Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Haha basi watanzania tunatabu sasa nikienda ubungo inter niseme asante magufuli, uwanja wa taifa niseme asante mkapa kwene mabarabara kibao hapa nchini nisemage asante kikwete asante kikwete khaaaa!!!
 
Nenda kaulize wizara ya madini utapewa mkataba, huwezi kuweka mkataba hadharani punguani mkubwa we.
Sheria haisemi nikaulize wizara ya madini.sheria inataka mkataba upelekwe bungeni.lakini pia mkataba huo ni dhidi ya nani na nani? Je ni dhidi ya magu na Barrick au Barrick na watanzania(nchi yetu) sasa hiyo siri ni dhidi ya nani?I am so sorry for you dude
 
Nenda kaulize wizara ya madini utapewa mkataba, huwezi kuweka mkataba hadharani punguani mkubwa we.
Japo kweli baadhi ya wenzetu wengine humu ni ma punguani, lakini sio vizuri kumtukana hivyo mwenzetu humu, sio yeye ndie ametaka kuwa punguani, amejikuta hivyo!.
Usimtukane mtu kutokana na hali yake.
p
 
Flyover ya TAZARA na Ubungo Interchange hata Chalinze Express way, ni miradi iliyobuniwa na kutengewa bajeti ya upembuzi yakinifu na hatimaye kufanyiwa upembuzi yakinifu uliokamilika wakati wa Serikali ya Kikwete.

Mradi wa Tazara Flyover tena ulipatiwa financing kabisa kutoka serikali ya Japan mwaka 2015, wakati huo JK akiwa raisi.

Mradi wa ubungo Interchange ulishatafutiwa hela huko Worldbank kabla hata Magufuli hajawa raisi, Magufuli kaingia madarakani kakuta msosi uko jikoni unapikwa!!

Maelezo yote hayo yapo kwenye Ripoti Maalum ya mwaka 2015 ya aliyekuwa Waziri wa Ujenzi kwenye serikali ya JK huyohuyo ndugu Magufuli kuhusu miradi ua ujenzi ya serikali ya awamu ya nne kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.

Paschal Mayala Soma huu uzi hapa chini, Kisha soma hii pdf nakuwekea kwenye attachment.

Tujikumbushe: Waziri Magufuli alipotoa waraka wa mafanikio ya Rais Kikwete kwenye mambo ya ujenzi kuanzia mwaka 2005 hadi 2015
 

Attachments

Hizi data zote ukizitaka utazipata kwa kufuata njia zinazokupasa kuzifuata.

Huwezi kupata hizo taarifa kwa kulalama na kutukana humu jamiiforum.
 
Japo kweli baadhi ya wenzetu wengine humu ni ma punguani, lakini sio vizuri kumtukana hivyo mwenzetu humu, sio yeye ndie ametaka kuwa punguani, amejikuta hivyo!.
Usimtukane mtu kutokana na hali yake.
p
Nimekusoma kaka, maana hayo maandishi yako pia ni matusi yaliyoandikwa kistaarabu.

Sio tatizo kaka sitarudia tena kumwambia mtu ukweli hadharani.

Halima Mdee juzi alikuwa bunju B, anatumia njia ile ile ya clips za Gwajima za miaka ya nyuma, kwa maoni yako njia hiyo haiwezi kumuathiri Gwajima kuelekea Oktoba 28?.
 
Nilikuwa nakuheshimugi ila akili yako imekuwa ndogo nadhani ata mtoto wangu kakuzidi kwa sasa
 
Yani majukumu ya serikali leo hii inageuka fadhila? Halafu huyu anaesema haya ni mtu mwenye LL.b hahahah...😀😀😀😀
Hawa ndiyo aina ya wasomi walijaa Tanzania ambao ni wanafiki wakubwa kazi kujipendekeza na kuweka njaa mbele badala ya maslahi ya taifa
 
Naomba sababu tatu tu, kwanini nisiseme ahsante walipa kodi watiifu niseme ahsante Magufuli ambaye tumemtuma asimamie vizuri fedha zetu ili zilete maendeleo kama hayo!?
Kama ni mtu alitoa pesa yake mfukoni tutasema asante, hatutaki kufundishwa ujinga na unafiki
 
Miongoni mwa wadau nisiowaelewa katika kipindi cha awamu ya tano ni pamoja na Paschal Mayala
 
Wewe ni mbumbumbu!Kwa nini useme asante kwa mtu kutimiza wajibu wake?Yaani mtu nampa kodi yangu ili akanitengenezee miradi ya maendeleo na kisha namlipa mshahara kama ujira wake halafu nimpe asante ya nini?Unafikiri kila Mtanzania ni mbumbumbu kama wewe?
 
Huyu jamaa kawa banned? Naona picha yake hapo ina wino mwekundu
 

Attachments

  • Screenshot_20201020-073541.png
    17.9 KB · Views: 2
Sio tu upembuzi yakinifu bali pia hata pesa zilitafutwa na awamu iliyopita!

TAZARA Flyover kwa mfano, mkataba wa utolewaji pesa ulisainiwa Oktoba 2015.

Watu wasichojua kuhusu Ubungo Exchange ni kwamba huu ni mradi ule ule wa BRT! Baada ya plan ya awali kuonekana italeta usumbufu pale Ubungo, JK akakaa na timu ya watalaamu wa TANROADS ambao wakashauri pale Ubungo ijengwe interchange.

Baada ya JK kukubaliana na ushauri huo wa watalaamu, akaagiza wahusika warudi tena kwa World Bank ambao ndio wafadhili wa BRT, na June 2015, JPM akiwa Waziri akaongea bungeni kwamba hatimae World Bank wamekubali kugharamia Ubungo Interchange!

 
Ile ni asante Kikwete. Jpm alikuta kula kitu mezani kuhusu daraja hilo. Myonge mnyongeni, haki yake mpeni. Ahsante JAKAYA MRISHO KIJWETE kwa flyover ya Ubungo.
 
Kwa hiyo na sisi tunaotumia reli ya kati Dar hadi Kigoma vp tuanze kupambana ili mjerumani arudi tena kutawala Tanganyika maana kama miaka hiyo alijenga hii reli si leo tungekua na underground railway network hapa dsm? This is Very cheap Paskal.

Sent from my itel P13 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…