PIA UTAFUTE MBOLEA INAITWA YARA NITRABOR (HII INA Calcium na Nitrojen kwa wingi) , husaidia kuzuia tikiti kunyauka, na kuzoa katika kitako-Ugonjwa unaitwa Blosom End Rot

WAKATI WOOTE WA MAISHA YA TIKITI USISAHAU DAWA ZA WADUDU, WANAOKATA MAUA , NA KUTOBOA MATUNDA, DAWA KAMA DUDU ALL AU SELECRON, AU MATCH, AU KARATE MOJA WAPO YATOSHA KUMALIZA WADUDU


LAKINI WAKATI WA KUPIGA HIZI DAWA KUWA MAKINI SANA USIPIGE MCHANA, UTAUWA NYUKI WA KUFANYA UCHAVUSHAJI KUTOFANYIKA-HAPO UTAPATA DIFORMALITIES NYINGI SANA KAMA SHAPELESS KATIKA MATUNDA, PIGA ASUBUHI SANA AU JIONI SANAA,




PIA KAMA UTAONA KUNA HALI YA UKUNGU (UNYEVU NI MWINGI AU BARIDI USIKU AU MCHANA) NI MUHIMU KUWEKA DAWA ZA JAMII YA COPPER, KAMA BLUEE COPPER, AU EBONY KUZUIA UKUNGU,


NI MUHIMU SANA KUHAKIKISHA TIKITIKI ZAKO ZINAPATA MAJI WALAU MARA 3 KWA WIKI, ILI KUPUNGUZA WATER SRESS


GHARAMA ZA MBEGU

KWA EKARI MOJA UTAHITAJI Gram 300 za mbegu , ambapo jumla ya gharama za mbegu ni kati ya tsh 200,000 hadi tsh 300,000

MAVUNO

Kwa kuwa kwa nafasi tajwa hapo juu utakuwa na mashimo yasiyopungua katiya 2000 hadi 3000 Kwa ekari moja. Hivyo kila shimo au kila kamba ya tikiti ikikupa matikiti matatu means utakuwa na mavuno ya vichwa vya tikititi kati ya 6000 hadi 9000, ambayo ni sawa na wastani wa tani 12 hadi 18 kwa ekari moja

Karibu Kiongozi
ASANTE Sana Mkuu,Ntadesa kama ulivyoelekeza
Je Mbegu ipi/matikiti yapi yana uzika kwa bei ya juu, eg Dar shilingi ngapi kwa tikikiti
 
kilimomaarifa.tajiri kaka tunashukuru sana kwa elimu unayoitoa. Nina swali katika kilimo cha tikiti. Maelezo uliyoyatoa hapo juu ni kuhusu tikiti maji ila je unaweza kutumia hatua hizohizo katika matikiti ya aina nyingine kama honeydew na cantaloupe??
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ahsante Mimi Nalima Kipato F1 Tayari Nimeotesha Mbegu Bado Kupandikiza Shambani Nitapanda Wiki Ijayo,sasa Mbolea Ninazotaka Kutumia Ambazo Nimeandaa Ni Dap SA na CAN sasa nimepanga kuweka mbolea ya DAP siku tatu kabla ya kuweka mche nimwage maji kila siku na siku ya nne niweke miche je itakuwa sawa? na je baada ya hapo nipulize dawa gani? na je hiyo abamectine peke yake inatosha kukinga funza? naomba ushauri wako.
 
Mkuu Ahsante,mimi Niko Mtwara Na Maji Yana Chumvi Kidogo,lakini Labda Ungenipa Ushauri Wa Dawa Nzuri Maana Hapa Nina Dudu All,konto Na Ninja,pia Naomba Kujua Endapo Nitaweka Mbolea Ya Dap Wakati Wa Kupanda Nikae Siku Ngapi Niweke Mbolea Ya Kukuzia?(SA)
 
Ok,sijaelewa Unaponiambia Nisitumie CAN kama nitaweka SA kwasababu mimi niliplan nianze na DAP,then SA na mwisho nimalizie CAN matunda yakianza labda nipate ushauri wako,kwa upande wa wadudu huku kuna panzi wanakata sana nyanya kuanzia kitalu mpaka ukishapanda
 
Back
Top Bottom