Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Je unatumia gas kwa kupikia?Tafadhali soma ujumbe huu na uchukue tahadhari ili isitokee kwako. Hili linaweza kuwa ni kosa la kawaida katika kila nyumba.JINSI ILIVYOTOKEA.jiko la gas lilikuwa linamewaka na mapishi yakiendelea.
Mama akaona mende jirani na sink la kuoshea vyombo. Mara akachukua kopo la dawa ya mbu na kupuliza karibu na lile jiko la gas linalowaka.Ulitoka mlipuko mkubwa na ndani ya muda mfupi yule mama alikuwa ameungua kwa asilimia 65.
Mumewe alikimbilia kuuzima ule moto na nguo zake nazo zilishika moto.Mumewe bado yuko hospitali akiuguza majeraha ya moto na bado hana habari kwamba mke wake alifariki alipofikishwa tu hospitali.
Ni vema tukafahamu kuwa dawa zote za kuulia wadudu "Hit", "Marten", "heaven", "Raid" n.k. zina mchanganyiko wa madawa mengi yanayosababisha mlipuko mkubwa.Mchanganyiko huu wa madawa ni rahisi sana kusababisha mlipuko haraka sana.
Tafadhali elimisha wanafamilia yako na rafiki zako kuhusu jambo hili na sambaza ujumbe huu.Tafadhali usiuhifadhi ndani ya simu yako, shirikisha wengine, huwezi jua utaokoa maisha ya watu wangapi. Mimi nimefanya kama nilivyopokea.