Je, unaweza kumpa wanafunzi au mwanao Elimu ya Afya na uzazi wa mpango?

Je, unaweza kumpa wanafunzi au mwanao Elimu ya Afya na uzazi wa mpango?

Ali Nassor Px

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,384
Reaction score
3,926
Dunia ya sasa imebadilika sana. ni ukweli uliowazi kabisa kuwa ngono kimekuwa sio kitu cha siri sana.

Na uwepo wa ujuaji wa watoto kuhusu ngono umechochewa na mabadiliko mbalimbali yaliyopo ikiwemo Utandawazi kama vile Simu za mikononi, Television na hata muingiliano wa tamaduni za jamii mbalimbali huku waathirika wakubwa wakiwa ni watoto wa kike wanafunzi na hata wa kiume pia.

Athari hizo ni kama vile mimba za utotoni, utoaji mimba, ukahaba, magonjwa ya zinaa na mengine mengi.

Waathirika wakubwa ni watoto kati ya miaka 9 - 17 ambao kuumri wao ni wanafunzi.

Je, wewe kama mzazi unaweza kumpa elimu ya uzazi wa mpango ( unayohusiana na kutokupata mimba zisizotarajiwa ikiwepo njia za kujingika kutopata mimba).

mtoto wako ambae ni wanafunzi? Kama unaweza, Je kwanini unaweza kumpa elimu ya uzazi wa mpango.

Na kama hauwezi, je kwanini hauwezi kumpa elimu ya uzazi wa mpango?

WOTE MUNAKARIBISHWA KUCHANGIA MADA KARIBUNI SANA WANA JF.

Changia kama wewe ni mzazi vaa vazi la baba/ mama
 
Binafsi naona inawezekana, as long mtoa elimu ametch jinsia na mtoto.

Hapo kwenye kuweza ili nitoe maelezo na wewe funguka kwanza hii ni research au?
 
Sijaelwwa uzazi wa mpango kivip!!! Yaani kupangalia familia kwa idadi ya watoto au kutopata mimba zisizotarajiwa ?
 
Sioni tatizo kwa aina ya maisha tuliyonayo sasa. Kukaa kimya bila kuzungumza nao ni hatari zaidi kuliko kuwaweka wazi. Dhana ya kusema ukimueleza ndio unamuweka katika exposure ya kujaribu naipinga. Ni muhimu sana. Baba aongee na wa kiume, mama na wa kike
 
Binafsi naona inawezekana, as long mtoa elimu ametch jinsia na mtoto....

Hapo kwenye kuweza ili nitoe maelezo na wewe funguka kwanza hii ni research au?
Ni research binafsi nimejaribu kuonhea na watu wengi wanasema kumfundisha mtoto wa kike kujilinda kwa kushirika tendo la ndoa kwa kuvaa condom na kutumia njia za kudhibiti mimba ni uhuni
 
kutokupata mimba zisizotarajiwa ikiwepo njia za kujingika kutopata mimba
Watanzania haswa watoto Wana akili mbaya unaweza kuwa unawapa elimu nzuri ila ndo kama unawafundisha..

Swala la mimba kwa kweli ni ngumu wanajiachia mno akishaanza michezo iyo basi ni hatari sana ipo siku atakuja kunasa tu.
 
Sasa tunawaokoa vipi hawa watoto tuwaambie ukweli au tukae kimya
 
Sioni tatizo kwa aina ya maisha tuliyonayo sasa. Kukaa kimya bila kuzungumza nao ni hatari zaidi kuliko kuwaweka wazi. Dhana ya kusema ukimueleza ndio unamuweka katika exposure ya kujaribu naipinga. Ni muhimu sana. Baba aongee na wa kiume, mama na wa kike
Kweli ila je hauoni kama tunaweza kutoa elimu ambayo sio kwa watu sahihi na wakati sahihi.

Tunamruhusu mtoto wa kitanzania ajikinge kwa kuvaa kinga hapa tutatarajia nini baadae
 
Sasa tunawaokoa vipi hawa watoto tuwaambie ukweli au tukae kimya
😂😂😂Kule shule wanaanza kupractise wakianza kusoma reproduction..ni balaa kuwaaambia tu haswa madhara na kuwalea kweny mifumo ya kiroho ..

Final Linaweza kutokea lolote hata mtoto awe vip ,anaweza kuwa gate kali akaja kupewa mimba na house boy.
 
😁😁😁😁 kwahiyo tumekosa solutions tunasubiri upepo wa kisurisuri ufanye maajabu yake
 
Back
Top Bottom