Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,702
Utakuwa unamuoa mama akokwang me nitakuwa nip teyal kumpa baba pesa ili akamilishe mahali sio big inshu wala nn nadhan hata kidin inakubalika
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utakuwa unamuoa mama akokwang me nitakuwa nip teyal kumpa baba pesa ili akamilishe mahali sio big inshu wala nn nadhan hata kidin inakubalika
Boss swala la kulipa mahali sio kuoa ... ndo maana unawez ukawez hata ww kumlipia mahar mtu mwngne ili aoe swala la ndoa linakamilika kwa uwepo wa wali wa bibi harus ( wenye idhini ya kumuozesha bi harusi , bi harusi mwnyw ( aliyelidhia) , muoaji ( babu harusi , mfungishaji ndoa ( Sheikh) na mashaidi bc wakipatkn watu ao ndoa tyal.Utakuwa unamuoa mama ako
Hao ndio wale watu wanadai mpaka maiti, huwezi kuishi na mwanamke mwenye roho ya hivi kwenye ndoa, ni chake chake, usitegemee kama atatumia hata mia yake kwa matumizi ya familia.hii KALI
😀😀😀.anadai ni HAKI yake ..ndo maana vipigo na manyanyaso hayaishi kwa wanawake kwa akili hizi...Hao ndio wale watu wanadai mpaka maiti, huwezi kuishi na mwanamke mwenye roho ya hivi kwenye ndoa, ni chake chake, usitegemee kama atatumia hata mia yake kwa matumizi ya familia.
Huyo ni bidhaa, Sasa bidhaa yoyote lazima uitreat hivyo kwa sababu yeye mwenyewe anajuwa amenunuliwa, na ukinunuliwa huwezi kumpangia mnunuzi.😀😀😀.anadai ni HAKI yake ..ndo maana vipigo na manyanyaso hayaishi kwa wanawake kwa akili hizi...
Mkuu, suala la mahari haiishi mimi niliona linakuwa mzigo kwangu, nilitafuta kiasi chote kilichobaki nikalipa chote, sikutaka kuendelea kusumbuliwa (and I was just thirty by then). Kwa sasa maisha yangu yako super kabisa, kwa ajili ya support wakiniomba sasa hivi kama ninacho nawapa kama sina nawaambia, hamna ule usumbufu tena!Hapa hakuna mjadala wowote, mahari huwa haimaliziwi yote hata uwe na ukwasi kiasi gani.
Wanachomtendea baba yako ni mambo ya kihuni tu na kukosa ustaarabu na issue siyo mahari.
Angekuwa amekwenda ukweni na Prado kumfuata mke wake na kuwapiga offer za bia wajomba zako haya usingeyasikia, Tena mama yako angefukuzwa kwao arudi kwa mume wake haraka.
In short poverty is decease, kama una pesa za kumsaidia mpe, unampa pesa yeye si kwamba wewe ndio unamalizia mahari, elewa vizuri sentesi hii, msaidie baba yako pesa anayokuomba, na usimpangie matumizi ya pesa hiyo yeye ndio atapanga matumizi ya pesa hiyo.
Ni uchuro kusema eti unamlipia baba yako mahari unatafuta laana, hujui mpaka hapo ulipofikia baba yako amepambana vipi au ameuza asset zake ngapi kuhakikisha wewe unakuwa na unasoma.
Nimemaliza.
Hiyo si mahari unamlipia, ni pesa ya dharula bila kujali inaenda kufanya kazi gani.Mambo vipi wanajamvi!
Nakuja na mada yangu inayohusu kumlipia mahari baba yako pale ambapo hali yake kiuchumi si nzuri. Umeshawahi lifikiria suala hili? Twende pamoja!
Iko hivi, baba na mama yako walioana miaka mingi iliyopita bila ya hata baba yako kumalizia mahari ukweni. Ahadi ya baba mzazi kwa wakwe ni kuja kumalizia taratibu huku wakiwa wanaendelea kuishi na mkewe (mama mzazi).
Wakwe wanamkubalia baba kuishi na mkewe kwa kuwa tayari amekwishalipa sehemu ya mahari. Kwahiyo, wakwe wanaamini kwamba baba angelimalizia mahari siku zijazo kwa kuwa tu uchumi ni mgumu kwake. Maisha yanaanza kati ya baba na mama; unazaliwa wewe na wadogo zako kadhaa lakini mahari bado haijakamilishwa.
Mnakuzwa na kulelewa kiugumu ugumu hivyo huku mahari bado hajikamilishwa. Watoto mnakuwa wakubwa na kuanza shule, kisha kumaliza shule kwa ngazi ya msingi, sekondari, na pengine vyuo huku baba bado mahari hajakamilisha.
Watoto mnaanza kujitegemea kimaisha na pengine Mungu amewajalia hali nzuri kiasi ya maisha bora, lakini baba mzazi bado hajakamilisha mahari. Kumbuka kwamba, ninyi watoto tangu kuzaliwa na kukua kwenu, hamkuwahi kuambiwa na wazazi wenu suala la ukamilishaji wa mahari; yaani si baba wala mama mzazi ambaye amewahi kuwatamkia kwamba "Baba yenu hajakamilisha mahari".
Baada ya ninyi watoto kuanza kujitegemea, na Mungu kuwainua kiuchumi kwa kiasi chake, siku moja baba na mama wanakorofishana na hatimaye mama mzazi anaamua kurudi kwao (ukweni kwa baba mzazi). Ndugu wa mama wanamjia juu baba kwa unyama wa kipigo aliyomfanyia mama. Baba anaomba msamaha na kuomba/kuhitaji mkewe arudi nyumbani ili maisha yaendelee.
Ndipo ndugu wa mama wanafungua faili la madai na kukuta baba hakumaliza mahari ya mkewe; ndugu wanatoa sharti kwamba ili mkewe arudi, lazima kwanza mahari ikamilishwe, la sivyo mkewe hawezi kurudi na ataendelea kuishi ukweni kwa muda wote mpaka pale mahari itakapokamilishwa.
Baada ya baba kupewa sharti hilo, hali inakuwa ngumu kwake kutimiza takwa hilo kwa muda wa haraka. Mkewe anamuhitaji, kaomba msamaha wa kadhia ya kipigo alichompa mkewe, mkewe na ndugu zake wanaupokea msamaha, lakini, changamoto ni mahari bado hajakamilisha.
Sasa je, afanyeje ili kumkomboa mkewe? Pesa ya haraka hana, hata kama atadunduliza kwa muda wa miezi sita hawezi kufikia kiwango cha mahari alichobakiza. Hii ni kwasababu kazi anayofanya baba ni yenye kipato duni sana. Ndipo wazo linamjia baba kwamba msaada pekee wa kumkomboa mkewe ni kutoka kwa watoto.
Baba anakuja kwako kukueleza tukio zima la kukorofishana na mama yako, na pia sharti alilopewa la kumkomboa mkewe. Kisha baba anakuomba msaada wa pesa iliyobakia ya mahari ili akalipe kwaajili ya kumkomboa mkewe. Wewe binafsi unatahamaki kusikia baba hakuwahi kumaliza mahari, ndipo siku hiyo unajulishwa ili umsaidie kiasi hicho cha pesa akamalizie.
Wewe kama mtoto uwezo kiuchumi siyo mbaya sana, hali ya kiuchumi inakuruhusu kumsaidia kiasi cha mahari kilichobaki. Swali ni je, utakuwa tayari kumsaidia baba yako kiasi hicho cha mahari kilichobaki ili akamkomboe mama yako na kisha maisha yaendelee?
Karibu kwa mjadala.