Je, unaweza kuacha mshahara wa milioni 7.8 na kuwa Mkuu wa Wilaya anayelipwa milioni 3 kwa mwezi?

MAMBO yamekuwa MAMBO. Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je, UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
Sema hao jamaa walivyo na hila. Wanakuteua ukikataa wanakubwaga kote.
Alafu nashangaa sana kwanini wasiteue watu wasio na kazi wamejaa Tele.
Kutafutiana ubaya tu
 
Ingekuwa maisha ya zamani UDC ni Sawa kabisa maana una uhakika wa miaka mingi hadi kustaafu au kupanda kuwa RC. Ila kwa sasa hapana aisee. Tena 2023 imebaki miezi michache mnaingia uchaguzi na mkeka mpya unatoka
Hapa ndipo tatizo linapoanzia. Kizazi cha nyoka kinafikiria kuiumiza nchi tu.
Kwani huwezi kuwa mtumishi wa umma bila kuwaibia wananchi?
 
Japhet Maganga Katibu mkuu wa chama cha walimu (CWT) aliteuliwa mkuu wa wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera. Ndugu Thadei Ole Mushi akasema Maganga atakataa huo uteuzi kwa sababu ana mshahara wa 7.8M kama Katibu mkuu wa CWT, lakini akienda kuwa DC atalipwa 3.5M.....Rais wa CWT na makamu wake wote wamekubali kuripoti kwenye wilaya zao jamaa ambae ndio katibu mkuu wa chama Cha walimu kagoma ,siku ambayo alitakiwa kuapishwa akaitisha kikao Tanga polisi wakaenda kumfata kwann kagomea teuzi wakamuhoji kwa dakika 50; jamaa kawaambia siwezi kuwajibu ninyi nitamjibu Alie niteua (Rais) unaambiwa kuandaa tshirts kwa ajili ya may mosi bajeti ni zaidi ya billion Moja jamaa kagoma kuacha hela ...na mama Samia alitumia busara kuwachagua Viongozi wa juu wa chama Cha walimu kuwa WAKUU wa wilaya kwasabab ya migogoro yao wote hawaelewani...pia kwa katiba ya Tanzania Rais anauwezo wa kumtoa hiki cheo ....ngoja tuone ataishia wapi
 
Acha uongo ww unajua trilion ww?
Piga idadi ya wilaya tanzania halafu assume tu nusu ya hizo wilaya wanapewa bajeti trilion ....

Na ufuatilie bajeti ya nchi uone ulichoandika ni kweli....na hapo kwenye bajeti bado ni kwa vitu vyote sio tu halmashauri
 
Una uhakika Rais wa CWT Leah Ulaya karipoti?

Martin Shigela (RC Geita) alisema mteule mmoja hakuwa ameripoti wala hakutoa taarifa yoyote kwenye ofisi ya muapishaji ambaye ni RC.

Unasuluhishaje mgogoro kwa kuwateua vyeo vingine watu wenye mgogoro?

Huu utaratibu mpya wa kutafuta suluhu haufai.

Au kuna kitu zaidi ya hiki tunachoaminishwa.
 
Hao viongozi wa CWT wanajielewa.Ya nini uache kazi permanent uende kuwa mkuu wa wilaya kazi ya kurisc,kutumbuliwa ni dakika sifuri. Bora kuwa CWT,muda ukiisha unarudi kuwa mwalimu na unaendeleza miradi yako swadka kabisa.
 
Hapa unamtia ubaya raisi na serikali kwa ujumla. Ukikataa Wala hakuna shida wengi tu wamewahi kukataa na hawakukutana na hayo unayosema.

Walichofanya ni kuijulisha mamlaka ya uteuzi na Wala hakutakua na shida. Tusiitie ubaya serikali Wala raisi, maana kesho ikitokea mmojawapo kaanguka au kafa ghafla mtaanza kusema ni serikali inahusika
 
MAMBO yamekuwa MAMBO. Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je, UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
Hapo inahitaji akili kidogo sana kupata jibu.sababu unaenda kwenye ajira ambayo kesho yake yanaweza tokea mabadiliko yakakuacha unashangaa tuu barabarani
 
Huwa nakuambiaga huna akili. Wilaya zipo karibu 130 nchi nzima. Ikiwa bajeti ni bil 500, tafsiri yake wilaya zote bajeti yake ni trillion 65. Hebu tuambia bajeti ya nchi ni kiasi gani? Na hapo bado bajeti za wizara na taasisi zingine.

Ukiwa huna akili usiwe unachangia mada
 
Humu wengi ni watu wajinga mno. Amini hivyo, wilaya zipo karibu 130, kwa anavyosema Ina maana bajeti ya wilaya zote ni trilion 130.

Sasa bajeti yq nchi nzima ni kiasi gani? Bado wizara na taasisi zingine
 
Unakubali .maan utatafuta sehemu ya kupiga.
Wala sihitaji kupiga, UPIGAJI ni upumbavu tu!
The fact kwamba mimi ni rais wa Wilaya na nilyeaminiwa na Rais wa JMT, nitaweza kubuni mradi wa maana sana na ambao lazima tu utanitoa. Advantage kubwa nitakayoitumia ni kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kukuwamisha mipango yangu HALALI.
Tatizo sisi wabongo tunapopewa nafasi za kufanya vitu HALALI ili tuweze kutoka, tunaanza kufikiria UPIGAJI; upigaji ni upumbavu tu.
Nchi hii ni ngumu kiasi; kiasi kwamba ukiamua kufanya kitu halali ukiwa ni mtu wa kawaida tu, UNAKWAMISHWA KWA MAKUSUDI. hata hivyo, ukiwa una cheo tuseme kama DC vile, hakuna business HALALI utakayoweza kubuni halafu akatokea mtu wa kukukwamisha, hayupo
 
Kitu kikubwa kinakuja mtakuja kuelewa tu achaneni na waropokaji malisa sijui Ole Mushi .
Wewe unaweza ukawa ni Nabii wa Karne katika hlii! Naelewa kabisa lecture uliyotoa hapa wala sihitaji tutorial kuweza kupata A kwenye mtihani kama mwanafunzi wako
 
Mambo yamekuwa mambo. Wewe ni mtumishi wa taasisi fulani unalipwa mshahara wa Tsh.Mil.7.8

Unateuliwa kuwa DC ili upate mshahara wa Tshs mil.3 na shangingi

Je, utakubali teuzi au utakataa?
yah inawezekana kwa mkereketwa wa CCM tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…