Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Yani majukumu ya serikali leo hii inageuka fadhila? Halafu huyu anaesema haya ni mtu mwenye LL.b hahahah...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
LLB ya wapi hamna kitu hapo.

Amekariri vijikanuni vichache vya constitutional law anawapoteza wajinga wasioijua sheria!

Huyo jamaa ni mjuaji asiyejua kitu.
 
Nchi ya kuomba, kushukuru, kupongeza, tumerudi utumwani
 
Unafiki bana...washukuru na walipa kodi kwanza

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Mbona hujawashukuru wajerumani kwa kuwajengea treni kutoka Mwanza kwenda Dar kuwaleta wasukuma mjini na ZNZ kwenye kazi za kilimo?
 
Chadema wamepata fedha kutoka kwa wafadhili wa nje na ndani, wabunge wao, michango ya Wananchi n.k lakini wameshindwa sio kujenga tu ofisi bali hata kukarabati au kupiga rangi. Apo ndipo tofauti ya uongozi ilipo.
Baada ya uchaguzi tutawafurumisha kutoka kwenye majengo yetu tuone kama mtapata hata wa kuwapangisha kibanda.
 
Paskali
Kwamba intachenji imejengwa na fedha za mfukoni za Magufuli?
Kutoka kuwa great thinker hadi praise team
 

Huyu Magufuli ni msanii kwerikweri!!Huyuhuyu alikuwa akiwananga Marais walopita kuwa hakuna walichofanya yaani yeye ndani ya miaka 5 amefanya kila kitu........!Chizi kabisa.
 
Unazungumzia interchange hii mkuu?View attachment 1605765

Huyu Magufuli na ri-CCM lake ni kuwapiga chini come 28 October,2020!
Yeye aliona Ubungo Interchange na Mfugale Flies(not Flyover) ni muhimu sana kuliko kuboresha miundo mbinu ya mitaro/mifereji ya maji. Matokeo yake Watanzania 13 waso na hatia wamepoteza maisha!!What a shame is this?
 
Nimepita mara nyingi sana pale. Inshort naipongeza serikali, lakini hili la kusema asante[emoji848][emoji848]
 
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Leo nimepita Tanzanite Bridge, nikamkumbuka JPM, kwa yeyote anayekatiza hapo, lazima atamkumbuka JPM na kumshukuru japo kimoyo moyo. JPM ameacha alama.
RIP JPM.
P
 
Lakini mbona hayo yote yalitafutiwa fedha na serikali ya Kikwete?, mimi ninachojua mradi wa ubungo ni mkopo fedha za worldbank na mradi uliandikwa na utawala wa Kikwete

Au kwa sababu ujenzi ulifanyika katika awamu ya Magufuli?

Mpishi na mpakuaji nani apewe sifa?
 
Tunamsifu aliyepata courage ya kutekeleza yote hayo kwakua hâta angeamua kutoyatekeleza hakuna ambacho angefanywa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…