Je, unatumia gas kwa kupikia?

Je, unatumia gas kwa kupikia?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
moto-wa-gasi-jpg.296235


Je unatumia gas kwa kupikia?Tafadhali soma ujumbe huu na uchukue tahadhari ili isitokee kwako. Hili linaweza kuwa ni kosa la kawaida katika kila nyumba.JINSI ILIVYOTOKEA.jiko la gas lilikuwa linamewaka na mapishi yakiendelea.

Mama akaona mende jirani na sink la kuoshea vyombo. Mara akachukua kopo la dawa ya mbu na kupuliza karibu na lile jiko la gas linalowaka.Ulitoka mlipuko mkubwa na ndani ya muda mfupi yule mama alikuwa ameungua kwa asilimia 65.

Mumewe alikimbilia kuuzima ule moto na nguo zake nazo zilishika moto.Mumewe bado yuko hospitali akiuguza majeraha ya moto na bado hana habari kwamba mke wake alifariki alipofikishwa tu hospitali.

Ni vema tukafahamu kuwa dawa zote za kuulia wadudu "Hit", "Marten", "heaven", "Raid" n.k. zina mchanganyiko wa madawa mengi yanayosababisha mlipuko mkubwa.Mchanganyiko huu wa madawa ni rahisi sana kusababisha mlipuko haraka sana.

Tafadhali elimisha wanafamilia yako na rafiki zako kuhusu jambo hili na sambaza ujumbe huu.Tafadhali usiuhifadhi ndani ya simu yako, shirikisha wengine, huwezi jua utaokoa maisha ya watu wangapi. Mimi nimefanya kama nilivyopokea.


jiko-la-gas-jpg.296234
 

Attachments

  • jiko la gas.jpg
    jiko la gas.jpg
    98.3 KB · Views: 1,471
  • moto wa gasi.jpg
    moto wa gasi.jpg
    38.7 KB · Views: 1,416
kwa kuongezea, makopo ya dawa, perfumes yaliyozibwa hayapaswi kuchomwa moto, cause yanavilipuko ni hatari sana pia
 
Je unatumia gas kwa kupikia?Tafadhali soma ujumbe huu na uchukue tahadhari ili isitokee kwako. Hili linaweza kuwa ni kosa la kawaida katika kila nyumba.JINSI ILIVYOTOKEA.jiko la gas lilikuwa linamewaka na mapishi yakiendelea.

Mama akaona mende jirani na sink la kuoshea vyombo. Mara akachukua kopo la dawa ya mbu na kupuliza karibu na lile jiko la gas linalowaka.
Ulitoka mlipuko mkubwa na ndani ya muda mfupi yule mama alikuwa ameungua kwa asilimia 65.

Mumewe alikimbilia kuuzima ule moto na nguo zake nazo zilishika moto.
Mumewe bado yuko hospitali akiuguza majeraha ya moto na bado hana habari kwamba mke wake alifariki alipofikishwa tu hospitali.

Ni vema tukafahamu kuwa dawa zote za kuulia wadudu "Hit", "Marten", "heaven", "Raid" n.k. zina mchanganyiko wa madawa mengi yanayosababisha mlipuko mkubwa.
Mchanganyiko huu wa madawa ni rahisi sana kusababisha mlipuko haraka sana.

Tafadhali elimisha wanafamilia yako na rafiki zako kuhusu jambo hili na sambaza ujumbe huu.
Tafadhali usiuhifadhi ndani ya simu yako, shirikisha wengine, huwezi jua utaokoa maisha ya watu wangapi. Mimi nimefanya kama nilivyopokea.

Ahsante.
Ila ifahamike kwamba hapa jiko la gesi sio chanzo cha huu moto. Chanzo ni kupulizia dawa ya mbu kwenye live flame na ndio ajali hiyo ikatokea. Hizi sprays zote zimeandikwa kwamba zisipulizwe kwenye moto, wala kuchomwa maana zinaweza kulipuka au kuspeed moto kuwaka.

Tuwaache wafanya biashara wa gesi na majiko waendelee kuuza maana sasa tunasababisha phobia ambayo haihusiani na matumizi ya majiko ya gesi (hata angepulizia kwenye jiko la kuni bado angepata ajali ya moto). Pia tuwe tunasoma masharti ya matumizi kwa vitu mbalimbali.
 
Yaani we mtu hebu badili kabisa heading ya thread yako,

Jiko la gas linahusishwaje moja kwa moja na shida iliyowapata hao wanandoa?

Vinginevyo hebu fafanua vizuri tukuelewe, kilicholipuka ni kopo la insectside au tank la gas au vyote viwili?

Km tank la gas lililipuka ni ktk mazingira yapi, fafanua
 
Yaani we mtu hebu badili kabisa heading ya thread yako,

Jiko la gas linahusishwaje moja kwa moja na shida iliyowapata hao wanandoa?

Vinginevyo hebu fafanua vizuri tukuelewe, kilicholipuka ni kopo la insectside au tank la gas au vyote viwili?

Km tank la gas lililipuka ni ktk mazingira yapi, fafanua
Huyu naye kaona mwenzake hapo juu kachangia na yeye anaiga tu
 
Back
Top Bottom