Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

naomba kuuliza juu ya kilimo cha kabeji, msimu upi ni mzuri kwa kilimo hiki? je ni mbegu gani nzuri,gharama na faida kwa ekari moja. Asante
 
naomba kuuliza je,kuzidisha ridomil gold na mbolea za majani kama mult k wakati wa upigaji kwenye nyanya kuna madhara?Yaani baada ya kupiga kila baada ya siku 14 ukapiga kila baada ya siku saba. Asante.
 
Tuko pamoja mkuu, japo dah hizo namba naomba utusaidie mibadala ya mitandao mingine ili iwe rahisi nasi kukupigia.
 
NATAKA KUJARIBU KULIMA TIKITI NJOMBE /UWEMBA AINA YA SUKARI FI ILA SIJAWAHI ONA MTU KALIMA, JE KINACHOFANYA TIKITI LIWEZE KUZAA VIZURI NI MAZINGIRA AU HUDUMA?. NILIKUWA NAONGEA NA MKULIMA WA NYANYA KUHUSU MMEA WA NYANYA UNAWEZA KUZAA NYANYA NGAPI,AKANIAMBIA MNYANYA MMOJA ULIOHUDUMIWA VIZURI UNAWEZA KUZAA NYANYA 30 HADI 70 JE NI KWELI? HAPO ZINAWEZA KUFIKA KILO NGAPI KWA NYANYA 70? ASANTE.
 
hiyo no yako mbona kama sio voda mkuu? 0744? ila inapatikana though..thanks
 
Samahan Ndg. naomba kuuliza juu ya matumizi ya mbolea itokanayo na kinyesi cha popo
 
kilimomaarifa.tajiri
Kaka mimi nakushukuru sana kwa elimu yako, nimefaidika sana uendelee na moyo huo huo.Mungu akuzidishie baraka.
PDF yako ya kitunguu imekuwa msaada mkubwa kwangu, nakushukuru sana , ntaboresha kilimo changu cha vitunguu
Ukimaliza na ya Nyanya nistue mkuu.

Shukrani.
 
Mkuu Naomba Kufahamu Kuna Utofauti Wa Ubora Baina Ya Mbegu Hybrid Za Nyanya? Kama Upo Ni Mbegu Gani Bora Kuliko Zote? Na Je Ni Kweli Mbegu Hizi Zinastahimili Magonjwa Kama Vile Ukungu,magonjwa Ya Udongo Ya Virus Na Bakteria Ikiwa Ni Pamoja Na Mnyauko? Na Je Nikikamua Mbegu Ya Hybrid Nikapanda Itakuwa Bora Kama Ya Awali?
 
Mkuu Kilimomaarifa.tajiri salaam sana ama baada ya salam mimi ni mzima wa afya.

Natafuta dawa ya kuulia magugu shambani (herbicides) ambayo itakuwa na uwezo wa kuua magugu kwa muda wa mwaka moja au angalau magugu yasiote kwa muda wa miezi 6.

Je, ni dawa gani nzuri?

Nipo Dar es Salaam.
 
ukiwa unamsubiria akujibu hebu jaribu kucheki page za mwisho za hii thread alishaelezea hii mambo, akija ataongezea
 

Mkuu Kilimomaarifa, asante sana kwa majibu yako yaliyoenda shule kali na ya uhakika. Mungu akuongezee zaidi maarifa.

Basically, mimi shamba langu lina miche ya miembe yenye umri kama wa mwaka na nusu hivi, na on average miche ina urefu wa kama 70cm.

Sasa mkuu Kazi ya kupalilia magugu mara kwa mara imenichosha, ndiyo maana nilikuwa natafuta hiyo Herbicide. Ila kwa sababu umenipa darasa zuri sana kwa Herbicides zinazofanya kazi muda mrefu kuwa kimazingira hazifai kabisa , basi nitatafuta hizo herbicides za muda mfupi.

BTW, nimepitia hiyo page 18.

Je, unaweza kunipatia mifano michache ya herbicides nzuri ili nitafute?
 
Angalia usije una hiyo miembe. Be extra careful on this regard.
 
Angalia usije ua hiyo miembe. Be extra careful on this regard.
 
miembe ya kisasa nini?
maana nishazoea kule kwetu, miembe wala hatuna habari nayo ila ukifika msimu wake inazaa hadi inakwanyuka matawi kwa kuelemewa na matunda mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…