SI KWELI Je, unaweza kujua kundi la damu la mtu kwa sifa alizonazo?

SI KWELI Je, unaweza kujua kundi la damu la mtu kwa sifa alizonazo?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Je, Kuna uhalisia wa kutambua sifa za mtu kutokana na kundi lake la damu? Au kundi la damu linaweza kuchangia tabia za mtu?
​
1791529887433.png

 
Tunachokijua
Damu zote zina kazi zinazofanana mwilini, lakini si damu zote zinazofanana. Aina za damu hutumika kuainisha damu ili watoa huduma za afya waweze kubaini kama damu ya mtu mmoja inaweza kuendana na ya mtu mwingine.

Uongezaji wa damu na upandikizaji wa viungo hutegemea ulinganifu wa aina za damu kati ya mtoaji na mpokeaji. Aina kuu za damu ni A, B, AB na O.

Madai

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na taarifa zinazosambaa zikieleza kuwa ni sifa za watu wa kundi la damu (O) , sifa hizo zimekuwa zikihusishwa na maeneo mbalimbali kama vile mahusiano nk.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa madai hayo yamekuwepo maeneo mbalimbali duniani ambapo huwa inaelezwa kuwa kulingana na kundi lake la damu mtu anaweza kuwa na mpole, mwenye hasira za haraka, mchangamfu nk.

Lakini uhalisia ni kuwa madai hayo hayana msingi wa kisayansi. Hakuna tafiti zozote za kisayansi zilizothibitisha uwepo wa madai hayo. Sifa za mtu zinatengenezwa na mambo mbalimbali na siyo kundi la damu. Mambo hayo yanaweza kuwa ni vinasaba, mazingira, uhusiano, ukuaji na uzoefu wake.

Judith Chale, Msimamizi wa Huduma za Wachangiaji Damu, Mpango wa Taifa wa Damu Salama anasema

“Hamna uhalisia kuhusiana na tabia za mtu na kundi la damu, hiyo ni dhana potofu ambayo baadhi ya watu wamekuwa nayo katika Jamii. Tabia ya mtu huwa inategemea mhusika na wakati mwingine mazingira, malezi au historia yake.”
U
Kila group la damu lina sifa zake. kama hizo sifa zipo kwa group la damu na rizazi, vipi kwa mtu mwenyewe!?
Mtu mwenye AB ni noma kwenye kujaribu vitu vingi.
Mtu mwenye A nature yake ni uaminifu.
...
Uliishia darasa la ngapi mkuu
 
  • Thanks
Reactions: apk
Hakuna ukweli wowote. Tabia za mtu anajifunza kutoka kwenye mazingira na nyingine za kurithi sasa group la damu linahusika vipi? Elimu ni muhimu sana
Kabisa watu ni mazwazwa sana hii nchi , Lowassa alikuwa sahihi kusema "Elimu,elimu,elimu" nchi inawapumbavu wengi sana sijui ndo mfumo wa elimu
 
Majinga majinga tu yanajiamulia mambo. Mechanism ya blood group na personal behaviours haipo. At least ingekuwa blood groups na magonjwa baadhi ina maana lakini eti "mimi group A ninapenda sana kukasirika bila sababu na nina hasira ya karibu 🤣🤣🤣"
Lowassa aliona mbali matatizo ya nchi yetu mengine yanasababishwa na ukosefu wa elimu. Jinga kabisa hao watu😂
 
Back
Top Bottom