Je, unaweza kuacha mshahara wa milioni 7.8 na kuwa Mkuu wa Wilaya anayelipwa milioni 3 kwa mwezi?

Je, unaweza kuacha mshahara wa milioni 7.8 na kuwa Mkuu wa Wilaya anayelipwa milioni 3 kwa mwezi?

Chama wa Waalimu kina nguvu kuliko Rais kumbe[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Labda kama una maelewano mazuri na mkurugenzi wa halmashauri maana uko ndo kwenye pesa lasivyo utakuwa mpiga domo tu jukwaani. Ukiona mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri hawaelewani ujue mkurugenzi anakula peke yake
Yanii kama DC huwezi funga angalau 10mil kwa mweziii bora uingie field kama sabayaa tuu..
 
ILA watajutia kukataa uteuzi ni dharau na kibri kwa mkuu wa nchi....kuna kitengo kitashughulika nao tena kimyakimya bila kelele! Labda kelele watapiga wao na si ajabu mkashangaa watu wakakimbilia kuropoti.. Serikali ni sirikali haijawahi kushindwa!
Kukataa uteuzi sio kosa wala dhambi....halafu wao sio wa kwanza kukataa na huenda wasiwe wa mwisho pia.
 
MAMBO yamekuwa MAMBO .Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?

Ningependa Mh Rais ateue watu wengine hao waliokataa wasisumbuliwe siyo kila mtu anapenda "makamera/mataataa/sportslights ,ukiachana na mshahara mkubwa pia uDC/URC majungu mengi sana ,chawa wengi sana wanaleta fitina ,hizo nafasi ni za mpito anytime pdf linatoka na unawekwa nje ya ulingo.

Taasis ya uteuzi usiweke beef na hao watu kabisa ,waachwe waendelee na shughuli zao!
 
Labda kama una maelewano mazuri na mkurugenzi wa halmashauri maana uko ndo kwenye pesa lasivyo utakuwa mpiga domo tu jukwaani. Ukiona mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri hawaelewani ujue mkurugenzi anakula peke yake
Na ndicho kilichomuondoa Basila Mwanukuzi aligombana na DED ha ha ha haaa.
 
MAMBO yamekuwa MAMBO .Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
Q. Je, utakubali U-DC au utakataa?
A. Naukataa,
Q. Na marupurupu yake yote ikiwemo shangingi?
A. Nayakataa!
 
MAMBO yamekuwa MAMBO .Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
Nan huyo analipwa hio taasisi gan??
 
Mkuu wa wilaya ni mjumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya, ni Mkurugenzi mjinga tu peke yake ndio hawezi kwenda sawa na Dc ambaye kimamlaka ni mkubwa wake wa kazi.
Duuh!!! Unafurahisha miaka ile waziri mkuu anagomewa na mkuu wa wilaya hukuwepo enzi za jk!?
Kisiasa tu ndio mkubwa ila wote ni wataeule na kimamlaka ya utendaji mkurugenzi ndio anamamlaka zaidi.
Hujasikia hata lile sakata la mkurugenzi na mkuu wa mkoa kulalamika mkurugenzi anakula hela mwanza
 
Its pure political post, marupurupu ni mengi kama ukielewana ma Mkurungenzi. Bajeti ya Halmashauri nyingi ni zaidi ya Bil 500 hadi Trilion moja, sasa masalia lazima yatakufuata mezani ndugu...cha msigini ni kuelewana na Bajeti holder ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri - mnakula taratibuuu... sasa hiyo 9m ni kitu gani.
 
Unaposikia neno mkuu wa wilaya yeye ndio Rais wa wilaya hiyo, hakuna mkubwa zaidi yake, na yeye ndio Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama, anayo hata mamlaka ya kuamuru Mkurugenzi awekwe ndani kwenye serious issue.

Sijui shule huwa mnaenda kufanya nini?
 
ILA watajutia kukataa uteuzi ni dharau na kibri kwa mkuu wa nchi....kuna kitengo kitashughulika nao tena kimyakimya bila kelele! Labda kelele watapiga wao na si ajabu mkashangaa watu wakakimbilia kuropoti.. Serikali ni sirikali haijawahi kushindwa!
Kwani si tayari polisi wamewahoji kwa saa kadhaa?

Tatizo lao wameangalia mshahara tu hawakuangalia fursa zinazowazunguka za halali na zisiszo halali ambapo nyingi Ni zisiszo halali!

DC amepewa mamlaka ya kusimamia shughuli zote wilayani kwake kwa niaba ya Rais! Njoo kwenye miradi ya maendeleo (hapo ndo penye pesa)

Unless tuseme wameamua kuwa waadilifu Ila jekweli Ni waadili kwenye dhamana walizonazo?

Kimsingi watajuta sana, katika mojawawapo ya makosa makubwa kwenye state Ni kumgomea Rais, Ni dharau kubwa kwa nchi na serikali! Hawa viongozi wa cwt Ni waalimu na Ni waajiriwa wa serikali hiyo hiyo inayoongozwa na aliyewateua! Kesho wanaweza kupata uhamisho wa lazima wakapelekwa huko periphery of peripheral!

Wakiwa huko wakashindwa kutumiza majukumu yao kwa.mujibu wa katiba na kanuni za CWT hali itakayofanya waondolewe kwenye nafasi zao!

Watarudi kuwa waalimu wa kawaida and totally blacklisted kwenye appointments za serikali!

Wakijihushsha na shughuli binafsi Kama biashara TRA na associates wako nyuma yao,

Wakijihushsha na kilimo NEMC and associates wako nyuma yao!

Wakifanya makosa kidogo tu TANPOL wanajazia ya kutosha!

Kiufupi they will be haunted till down! Kuna watu tayari wanaandaliwa kuwa nyuma yao for pay! Mark my words

Bila kujali mshahara waneitikia wito wa Rais Basi!
 
Unaposikia neno mkuu wa wilaya yeye ndio Rais wa wilaya hiyo, hakuna mkubwa zaidi yake, na yeye ndio Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama, anayo hata mamlaka ya kuamuru Mkurugenzi awekwe ndani kwenye serious issue.

Sijui shule huwa mnaenda kufanya nini?
Mkuu hizo ni siasa tu, kiutendaji mkuu wawilaya hana kazi yeyote wala majukum yanayoeleweka.
Pili hao wote ni wateule wa raisi, mkuu wawilaya, mkoa au waziri mkuu wote hao hawana mandate yeyote yakumuwajibisha zaidi ya kupiga kelele raisi labda ndio amtengue.
Enzi za lowasa kuna mkuu wa wilaya alimgomea akamwambia mamlaka iliyokuteua ndio iliyoniteua
 
Its pure political post, marupurupu ni mengi kama ukielewana ma Mkurungenzi. Bajeti ya Halmashauri nyingi ni zaidi ya Bil 500 hadi Trilion moja, sasa masalia lazima yatakufuata mezani ndugu...cha msigini ni kuelewana na Bajeti holder ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri - mnakula taratibuuu... sasa hiyo 9m ni kitu gani.
Wewe unajuwa tender moja tu ta T-shirt za mei mosi CWT wanaorder za sh ngapi na commission inatoka ngapi?

Unajuwa kama walimu wana bank? Unajuwa kitega uchumi kama Mwalimu house pesa zinakwenda wapi?

Yani Mwalimu aliyekufundisha Wewe kukutowa ujinga simple tu unamuona yeye ndio mjinga?
 
Unaposikia neno mkuu wa wilaya yeye ndio Rais wa wilaya hiyo, hakuna mkubwa zaidi yake, na yeye ndio Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama, anayo hata mamlaka ya kuamuru Mkurugenzi awekwe ndani kwenye serious issue.

Sijui shule huwa mnaenda kufanya nini?
Na kama ulifuatilia pia kisa cha mkenda na kigwangala, kisiasa waziri ni mkubwa ila kiutendaji katibu mkuu ndio mwenye mamlaka.
Au kile cha Dorothy gwajima akiwa katibu na waziri wake.
Hivyo hivyo kwa waziri mkuu na katibu mkuu kiongozi,
Cdf na waziri wa ulinzi.
Wote mkiwa wateule wa raisi hakuna anayeweza kumuwajibisha mwenzake labda kufanyiana fitna tu
 
Mimi ningekuwa DC tu.

Kwanza marupurupu.

Ninaweza kukopa zaidi ya million 100 na kufanya miradi.

Ntaendeshwa na gari na kuwa bosi wa wilaya nzima.

Mwisho nitakuwa chawa wa mama hadi anarudishe Tena madarakani niendelee kula mema ya ya nchi.
umewahi kubeti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kutajirika kwa kuwa mtumish wa umma labda uwe mwizi, kutumikia wananchi ni wito na sio biashara, kama unaenda kwenye teuzi ili upate mshahara mnono na marupurupu bora usiende maana utaharibu tu legacy yako na unaweza kuishia gerezani
 
MAMBO yamekuwa MAMBO .Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
Teuzi haina security yoyote mteuzi akiamka vibaya hata kesho tu anakutengua. Uteuzi ni utumwa wa aina yake na unalazimika kuwa chawa kwa mteuzi
 
Wamefanya maamuzi magumu lkn mazuri - kosa halikutoka kwao wala kwa Rais isipokuwa timu ya vetting ndiyo iliyompa mteua taarifa za udhaifu.

Huwezi kuacha 7.3M afu ukaenda kukimbizana na madiwani kwa 3.9M. Afu siku za nyuma kulitokea tatizo mtu unateuliwa leo kesho unatumbuliwa. Usitese nafsi yko
 
Back
Top Bottom