Je, unaweza kumshauri mwanao kuwa msanii?

Wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa (bongofleva) kwa harakaharaka ni kama;

*Diamond
*Alikiba
Harmonize
Rayvanny
Nandy
Jux
Aslay
'Weusi'
'Navy Kenzo'
Vanessa
Mbosso
Lavalava
Ney Mitego
Ben Paul
Marioo
Barnaba
Janjaro
Whozu
Ruby
Maua Sama
Darassa
Ommy Dimpoz
Bill Nass
Young Killer
Young D
Luludiva
Giggy
Mimi Mars



N.k

Je uhalisia wa maisha yao unaendana na majina yao, ukiacha hao wawili niliowawekea nyota ambao angalau wengi tunafahamu maisha yao



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini umzuie kufanya mziki? Ongea nae kirafiki tena sana mtaenda sawa, si unajua binadamu huwa tunakua na hulka fulani hivi ya kutaka kujua kwa nini kitu fulani kinazuiwa?

Ushauri wangu jaribu kumuongoza awekeze katika vyote viwili, elimu na sanaa, unapomkataza kufanya sanaa na kumlazimisha kwenye elimu au kumfundisha mtazamo hasi wa sanaa ndio utampoteza kabisaaa.

Nenda nae taratibu tu ikiwezekana mlipie na studio arekodi singo, hata kama uko vizuri mlipie na collabo ya msanii mkubwa anaempenda(wasanii wetu hata laki anafanya kollabo).

Kumkataza kabisa kufanya mziki na kumshauri asome tu hiyo ndio tunaita kuendeleza cycle ya umasikini, kama kweli ana kipaji usisite kukiendeleza maana hatujui kesho yetu. Vipi kama akisoma halafu akaja akawa ni hawa wanaokosa ajira? utamshauri auze karanga mtaani?

Muhimu zungumzeni na kisha mfikie muafaka kwamba kusoma atasoma na muziki atafanya.
 
Hata enzi hizo ni wangapi waliofanikiwa kuwa kama Mr. Nice? Utagundua ni yaleyale mmoja kati ya maelfu

Sent using Jamii Forums mobile app
Je huyo mmoja kati ya maelfu unayosema umeshamjua ni nani? huenda ndo huyo mwanao utakaemkataza.

Binafsi mimi sitakuja kumzuia mwanangu kama atahitaji, ila tutawekeza kotekote(elimu na sanaa)
 
Je huyo mmoja kati ya maelfu unayosema umeshamjua ni nani? huenda ndo huyo mwanao utakaemkataza.

Binafsi mimi sitakuja kumzuia mwanangu kama atahitaji, ila tutawekeza kotekote(elimu na sanaa)
Uwezekano wa kutoboa upo ila probability ni ndogo mno, je utamshauri mwanao awekeze sehemu ambayo ni kama gambling?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wonderful contribution
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wengi wao walikuwa hawana elimu na hawakufanya muziki kama business. Fuatilia wasanii kama jay z au P didy wamepata mali zaidi nje ya muziki yaani ukishakuwa kwenye spotlight tayari ni platform ya wewe kufanya zaidi ila kibongobongo ni upuuzi tu wa ngono na pombe kama tulivyo mtaani

Mtoto wangu akiwa na kipaji exceptional !!!.... sio kumruhusu tu, ntakuwa manager wake kabsaaa 😊😊😊ili kuhakikisha anakuwa brand na jinsi ya kutengeneza pesa lakini anapata elimu ya kumsaidia hata nisipokuwepo duniani

Bila sacrifise za wazazi leo usingemjua Beyonce, Michael Jackson au hata kibongobongo Diamond platnumz
 
Maisha ya usanii ni magumu sana,unakuwa na jina kubwa ila huna kitu ,au unaweza kuwa kwenye peak ukafanikiwa lakini talent tu ikishuka hata kama umeinvest sana na una mali kama huzungumzwi lazima upate stress ,unakuta msanii alikuwa peak na jina kubwa lakini baada ya kufulia haheshimiwi tena na akikumbuka kina Poshie queen hawezi tena kuwamudu na kwenda mahotelini na baa kali basi lazima avute unga

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Kwa mbele wengi wanatoboa kiukweliukweli, ndo maana nimezungumzia kibongobongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida kweli, hakuna kitu kigumu kama kuwa na jina kubwa halafu huna hela, maana utatamani uishi kama jina lako ila pesa hakuna je nini kinafuatia? Ndio maana wengi wanajaribu kufake maisha, ila kufake maisha kuna mwisho wake kuna muda utafika hata kufake haiwezekani tena hapo ndipo stress zinaanza
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mbele wengi wanatoboa kiukweliukweli, ndo maana nimezungumzia kibongobongo

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata kibongobongo kuna Vanessa na Diamond ambao wanafanya wonders na wanafika mbali kupitia muziki...

Kwanza bongo kuna sponsors na sio managers. Mtu ana pesa ya studio na video then nae ni manager !!!...

Manager anapaswa kuajiriwa na msanii, ajue jinsi ya kumkuza na kumletea biashara. Ndo maana Vee na mondy wana manager zaidi ya mmoja na wanafika mbali..

Bongo artists hiki kitu hawana plus nidhamu, elimu wala time ya kuwekeza katika brand zao.. sasa hapo unatokaje mkuu
 
Niliskia Diamond anakesi kafunguliwa na landlord wake kasababisha hasara kwenye nyumba ya watu na ana madeni ya kodi zaidi ya milion 400

na saizi show zimebuma labda views
Mondi kafanikiwa Sana alafu anadaiwa kwenye jengo la biashara tokea arudi bongo kutokea ufaransa umesikia Tena anadaiwa? diamond ni balozi wa kampuni 7 kubwa Pepsi,niceone,voda, parimatch n.k hapa nchini moja ni kinywaji Cha ufaransa ukija kwenye label yake kaajilri si watu chini ya 60 hapo ujazungumzia media, mauzo ya nyimbo, pesa za show n.k
 
unaongea kiushabiki...............kumbuka kama ni pesa za show kuna middle men wanakula chao,kuna kulipia ukumbi waweza shangaa watoka na 20% ya hela uliyoingiza........kuhusu media kumbuka kunawatu wameweka hela zao wkala dili naye kwa kutumia jina lake....nahauwezi jua mkataba wake na wamiliki halisi ukoje..waeza shangaa halipwi ila wakamuhakikishia kumpa airtime ya nyimbo zake na kumtangaza only that
behind the scene biashara sio simple kama udhaniavyo.......wawekezaji hawawezi kubali kulaliwa kizembe!!!
 
Wewe ndo unaongea kiushibiki angekuwa aingizi hela si angekuwa Kama Mr nice,juma nature
 
Wewe ndo unaongea kiushibiki angekuwa aingizi hela si angekuwa Kama Mr nice,juma nature
tusibishane,nauhakika kuwa hata connection na hawa watu huna...............achana na ubishi na watu ambao tuna connection huku juu
na nina imani hata exprience na hizi kazi huna
 
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…