Je, Kuna uhalisia wa kutambua sifa za mtu kutokana na kundi lake la damu? Au kundi la damu linaweza kuchangia tabia za mtu?
Your browser is not able to display this video.
Tunachokijua
Damu zote zina kazi zinazofanana mwilini, lakini si damu zote zinazofanana. Aina za damu hutumika kuainisha damu ili watoa huduma za afya waweze kubaini kama damu ya mtu mmoja inaweza kuendana na ya mtu mwingine.
Uongezaji wa damu na upandikizaji wa viungo hutegemea ulinganifu wa aina za damu kati ya mtoaji na mpokeaji. Aina kuu za damu ni A, B, AB na O.
Madai
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na taarifa zinazosambaa zikieleza kuwa ni sifa za watu wa kundi la damu (O) , sifa hizo zimekuwa zikihusishwa na maeneo mbalimbali kama vile mahusiano nk.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa madai hayo yamekuwepo maeneo mbalimbali duniani ambapo huwa inaelezwa kuwa kulingana na kundi lake la damu mtu anaweza kuwa na mpole, mwenye hasira za haraka, mchangamfu nk.
Lakini uhalisia ni kuwa madai hayo hayana msingi wa kisayansi. Hakuna tafiti zozote za kisayansi zilizothibitisha uwepo wa madai hayo. Sifa za mtu zinatengenezwa na mambo mbalimbali na siyo kundi la damu. Mambo hayo yanaweza kuwa ni vinasaba, mazingira, uhusiano, ukuaji na uzoefu wake.
Judith Chale, Msimamizi wa Huduma za Wachangiaji Damu, Mpango wa Taifa wa Damu Salama anasema
“Hamna uhalisia kuhusiana na tabia za mtu na kundi la damu, hiyo ni dhana potofu ambayo baadhi ya watu wamekuwa nayo katika Jamii. Tabia ya mtu huwa inategemea mhusika na wakati mwingine mazingira, malezi au historia yake.”
Kila group la damu lina sifa zake. kama hizo sifa zipo kwa group la damu na rizazi, vipi kwa mtu mwenyewe!?
Mtu mwenye AB ni noma kwenye kujaribu vitu vingi.
Mtu mwenye A nature yake ni uaminifu.
...
Kila group la damu lina sifa zake. kama hizo sifa zipo kwa group la damu na rizazi, vipi kwa mtu mwenyewe!?
Mtu mwenye AB ni noma kwenye kujaribu vitu vingi.
Mtu mwenye A nature yake ni uaminifu.
...
Wahuni tu mnashindwa kutofautisha group O na introverts ,omnivents na extroverts
Mimk ni introvert na sipo group O .
Ni uhuni tu unakuta jitu linaropoka kabisa eti me group O ukinipigia cm sipokei tena jingine toto la kiume kabisa
Majinga majinga tu yanajiamulia mambo. Mechanism ya blood group na personal behaviours haipo. At least ingekuwa blood groups na magonjwa baadhi ina maana lakini eti "mimi group A ninapenda sana kukasirika bila sababu na nina hasira ya karibu 🤣🤣🤣"
Lowassa aliona mbali matatizo ya nchi yetu mengine yanasababishwa na ukosefu wa elimu. Jinga kabisa hao watu😂