Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Emoj


POLE KWA HIZO CHANGAMOTO.

UMESEMA UMEPANDA BILA MBOLEA, NA KAMA MPAKA SASA HUJAWEKA MBOLEA JITAHIDI SANA UWEKE MBOLEA KWA SASA TAFUTA YARA MILLER WINNER, AU NPK JAPO YENYE NAMBA 17:17;17, BADAE MATUNDA YAKIJA UTAWEKA CAN KWENYE MIZIZI,

KIONGOZI AGRIFOS 400SL NI DAWA NZURI YA KUTIBU FANGASI (SOIL FUNGAL)WA UDONGO AMBAO HUSABABISHA KUNYAUKA KWA MIMEA KUTOKA JUU-MAJANI KUJA CHINI-SHINA, WENGINE TATIZO HILI HULIITA "KINYAUSHI", HUTOKEA SANA KATIKA MAZAO KAMA , HOHO ,NYANYA, VITUNGUU, VIAZI, MVIRINGO, NA KWA SASA SHIDA HII YA KINYAUSHI IMEANZA KUKUMBA SANA WATU WANAOLIMA MAZAO YAFUATAYO, PARACHICHI, APPLE, NYANYA, VIAZI MVIRINGO NA KITUNGUU KWA MIKOA YA IRINGA, MBEYA, NJOMBE, KATAVI NA RUVUMA ETC.

KI UKWELI AGRIFOS 400 HAINA UWEZO MKUBWA WA KUUUA WADUDU WARUKAO WANAOTAMBAA JUU YA ADRHI, KAMA WALE WANAOTOABOA MAJANI, AU WANAOKULA MICHE MICHANGA (WANAOKATA MASHINA-CUTWORM-NG'ONYO) AU WANAOSUCK MATUNDA (KUNYONYA MATUNDA),

YENYEWE AGRIFOS 400SL NI NZURI SANA KUTIBU FANGASI WA UDONGO WANAOSABABISHA KUOZA KWA MIZIZI YA MMEA NA KUSABABISHA KUKAUKA, PIA NI NZURI SANA KUUA WADUU WALIPO NDANI YA UDONGO SI NZURI KUUA WADUDU WARUKAO ANGANI

ZIFUATAZO NI DETAILS ZA AGRIFOS 400 SL

Trade Name; Agrifos 400SL
Common Name:A mixture of monopotassium and dipotassium phosphonates455g/L (equivalent to phosphonic acid 400g/L)
Reg No: FU/0114
Registrant: Fluence Middle East Limited
Usage: Against late blight on tomatoes and fungal diseases on horticultural crops.

AGRIFOS, AU FUNGURANI NA ZINGINE KAMA HIZO HUWA ZINATUMIKA MAPEMA KUTIBU UDONGO WA SHAMBA AU KITALU KABLA HUJAPANDA MICHE, AU PIA HUTUMIKA KUKINGA MCHE DHIDI YA MNYAUKO (WILTING/BLIGHT).

CHA KUFANYA

1. KWA SHIDA YA WADUDU WANAOKATA MAJANI/SHINA, TAFUTA DAWA MOJA WAPO YA HIZI; 1. MATCH 500EC YENYE-Lufenuron 500g/L INATENGENEZWA NA SYNGENTA ITAKUSAIDIA SANA, AU TAFUTA 2. KARATE YA SYGENTA PIA, AU 3. DUDUALL, AU 4. SUBERCLONE, AU 5. BLAST 60EC


2. KWA SHIDA YA KUNYAUKA KWA MIMEA, KAMA DAWA HIYO ULIYONAYO NI AGRIFOS HARIS (ORGINAL) NA KWELI IMEFELI, BASI TAFUTA DAWA INAITWA
FUNGURAN, AU Apron Star 42WS AMBAYO NI YA SYNGENTA, IKO NA VIAMBATA HIVI Thiamethoxam 20g/Kg + Metalaxyl ?M 20g/Kg +Difenoconazole 2g/Kg HII ITAKUSAIDIA SANA KUUA WADUDU WA KWENYE UDONGO WALE WAHARIBIFU WA MIZIZI, LAKINI PIA IKO NA METALAXYN AMBACHO NI KIAMBATA KIKUU KATIKA KUTIBU KINYAUSHI KINACHOSABISHWA NA FANGASI

3. MICHE KUKAUKA MARA NYINGI PIA HUCHANGIWA KWA KIASI KIKUBWA NA UKAME HIVYO JITAHIDI SANA KUWEKA MAJI YA KUTOSHA ENEO HILO, KAMA NI PAKAME (HAKUNA MVUA)

KWA UPANDE WA BOOSTER ILI KUSAIDIA MICHE IKUE HARAKA

HAPO TAFUTA BOOSTER MOJA WAPO KATI YA HIZI 1. POLYFEEED STARTER, AU WUXAL MACRO MIX, SUPER GROW AU VIJIMAX

asante sana mtaalam
 
Asante sana sana na ubarikiwe na kuzidishiwa zaidi kwani ni ngumu kwa watu kujitoa namna hii kwa kupoteza muda wa kusaidia wengine pasipo malipo. Asante sana.
 
kilimomaarifa.tajiri kwanza nikushukuru kwa kuendelea kutuelimisha, nimelima butternut kidogo na zucchini lakini sina a,b,c zake. Naomba kujua kama natakiwa kupiga dawa zinapotoa maua, na ni mbolea gani napaswa kuweka? Mpaka sasa kwa sababu bado mimea ni midogo na niliotesha direct siyo kitaluni nimeweka DAP. Pia kuna jani linanisumbua sana sana (siyo shambani) naomba kujua dawa ya kutumia ili iweze kuua mpaka mizizi yake. Asante
 
Last edited by a moderator:
ASante sana kilimomaarifa.tajiri nitazingatia. Hapo kwenye dawa yenye hicho kiambata unaweza kunitajia yoyote? Niliwahi kupiga round up!(sijui nimepatia sp!) jani likakauka lkn baada ya muda likachipua upya! Asante
 
Last edited by a moderator:
NINA IMANI

check huo mfuko wa NPK, UTAKUTA UNAMAKUNDI MATATU YA NAMBA MFANO: 17:17:17, (IKIMAANISHA NITROGEN-N-17, PHOSPHORUS-P-17,POTASSIUM-K-17) INAYOFAA KUKUZIA NYANYA NI ILE AMBAYO NAMBA YA KWANZA NI KUBWA KULIKO ZILE MBILI ZILIZOBAKI MFANO UKUTE NI NPK YENYE HIZI NAMBA 20:10:10, UKIKOSA HIYO BASI CHUKUA HATA NPK YA 17:17:17:

KILA LAKHERI


Naomba kuuliza npk yenye namba gani inafaa kukuzia nyanya
 
I can declare, this is one or few of the best thread i ever come across since i join Jamiiforum, 1000000 likes kudos!, thumb up...
 
Naomba kuuliza je mbegu ya nyanya aina eden f1 na assila f1 ni ipi inazaa sana. Asante.
 
kilimomaarifa.tajiri nini sababu ya nyanya kusinyaa majani pia majani yanakuwa njano na vidoti vyeusi! Baadhi ya matunda ya nyanya nayo yanaoza kny kitako nifanyeje?
 
Last edited by a moderator:
kilimomaarifa.tajiri nini sababu ya nyanya kusinyaa majani pia majani yanakuwa njano na vidoti vyeusi! Baadhi ya matunda ya nyanya nayo yanaoza kny kitako nifanyeje?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Invisible heshima mbele, nakusihi uuweke huu uzi sticky ili tunapotaka kuurejea iwe rahisi tafadhali. Asante
 
Last edited by a moderator:
Naomba kuuliza je miche ya nyanya ikichelewa kuhamishiwa shambani,ikipandikizwa wiki ya tano badala ya wiki ya tatu kuna madhara kiuzaaji?
 
Asante kwa majibu mazuri,nilisafiri niliacha miche ikiwa na wiki 3 kitaluni nategemea kurudi ikiwa na wiki 5 au 6. Wasiwasi wangu ni kwamba je itazaa vizuri kama mmea mmoja unatoa kilo 3 nami nimechelewesha kupandikiza ,na ukatoa machipukizi mapya licha ya gharama za kuhudumia na kuchelewa uzaaji , je utatoa kilo zile zile au mapato yatakuwa sawa na ambavyo ningepanda kwa wakati? Asante.
 
NEW NEW NEW NEW NEW
AMANI YA BWANA IWE NANYI



Tarehe; 18/10/2015 Saa 12.00 JIONI

Leo tutajifunza Faida na Agronomy ya matunda yaitwayo Parachichi (Avocado)

SOMO LA TATU; ZAO LA PARACHICHI (AVOCADO)

avocado-sliced-in-half.jpg

Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili

1. Faida za Parachichi upande wa Lishe

-Tunda lina vitamini zifuatazo

1. Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri

2. Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve

3. Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa

4. Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili

5. Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi

6. Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu

Madini- (Mineral Elements)

Ni tunda lenye

1. Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi

2. Madini ya Calcium-Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili

3. Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili


2. Agronomy ya Parachichi

Hali ya hewa

-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

Joto

Nyuzi 15-25 Sentigrade

Muinuko

Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

Aina za Parachichi

1. Zipo aina za kiasili
Kila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi

images



-Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi

ii. Aina ya pili ni Fuerte
-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu


images




-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana

UPandaji wa Parachichi

Nafasi kati ya shimo na shimo

-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

-Hivyo nafasi yaweza kuwa

8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

Ukubwa wa shimo
-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

Mbolea

-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

Kipimo cha mbolea,

-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO

-Parachichi hasa hizi za kisasa, huanza kuzaa baada ya miaka 3 na matunda yake hukomaa baada ya miezi 6 hadi 12. Tunda la aina ya HASS ndilo huchelewa zaidi kukomaa huchukua kati ya mizei 7 hadi 12 tangu lilipo jitengeneza katika mti.

MAVUNO
-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '

FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)

Magonjwa ya parachichi

Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda

1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni

5824734299_4940d330eb_o.jpg
2372468252_ea77e64362_z.jpg
Jani lililoshambuliwa na Alga

14991342145_8fb7f1fe14_z.jpg
5684201507_a9cb170821_z.jpg

Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri

2.Magonjwa ya matunda
Yasababishwayo na fangasi/Ukungu, Wadudu,na Lishe dunipia
15085900645_f4932bf337_z.jpg
-Tatizo la Athracnose husababishwa na Ukungu/Fangasi

Scab.jpg
-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi

1390031-SMPT.jpg
1390032-SMPT.jpg

Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips


DAWA

-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

-Lishe ya mmea

Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.

BEI

KUANZIA MWEZI WA 8 PARACHICI HUWA ADIMU SANA, NA KWA MAENEO YENYE MUINUKO WA MITA 1700, NDIO MUDA WA PARACHICHI AINA YA HAAS HUKOMAA, AMBAPO


KILO MOJA YA HAAS HUWA MATUNDA 3 HADI MATUNDA 5. DEBE MOJA LA KILO 20 HUWA NA MATUNDA 40 HADI 70 KUTEGEMEA NA UKUBWA.

KUANZIA HUO MWEZI WA SABA NA KUENDELEA DEBE MOJA LA PARACHICHI AINA YA HAAS HUANZIA TSH 15000 NA KUENDELEA

JUST IMAGINE

UNA EKA MOJA (1 ) TU YA PARACHICHI YA MITI 100 TU (MITI MICHACHE KABISA), NA KILA MTI UKUPE JAPO KILO HIZO 40 (DEBE 2), NA KILA DEBE 1 UUZE KWA TSH 15000 TU


MAHESABU

MICHE 100 X DEBE 2@ MCHE X 15,000TSH@DEBE 1= 3,000,000 TSH-MAPATO HASA HUPATIKANA BAADA YA MIAKA 3 NA KILA MWAKA MAVUNO HUONGEZEKA PARACHICHI ZENYE UMRI WA MIAKA 5, HUFIKIA KUTOA MAVUNO HADI YA DEBE 8 (KILO 160) KWA MMCHE MMOJA. JE KWA MICHE 100??

MAHESABU

MICHE 100 X DEBE 8 KWA KILA MMCHE MMOJA X TSH 15,000 KWA KILA DEBE 1=TSH 12,000,000

UMRI WA MAVUNO BORA KWA MMEA WA PARACHICHI NI MIAKA 40 HADI 50

Hitimisho

Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini


Masomo mengi zaidi kuhusu kilimo yatakuwa yanakujia kupitia hapa Jf na blog yetu ya
KILIMO MAARIFA punde itakapo kamilika kuandaliwa



attachment.php


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx




AMANI YA BWANA IWE NANYI

9/10/2015; 10.45 jioni

kilimomaarifa.tajirinawakaribisheni katika ukurasa huu KADRI NITAKAVYOKUWA NIKIPATA WASAA (MUDA) ntakuwa nikitoa mada mbalimbali katika ukurasa huu ZIHUSUZO KILIMO CHA MBOGA MBOGA NA MATUNDA na kujibu maswali mbalimbali yahusuyo kilimo cha mboga mboga na matunda; (Ukipata wasaa waweza jifunza mengi zaidi kupitia blog hii KILIMO MAARIFA

SOMO LA PILI ;
KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KILIMO HAPA NCHINI.

Karibuni sanaa

Kwa leo ntajikita kueleza kwa kifupi sana na kwa lugha rahisi , KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KILIMO HAPA NCHINI.

1.UKOSEFU WA MAARIFA SAHIHI

-Ni vizuri ikafahamika kuwa kilimo ni utaalamu kabisa (Sayansi) kama ilivyo udaktari au uhandisi au fani yoyote ile inayohitaji maarifa.Ndio maana mimea usipojua mahitaji yake kwa wakati sahihi, baadhi itakufa, au itakuletea mavuno hafifu, n,k

Hivyo kabla ya kwenda shambani na kuwekeza muda wako na pesa zako, ni muhimu sana KWANZA ukajifunza kupata maarifa sahihi ya kitu gani unataka kuzalisha, mbegu gani utatumia, madawa (WADUDU &UKUNGU), mbolea, wadudu gani waharibfu utakabiliana nao vipi, utahifadhi vipi mazao yako baada ya kuvuna na mambo mengine mengi.

BILA KUFANYA HIVYO UTAPATA HASARA TU, kwa sababu sasa hivi kilimo ni soko huria, hivyo utakutana na pembejeo feki nyingi sana za kilimo humo madukani, wauzaji na wasambazaji BAADHI SI WAAMINIFU (ANZIA MBEGU, MADAWA, MBOLEA).

Utapanda mbegu feki hazitaota, utatumia madawa feki yata kuunguzia mimea yako, na wakati mwingine utauziwa madawa hata iaina 5 yanayofanya kazi mmoja ya kuua wadudu (hivyo kupoteza fedha zako). Ukisosa maarifa sahihi utakuwa mtu wa kutanga tanga tu, kwa mfano wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia wewe unaweka mbolea ya kupandia, wakati yan kuweka dawa za kukinga mimea yako na ukungu wewe unaweka dawa za kuua wadudu, aina fulani ya dawa hazifai kuua magugu ukiwa umeshapanda mimea wewe utatumia tu kiua gugu chochote herbicides bila kujua ipi inafaa wakati gani, hivyo utapoteza pesa zako nyingi kwa kutanga tanga na kutokujua ufanye nini kwa wakati sahihi

-Jambo lingine sambamba na maarifa, ni kuwa UNAPASWA KUANZIA SOKONI KWANZA KABLA YA KUZALISHA ZAO LOLOTE LILE, LENGO NI UJUE

i). NI ZAO GANI LINAKUWA ADIMU/LINAPENDWA SOKONI (WALAJI) WAKATI GANI LINAKUWEPO SOKONI KWA WINGI AU LINAKUWA NA MAHITAJI MAKUBWA-

Lengo la kutambua hili ni Ili sasa ukajipange kuzalisha kuendana na mahitaji ya soko, ili huo wakati uatao vuna na kupeleka sokoni ukutane na bei nzuri kwa maana ya demand and supply-kama mzigo upo kidogo sokoni na mahitaji ni makubwa automatically bei itakuwa juu na hivyo kuwa faida kwako wewe mzalishaji.

Mfano kwa uzoefu wangu- nafahamu mazao mengi sana huwa adimu sokoni kuanzia miezi ya disemba hadi April maana mvua huwa nyingi nyakati hizo hivyo wengi huogopa kuzalisha wakati huo kuhofia mafuriko, wadudu na magonjwa ya ukungu ni mengi sana, na hapo ndio bei za vyakula huwa juu, hivyo ukiweza kutime nyakati hizo lazima utapata faida

ii). NI MUHIMU PIA KUTAFITI, ni aina ipi ya hilo zao linapendwa sana na walaji, mfano je walaji wanapenda nyanya size nene sana, au saizi ya kati au ndogondogo, au mfano katika matikiti je wanapenda ya rangi zenye michirizi maarufu kama zebra, au ya kawada, je katika Karoti wanapenda karoti fupi nene, au nyembamba ndefu, au mfano katika kabichi walaji/soko wanapenda za iana gani zenye ngozi ngumu na umbo kubwa (kilo 4-7 etc) au saizi ndogo? etc.


2. UKOSEFU WA MAANDALIZI SAHIHI (MTAJI)

Wakulima wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawakujipanga, kuanisha mahitaji mahususi yanayotakiwa katika kilimo husika, hawakujipanga vizuri kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mfano- (Mkulima hakupiga mahesabu sahihi ya mahitaji ya shamba lake tangu kuandaa shamba, kupanda, mbegu madawa, mbolea, palizi, mavuno, hadi kufikisha sokoni) anapoanza kilimo akikutana na changamoto mfano za mbolea za kupandia, kukuzia, au za maua na matunda (booster), pesa inakata naye anakata tamaa anaamua kuzalisha tu ili mradi au kutelekeza mashamba, hivyo ni muhimu sana , kujipanga kabla ya kuanza shughuli yoyote, ambayo utajitoa muda wako na pesa yako.

Wasalaamu. mawasiliano. kilimomaarifa.tajiri@gmail.com
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

SOMO LA KWANZA; KILIMO CHA NYANYA

TAREHE; 20/09/2015 SAA 12. 49 JIONI



KARIBU


NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA KUNA MDUDU ANAITWA Tuta Absoluta.. au waswahili wanaimuita KANITANGAZE (MAANA AKIKUVAMIA SHAMBANI HAKUNA NAMNA UTAACHA KWENDA KUMSIMULIA) Anakausha matunda, na kuyaozesha pamoja na kusababisha matunda kudhoofika.CHANGAMOTO KUBWA WASIYOIJUA WAKULIMA NI KUWA DAWA ZA KUZUIA MDUDU HUYU INABIDI ZIPIGWE KUANZIA MCHE UNAPOKUWA KATIKA KITALU..

WENGI WA WAKULIMA HUKIMBIZANA KUTIBU MDUDU HUYU WANAPOONA MATUNDA YAMEVAMIA (YAMEOZA, AU YAKO NA MAKOVU KATIKA KISHIKIO Calyxn)
LAKINI DAWA DHIDI YA MDUDU HUYO ZIPO KWA SASA


DAWA ZA KUTUMIA
1. Colagen,na Belt (Hizi lazima uzitumie alternatively, wiki hii unapiga Belt wiki ijayo unapiga Colagen) Ukitumia moja tu hautafanikiwa, maana Colagen inweza kuua zaidi mayai na yule funza, na Belt inamafanikio zaidi katika kuua yle moth kipepeo mwenyewe. Dawa hizo ni za kampuni ya Buyer (Waingereza/Wajerumani)


2. Nimbecidin-Ni dawa ipo kwa sasa inafanya vizuri, asili yake ni mafuta ya Mwarobain (Neem)
3. Evisect-Inasambazwa na Arysta Life Science inafanya vizuri
4. Abamectini au Dyinamec pia inafaaa sana


AGRONOMY YA NYANYA


AINA
Ziko nyingi kama fupi kiasi (Semi Determinent), kama-AINA HIZI HUWEZA KUVUNA KWA MIEZI 2 HADI 4 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA

A; Semi-determinent


1. Eden (Hii inafaa sana wakati wa mvua nyingi-Ni imara dhidi ya ukungu,/Baridi)
2. Ipo Shanty
3. Assila-Hii ni imara sana wakati wa Ukame
4. Kipato-


B; Aina Ndefu (Indeterminent)-AINA HIZI NDEFU HUWEZA KUVUNWA MFULULIZO KWA MIEZI 8 HADI 12 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA)-HUWEZA KUREFUKA HADI MITA 5 KWENDA JUU


AINA HIZO NI 1. ANNA F1 2. COLAZON 3.DIVINE 4. GALILEYA 5. EVA


C; AINA ZA OPV-OPEN POLLINATED VARIETIES
1. RIo Grande
2. Onyx
3. Tengeru 97
4.Mkulima


MAZINGIRA
i. Joto la kadri 20-35 degree sentigrade

ii. UDONGO
-usituamishe maji, Kichanga tifutifu utafaa zaidi, Wakati wa kupanda ukipandia samadi au mboji itafaa zaidi ili kuimarisha udongo


iii. NAFASI YA KUPANDA


-Ni vizuri ukatengeneza matuta ya upana japo wa sm 60, na ukapnada double line (Mistari miwili katika tuta moja) nafasi ndani ya mstari ni sm 60 kwa 60 na umbali kati ya mstari na mstari ni sm 45, LAKINI kama utapamda mistari miwili ndani ya tuta moja (raised bed) hakikisha mche wa kwanza katika mstari wa pili unakuwa upo katikati ya miche miwili ya mstari wa kwaza ili KUPATA ZIG ZAGA SHAPE


-Umbali wa tuta hadi tuta,
Umbali wa kutoka katikati ya tuta moja hadi jingine liwe ni 1.5 MITA


Njia hii ya matuta ni nzuri sana kama utaweka drip line (Drip Irrigation)


Kama hauna drip, basi tengenza matuta lakini pande pembeni mwa tuta (chini kidogo mwa tuta) maana kwa njia hiyo utamwagia kwa njia ya Furrow (Mifereji)


KIASI CHA MBEGU
kwa ekari moja utahitaji Mbegu gram 100-150 kwa OPV variety, na Gram 30-50 kwa hybrid (F1) . Ghrama za kutosha eka moja kwa OPV variety ni tsh 100,000-180,000, na kwa Hybrid (F1) Gharama ni kati ya tsh 200,000-400,000 kutegemea na aina yenyewe ya mbegu.


UPANDAJI


Sia mbegu katika kitalu, tengeneza tuta la upana wa mita moja hadi mbili, na urefu wowte utakao, na kisha chora vimefereji vidogo vidodgo kwa kijiti, vilivyoachana baina yake kwa sm 5, kisha dodondosha mbegu taratibu, na kisha fukia na layer ndogo ya mchanga, kisha weka nyasi kavu na mwagia maji, hakikisha unamwagia mwaji uliyochanganya na DAP MBOLEA, Gram 100 sawa na UKUBWA WA KIGANJA CHAKO KIMOJA, WEKA KATIKA MAJI LITA 15/20 KISHA MWAGIA KWA KILA TUTA.


Maji yamwagiwe angalau kwa siku mara mbili (SAA 2 ASUBUHI NA SA 11 JIONI)


MBEGU ZITAOTA BAADA YA SIKU 7 HADI 10 tangu kusia mbegu.


ZIACHE MBEGU KATIKA KITALU KWA MUDA WA WIKI 3 TU KISHA HAMISHIA SHAMBANI.


MAMBO YA KUFANYA SHAMBANI


Kabla ya kupandikiza hakikisha kitalu kimemwagiwa maji ya kutosha-ili iwe rahisi kung'oa miche, na sahamba mama pia liwe limemwagiwa vya kutosha


-hakikisha umechimba mashino mashimo yako kwa nafasi, na kisha kila shimo lipate angalau gram 10 hadi 20 za mbolea moja wapo ya hizi (Yara Miller winner, TSP, DAP, AU Minjingu au NPK)


Kisha weka mmea wako na fukia vizuri udongo, siku hiyo paada ya kupandikiza hakikisha kila mmea unapata angalau ml 250 za maji


BAADA YA KUPANDIKIZA


Chunguza sana juu ya wadudu, wakatao shina (Cutworm), pamoja na wale wanaoharibu majani


Dawa kama Karate, Duduall, Match, Selecron, moja wapo itakufaaa kukabiliana na wadudu hao


Baada ya siku 15 tangu kupandikiza weka mbolea ya kukuzia moja wapo ya hizi, CAN, UREA, Yarra miller winner, au Hata NPK,


Baada ya siku 25 tangu kupandikiza miche itaanza kutoa vitumba vya maua, Hapo unahitaji booster za majani na maua (KUZUIA MAUA YASIDODNDOKE) kama vile, Polyfeed starter, au Multi K (19:19;19), au Yara Miller Tracel Biz AU Wauxal Macro Mix


WAKATI HUU WA MAUA NI MUHIMU


Kuzingatia dawa za kuua wadudu, zipingwe asubuhi sana au jioni sana, ukizipiga mchana sa 6 hadi sa 9, utaua nyuki (watakimbia) na matunda yatajitengeneza bila fertilization, yatakuwa seedless au shape less


MATUNDA YAKIJA

Ni muhimu kuzungusha chini katika mizii mbolea ya Yara Nitrabo, au yoyote yenye Calcium, ili kuzuia kuoza kwa kitako cha matunda (Blosom End rot), au matunda kupasuka-Cracking

WADUDU

Wadudu wasumbufu wa nyanya, ni funza wa matunda, wanaokata miche michanga, wadudu wanaoscratch majani. Leaf miner (Wachora ramani katika majani)


Magonjwa


Kinyaushi cha kwanza, (Early Bright), Kinyaushi cha mwisho (ate Bright), magonjwa ya bakteria na ukungu(Unga mweupe katika matunda), Baka jani (Leaf spot)


MUDA WA KUKOMAA
NYANYA HUCHUKUA KATI YA SIKU 120 HADI 150 TANGU ZILIPOSIWA KATIKA KITALU HADI KUKOMAAA


MAVUNO


Ekari moja inaweza kutoa cret 1300 za kilo 50, sawa na tani 65


SOKO


Nyanya yenye bei nzuri ni ile ya inayoingia sokoni kuanzia disemba hadi March-Nyakati hizo bei kwa cret moja hufika hadi tsh 80,000


Gharama za kuhudumu shamba la Nyanya kwa eka 1 ni takribani 2.5 hadi 3.5 Milioni ( Gharama kubwa ipo, katika mbegu hasa kama ni hybrid (F1), mbolea, maji (Pump), Vibarua (wakati wa kupanda na kupalilia) na madawa ya kuzuia wadudu na kutibu magonjwa.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dah! Somo zuri sana.Tupia somo la TIKITI Mkuu.
 
kilimomaarifa.tajiri barikiwa mpaka ushangae, leo nimehamisha miche ya nyanya kutoka kitaluni, nasubiri siku ya kumi na tano niweke mbolea ya kukuzia kulingana na maelekezo yako. Hivi buster pia inaweza kuwekwa mapema na baadae ikawekwa tena?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom