Kama mnawajua watajeni majina yao ,ndio mtawafahamu ni akina nanni na wanahusiana ni ndugu au watoto wa wakuu wakuu ,nyie andikeni majina yao hapa ,mtazidi kuzinduka.
Tumtafute Mungu na nguvu zake na mengine yote tutazidishiwa
Mathayo 19: 27 - 29
Ndipo Petro aka mwambia, “Na sisi tulioacha kila kitu tukakufuata tutapata nini?”
Yesu akawajibu, Ninawahakikishia kwamba, mtu aliyeacha vyote kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na atarithi uzima wa milele.
Kumbukumbu la Torati 28:1-19 SRUV
Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, kuongezeka kwa ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.
Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.