Je, unaweza kumshauri mwanao kuwa msanii?

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Mimi hapana kabisa.

Kibongobongo mwisho wa maisha ya ustaa kwa asilimia kubwa huwa mabaya sana ya kutia huruma.

Nimeanza kufatilia sanaa ya bongo (muziki/muvi) tangu miaka 90 mwishoni lakini hadi leo hii watu 'waliotoboa' kupitia sanaa zao ni wa kuhesabika.

Wengi wameishia kuwa maskini wenye majina makubwa na kugeuka kichekesho mbele ya jamii kiasi kwamba wanajuta kwanini waliwahi kuwa 'mastaa'.

Je, unaweza kumshauri mwanao kuwa msanii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah! kwa jinsi teknolojia inavyokua wala sina wasi wasi kwamba sanaa itakuja kumlipa.

Ukimtazama Mr Nice wa enzi zake na Diamond wa sasa utagundua ni watu walio sawa ila Diamond anaonekana kufanikiwa kwa kuwa amewika kipindi ambacho teknolojia imekua ndio maana ameweza kuvuta mipaka mpaka duniani.

Hebu jaribu kuwaza Diamond bila youtube, instagram na the like, angeweza kutoboa mpaka Nigeria?

Wasanii wa enzi za Mr Nice walikua maarufu sana E.A kwa sababu ya ukaribu.

Hata wewe jiulize enzi za kina Mr Nice, je wasanii wa Nigeria walikua wanatamba huku kwetu? jibu
 
Hata enzi hizo ni wangapi waliofanikiwa kuwa kama Mr. Nice? Utagundua ni yaleyale mmoja kati ya maelfu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je kati ya maelfu ya wasanii waliowahi kufanya vizuri, tunaweza kuwa na listi ya wasanii angalau hata 200 wa kujivunia kwamba wameweza kusimama vizuri kimaisha kupitia sanaa (achana na hawa wadangaji[emoji1])

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mda mwingine specify msanii wa nini ? Je unaongelea hadi msanifu majengo sababu yeye pia ni msanii ......futa hio mindset mlee mwanao katika maadili mazuri jaribu pia kumfundisha mambo ambayo haya fundishwi shule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna dogo huku hataki shule hata kidogo.. yeye ana mpango wa kuwa kama Mondi anaamini mziki utamtoa.

Nafuatilia uzi huu kwa karibu sana.
 
Kuna dogo huku hataki shule hata kidogo.. yeye ana mpango wa kuwa kama Mondi anaamini mziki utamtoa.

Nafuatilia uzi huu kwa karibu sana.
Stereo anakuambia

Usiache shule mziki haulipi dogo, kua hapa kunahitaji miaka wiki ndogo.../
 
Wapi Saida Karoli? Mr. Nice? Feruz? 20%? Z-Anto? Matonya? Marlaw? Afande? Daz Baba? OTen? Joslin? Caz T? Zay B? Sister P? Wagosi? Inspector? Dudubaya? Chid Benz? Mwinjuma Muumin? Ally Choki? Badi Bakule? Banza Stone(kabla hajafa)? Ngwea (kabla hajafa)? Bambo? Norah? Kibakuli? Matumaini? Sinta? Nina?Johari? Na list ndefu inaendelea.... Hao ni baadhi tu ya wasanii waliowahi kufanya vizuri, je maisha yao kwasasa yakoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto kama hao ni wa kutia bakora kilasiku

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tumetia bakora na kumsimamia akisoma kila siku.. kumbe jamaa anasoma kama nusu saa masaa mengine ukitoka anaanza kutunga mistari.

Nimemtafutia historia za wasanii waliosugua miaka zaidi ya 10 bila kutoboa.. nikamtafutia history za wasanii wenye elimu na wanaofanya vizuri kwenye mziki.

Lakini dogo anaona kama vile mimi namuonea wivu na kipaji chake.. eti sitaki afanikiwe kimuziki ndio maana namwambia asome.
 
Nasikia Mr. Nice ana ela mpaka anagongwa bia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia Daz baba anavuta bangi maeneo ya tbt segerea
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wangu mimi wananidai ada ya shule na ushauri tu, huko mbele ya safari wafanye maamuzi yao wenyewe kwenye maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…