Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Sasa kazi iko hapa.. Siku ya 41.. Mweee vitumba vya maua vimekuja.. miche bado midogo chini... Kazi ipo... Dah
 

Attachments

  • IMG-20160218-WA0002.jpg
    90.5 KB · Views: 174
  • IMG-20160218-WA0011.jpg
    139.6 KB · Views: 168
  • IMG-20160218-WA0009.jpg
    89 KB · Views: 195
SAFI KIONGOZI, KAZI NZURI

USHAURI WANGU KWAKO

1. USIACHE KUPIGA WAUXAL MACRO MIX-BOOSTER NYAKATI HIZI WIKI YA 6-8 TANGU KUSIA MBEGU , ILI TUPATE MAUA MENGI,MAUA MENGI, NDIO MATUNDA MENGI, MATUNDA MENGI NDIO PESA NYINGI

2. JITAHIDI SANA SASA NI MUDA WA KUFANYA STAKING, KUFUNGA KAMBA WAKATI HUU NI MUHIMU SANA, TAFUTA MITI NA ZILE MANILA KAMBA, UKICHELEWA UKASUBIRI MATUNDA BASI WAKATI WA KUFUNGA UTAKUWA UKIGUSA NYANYA (MATUNDA) NA KUZIANGUSHA

3. MAJI YAENDELEE KUWEKWA KWA WINGI ILI KUPUNGUZA TATIZO LA UPUNGUFU WA MAJI (WATER STRESS) SHIDA IHIYO NAYOWEZA KULETA FRUIT/FLOWER ABORTION)

KILA LAKHERI

SHIDA YOYOTE TUENDELEE KUWASILIANA KIONGOZI



Sasa kazi iko hapa.. Siku ya 41.. Mweee vitumba vya maua vimekuja.. miche bado midogo chini... Kazi ipo... Dah
 
UKUMBUSHO;
KWA WALE WOTE ambao mmelima mazao ya mboga mboga na matunda kipindi hiki cha mvua (Nyanya, Kabeji, Hoho, Matango, Kitunguu, Viazi Mviringo etc) na upo maeneo ambayo mvua zinanyesha kwa wingi, Ni muhimu Sana kupiga dawa za Kujikinga na Ukungu/Fangasi, kila baada ya siku 7. Ni vyema pia kuchanganya dawa hizo za ukungu na kinatishi Sumu/Steaker Spreader/Aquar Sticker, ili kusaidia kunatisha dawa katika mmea, na kuifanya iweze kunyonywa kwa urahisi ndani ya mmea. Itakuwa bora zaidi kama utakuwa unaalternate dawa za Kujikinga (Zenye Mancozeb, au Copper, Cholothanil et al..) na za Kutibu Ukungu ( Zenye Metalaxyn, Azoxtroboni, Pottasium et al..) kila baada ya wiki moja moja.
 
mkuu unaweza ukatupa pia clue kuhusu kilimo na masoko ya kitunguu saumu??
 
[/QUOTE]
mkuu vp kuhusu kitunguu saumu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…