Ibilisi Mjalaana
JF-Expert Member
- Aug 13, 2019
- 8,297
- 16,529
Wana Jamii,
Tunaongea sana kuhusu "fizikia ni rahisi", au "hesabu za shule zinatosha kuelewa dunia"... lakini leo twendeni mbali zaidi kidogo.
Kuna equation moja ya dunia halisi—Navier–Stokes—ambayo inakataa kutii akili za watu kwa zaidi ya karne moja. Na ndio, anayefanikiwa kuielewa kikamilifu na kutoa suluhisho lake la jumla, anazawadiwa USD $1,000,000 na Clay Mathematics Institute.
Navier–Stokes ni nini?
Ni seti ya equations zinazofafanua jinsi vimiminika (maji, hewa, mafuta n.k.) vinavyotembea. Zinatumiwa kila siku:
Lakini bado, hatujui kama equation hizi daima zina suluhisho, au kama zinaweza kulipuka (infinite solution) bila onyo. Hilo ndilo tatizo!
Kwa nini ni changamoto?
Tatizo ni kwamba equation hizi ni nonlinear, zinahusisha derivatives za muda na nafasi, msuguano, na mabadiliko ya shinikizo—all in one. Katika mazingira mengi ya kweli (turbulence, pressure drops, variable boundaries), equation inakuwa ngumu kiasi kwamba hata supercomputers zinatoa makadirio tu.
Wito kwa Vichwa:
Kama wewe ni mmoja wa wale wanaosema “Physics ni rahisi,” “Calculus ni mchezo wa watoto,” au “Kariri formula tu maisha yanaenda,”...
Karibu hapa uonyeshe ubabe! Hii si mitihani ya kuchora graph darasani bali changamoto halisi ya dunia.
Je, kuna Mbongo anaweza kutupa mwanga?
Je, kuna kijana wa Kagera, Iringa au Mtwara anaweza kuvunja ukimya huu wa karne?
Karibu kwenye mjadala. Tunaweza pia kuchambua mifano rahisi ya Navier-Stokes na angalia pale equation inapoanza "kukataa kueleweka".

- Kuunda mabawa ya ndege
- Kutabiri hali ya hewa
- Kuelewa maporomoko ya maji
- Kupanga mifumo ya maji mjini