Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

JEMEDARI .H.

Salaaamu kiongozi

Samahani kwa kuwa kimya ni majukumu tu


Mkuu Habari,naomba Kujua Eti Ni Kweli Kwamba Nyanya Inavyoanza Kuzaa Matunda Katika Matunda Ya Mwanzo Unatakiwa Utoe Tunda Moja La Kwanza Kabisa-MKUU HII SI KAWAIDA KUFANYIKA KATIKA NYANYA, BALI HUFANYIKA SANA KAKA PILIPILI HOHO (CAPSICUM- SWEET PEPPER)? Sababu Nimeambiwa Hilo Tunda Linakula Sana Mbolea Na Maji Mengi-KWA PILIPILI HOHO, HILO TUNDA LA KWANZA-King fruit KUONDELEWA ILI KURUHUSU MMEA KUTOA MAUA NA MATUNDA MENGI YENYE AFYA NJEMA (UBORA) NI KAMA PRUNNING VILE-Upogoleaji, HII HUFANYIKA ILI KUUPA MMEA STRESS ILI UZAE ZAIDI. Hivyo Ukilitoa Hilo Matunda Mengine Yanakuwa Makubwa Na Shape Nzuri,naomba Kujuzwa Hilo.
 
Mkuu ningependa kujua ni mbolea gani zina calcium kwa wingi ambazo hupatikana zaidi kwa urahisi? mana ile uliyotaja maeneo mengine haipatkani...
 
Tatemahunda

Kama umekosa Yara Nitrabor tafuta CAN, naamini hii utaipata, ila siku ya kuweka CAN , hakikisha shamba limelowana maji (Mwagia kwanza maji) then ndio uweke CAN-Usiweke mbolea shamba likiwa KAME, LAKINI usije kuichanga CAN na mbolea nyingine siku hiyo unapoweka, CAN iwekwe ikiwa pekeyake.

Ahsante sana mkuu, nimeelimika sana, najua tupo wengi tuliopata elim hii, hata hivyo niko kwenye maandalizi nianze kuingia shamba kati ya December na January ili nisikutane na nyanya ya iringa mana naskia wale huanza kuvuna mwishoni mwa April(although I'm not sure), pia naskia nyanya yao ikianza zao la nyanya hua linashuka thamani sana..naamin ajaliapo Muumba nitaleta mrejesho humu ili wengi zaidi wafaidike...
 
Tatemahunda

Nakushukuru sana kiongozi

Kuhusu nyanya ya Iringa hiyo miezi sina hakika sana ila nachojua ni kuwa kuanzia mwezi wa nne na kuendelea mpaka wa 8 hapo bei ya nyanya na mazo mengi ya matunda bei zinashuka kidogo maana wengi wanatumia maji ya mito na madimbwi kuzalisha, na mazao yakuwa mengi hivyo bei huwa chini (demand and supply). Sababu hasa ni kwamba kuanzia mwezi wa 4 sehemu nyingi za nchi masika inakuwa inaelekea ukingoni hivyo wengi wanalima sana mbonga mbonga na matunda, wengi wanaogopa kulima mboga mboga namtunda wakati wa masika (December-March) maana changamoto ni nyingi sana, hasa magonjwa ya ukungu/barafu, wadudu na mafuriko pia.
LAKINI HAYA MAZAO YA HORTICULTURE UKIWEZA KULIZALISHA KIPINDI CHA MASIKA (DEC-MARCH) BEI YAKE HUWA NZURI SANA, MAANA SUPPLY INAKUWA KIDOGO, WAKATI DEMAND IKO CONSTANT/JUU ZAIDI.

Nakushauri ingia shambani December mkuu, ila jipange sana uwe na dawa za Ukungu na za wadudu za kutosha, tengenza mifereji ya kuzuia na kupitisha maji ya mvua, pia hakikisha maji hayatuami shambani.

Nakutakia mafanikio mkuu.






Ahsante sana mkuu..
 
Ahsante sana mkuu, nimeelimika sana, najua tupo wengi tuliopata elim hii, hata hivyo niko kwenye maandalizi nianze kuingia shamba kati ya December na January ili nisikutane na nyanya ya iringa mana naskia wale huanza kuvuna mwishoni mwa April(although I'm not sure), pia naskia nyanya yao ikianza zao la nyanya hua linashuka thamani sana..naamin ajaliapo Muumba nitaleta mrejesho humu ili wengi zaidi wafaidike...

Naomba msaada ,tayari nimewatika miche ya nyanya gram 30 aina ya eden f1 imeanza kuota,naomba kuuliza je natakiwa kuanza kupiga dawa ya ukungu kabla sijapandikiza shambani? ipi ni dawa bora ya ukungu na wadudu kwa nyanya za masika? Ipi ni booster bora kwa zao la nyanya msimu huu,je wakati wa kupiga booster naweza changanya na dawa ya ukungu au ya kuzuia wadudu? Je nitatumia mifuko mingapi ya mbolea kuanzia kupanda na kukuzia. Asante na kazi njema.
 
Asante sana kwa msaada wako na pia naomba usinichoke kwa maswali yangu mengi,hii inatokana na ugeni kwenye kilimo hiki cha nyanya.naomba kujua hiyo booster natakiwa kupiga mara ngapi mpaka naanza mavuno ?na nikianza kuvuna nitaendelea kupiga booster,hiyo booster inaweza kugharimu tsh ngapi? Tafadhali naomba usinichoke,asante.
 
Ahsante kwa majibu mazuri kutoka kwa kilimo maarifa ila kwa matokeo mazuri zaidi usichanganye dawa za wadudu na mbolea, kila la kheri
 
Nimelima viazi mviringo je naweza kutumia mult k au poly feed kama booster na ikafaa? Mbolea nilipandia dap ,je ni mbolea gani nzuri kwa kukuzia kwa pato zuri la viazi. Asante
 
Ngoja nipitishe macho naweza ondoka na la maana
 
Naomba msaada tena, miche ya nyanya ina wiki mbili sasa tangu niwatike na imeshaota,je naweza kupiga dawa kwa ajili ya kuzuia mdudu kanitangaze ? Kwa vipimo vipi na mara ngapi kabla sijapandikiza shambani, na pia naweza piga au kuchanganya na dawa ya kuzuia ukungu kwa siku hiyohiyo. Asante sana.
 
Samahamani naomba kuuliza tena, mbolea aina ya yara miller winner na npk zina ubora/utendaji sawa? Asante.
 
Mkuu, naomba msaada wa kitaaluma, nataka nikalime nikakodi shamba nifanye kilimo cha umwagiliaji nipande vitunguu maji, ni nini cha kuzingatia
 
Back
Top Bottom